JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Anord Patrick Kalinga (21) mkazi Mlevelwa, Kata ya Mdabulo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambae ni miongoni mwa vijana 100 kutoka kwenye familia duni walioibuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) amepongeza mradi huo kwa kumuona.
Anord alisema akiwa mdogo alipitia mazingira hatari na hata wakati mwingine alinusurika kifo kutokana na kazi ngumu za mateso alizokuwa akipewa na ndugu zake.
Akitoa shuhuda zake Alhamisi Machi 10, 2022 katika warsha ya Afya ya Akili katika Ukumbi wa Yatima Igoda, Wilaya ya Mufindi alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekata tamaa ya maisha hasa kutokana na mazingira magumu aliyopitia.
Hivyo, kupitia mradi huo wa YAM anaamini atasimama tena na kupambana kuwa na maisha bora kwani kwa muda wa mafunzo aliyopata kuna mambo mengi na mazuri amejifunza ambayo kwake ni kama mtaji.
"Kutokana na changamoto za maisha niliyopitia leo nimenifunza mambo mengi ya kunifanya kusonga mbele kimaisha na sasa sijuti tena kuwa kijana kutoka mazingira magumu ila naitumia fursa hii niliyofikiwa kusonga mbele," alisema Anord.
Malengo yake ni kwenda chuo cha ufundi wa magari na udereva ili kupitia kazi hiyo aweze kusimama kiuchumi.
Alisema mbali ya kuwa na maisha duni ila amekuwa nguzo ya familia kwa kutafuta fedha za kusaidia kuendesha familia yake na kupitia elimu ya ufundi atakayoipata ataweza kuondoa hofu ya kiuchumi inayomkabili kwa sasa.
Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dr Heriel Mfangano aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuitumia elimu hiyo kama plani B ya kuendelea na ndoto zao za kumiliki uchumi wao.
Alisema elimu ya ujasiriamali ni nguzo sahihi kwa vijana hao kuja kukuza uchumi wao na kuondokana na hali ya kujitenga, kuona hawana uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi.
Halmashauri ya Mufindi chini ya mradi wa FCWC na YAM kupitia ufadhili wa Finland utatelekelezwa kwenye kata za Luhunga, Ihanu na Mdabulo ni mradi wa miaka minne ulioanza mwaka jana na utekelezaji wake utakaonufaisha vijana na watoto wanaotoka katika familia duni zaidi ya vijana 770 katika vijiji 16.
Source: Matukio Daima Blog