Kijana aliyemdhalilisha askari polisi aliyebandua picha za Mtulia lazima akamatwe ili kulinda heshima ya jeshi letu

Kesho ataitwa white house apige selfie na baadae apewe wilaya kwa "ujasiri" wake! Awamu ya vi.wonder hii
 
Jeshi la Polisi nchini hata kama lina mapungufu yake lazima liheshimiwe. Haiwezekani mtu mimi namuita mhuni kuanza kujibizana hadharani na Askari Polisi kwa kumporomoshea matusi askari anayetekeleza wajibu wake kwa vile tu yeye ni mwanachama wa chama tawala.



Nategemea huyo kijana anayesikika kumdhalilisha askari kama bado hajakamatwa jeshi limtafute na kumfikisha kwenye vyombo husika ili kulinda heshima ya jeshi.

Iwapo polisi kwa kitendo kile itakaa kimya kuna hatari siku moja vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa kiburi cha kulindwa na dola, watajichukulia sheria mkononi na kumnyang'anya polisi silaha kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha usalama wa raia wasiohusika.

Huna tofauti na Kigwangala,unalifundisha kazi Jeshi la Polisi siyo? Halafu tusi ni lipi hapo na ni nani katukanwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom