Kijana aliyekaribia kumkamata aliyerusha Bomu Jumamosi alipigwa risasi.!

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
811
Majeruhii, Abdallah Hilali (39), aliyelazwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Center, amedai kuwa majeraha aliyopata miguuni yametokana na kupigwa risasi na polisi na kudondokewa na vipande vya bomu.

Alisema alikuwa nyuma ya jukwaa kuu akimsikiliza Mbowe na alipomaliza kuhutubia alishuka jukwaani kukusanya sadaka, ndipo alipoona mfuko wa mweusi mdogo wa plastiki ukipeperuka juu.“Nilidhani ni upepo unapeperusha kitu, lakini ghafla nilisikia kishindo na nikamsikia mama mmoja akipiga kelele kuwa aliyerusha mfuko anakimbia, nilipogeuka nikajikuta nipo chini,” alisema Hilali.

Alisema alipokuwa anaangalia aliona kijana mmoja amekaribia kumfikia aliyerusha bomu lakini ghafla akapigwa risasi na kuanguka chini na aliyekuwa anafuatia kwa nyuma naye akapigwa risasi akaona anaruka na kudondoka chini huku damu zikivuja.“Lakini mwisho wa yote kijana aliyerusha hilo fuko aliingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi. Mimi nilikuwa chini,” alisema Hilal mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipotembelea majeruhi hospitalini hapo..

Source,:Mwananchi toleo la leo

Maswali ya kujiuliza:

Kama siyo polisi, ni nani alimpiga huyu kijana risasi?! Kwa nini hajakamatwa hata sasa?. JE, kulikuwa na snipers wameandaliwa kumlinda mrusha bomu?!. Kama siyo polisi waliompiga risasi, je hawakumuona huyu sniper aliyepiga risasi watu wawili waliokuwa wakimkimbiza?. Polisi kwa uwingi wao pale uwanjani, je ni kweli walishindwa kumspot huyu mrusha bomu, tangu anafanya hilo tukio mpaka anaingia kwenye gari na kuondoka?.
 
Polisi ni wauaji, na sasa wamejitangazia kuwa adui namba moja wa raia na chadema

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
....kifupi ni hivii, hii nchi ni mali ya mfukoni ya watu wachache......amabo wataua, watawatoa kucha na meno bila ganzi ili kulinda mali yao hii (nchi) isichukuliwe na sisi tunaodhani kuwa, Tanzania ni mali yetu sote!
-watoto wao wanasoma nje
-wakiumwa wanatibiwa nje
 
Yule polisi aliyekataa kushiriki uovu unaondelea ndani ya jeshi la polisi pale Morogoro, alipoamua kutoa ushahidi wa tuhuma nzito za polisi aliambulia kukutwa chini ya daraja pale shan cinema eti "amejinyonga"! Ndo leo mnanitaka namimi niwaletee ushahidi wa polisi kuhusika kwenye tukio la Arusha ili nikutwe "nimejinyonga"?
 
Hizi ni siasa za majitaka tu, nani hawajui mwananchi uandishi wao wa kichochezi na kupidhisha mambo
 
Polisi walipoanza kumfukuzia mhalifu, wanachadema wakaanza kuwarushia mawe,unategemea nn hapo
 
Ni aibu kubwa kwa serikali Na jeshi la polisi!

Hata kama ingalikuwa kwamba Polisi hawakushiriki kwenye haya madhira yaliyowapata wananchi bado ni aibu kubwa inayofikia kiwango cha hawa viongozi kuwajibika.

Haiwezekani mchana kweupe mauaji yafanyike tena kwa Bomu Na silaha halafu mhalifu hata mmoja asikamatwe!
 
Police hawachomoki katika hili. Kwakweli leo sikuona uhalali wa polisi kupiga mabomu kiasi kile maana wananchi walishatawanyika lakini polisi wakawa wanatamba na magari yao huku wakipiga mabomu ya machozi na risasi ovyo na kuharibu magari yaliyokuwa yamepark na kuua mbwa kwa risasi waliokuwa wakikatiza mbele zao[ Hili nimeliona kwa macho yangu maeneo ya mianzini].
Kwakweli serikali sijui itaongea jambo gani mbele ya jumuiya za kimataifa. QUOTE THIS; Tanzania is no longer Island of peace
 
wajameni mambo mengine hayataki darubini kujua ukweli. kama waliweza kumuuwa mwandisi wa CHANEL 10 live, ndani ya mikono yao kwa kumchawaya nyama zake, vipi washindwe kufanya uhalifu huu Arusha?
 
wajameni mambo mengine hayataki darubini kujua ukweli. kama waliweza kumuuwa mwandisi wa CHANEL 10 live, ndani ya mikono yao kwa kumchawaya nyama zake, vipi washindwe kufanya uhalifu huu Arusha?

Kwa kweli inauma sana. Nadhani hakuna jeshi brutal kama la Tanzania Afrika nzima
 
utawala dhalimu unakaribia mwisho.
hata Farao, Herodi walikufa vifo vya kujitakia kwa kiburi chao
Huko tuendako wana CCM na Chadema watauwana wao kwa wao.
 
Hizi ni siasa za majitaka tu, nani hawajui mwananchi uandishi wao wa kichochezi na kupidhisha mambo

Please take note: huyu majeruhi aliongea mbele ya waziri wa serikali ya Tanzania. Kwa kuwa nahisi upo karibu na serikali. Nakuomba ukafanye verification kwa huyo waziri. Yaani wewe furaha yako ilikuwa haya yaliyosemwa yafichwe, tusiyajue?. Shameless guy
 
Majeruhii, Abdallah Hilali (39), aliyelazwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Center, amedai kuwa majeraha aliyopata miguuni yametokana na kupigwa risasi na polisi na kudondokewa na vipande vya bomu.

Alisema alikuwa nyuma ya jukwaa kuu akimsikiliza Mbowe na alipomaliza kuhutubia alishuka jukwaani kukusanya sadaka, ndipo alipoona mfuko wa mweusi mdogo wa plastiki ukipeperuka juu.“Nilidhani ni upepo unapeperusha kitu, lakini ghafla nilisikia kishindo na nikamsikia mama mmoja akipiga kelele kuwa aliyerusha mfuko anakimbia, nilipogeuka nikajikuta nipo chini,” alisema Hilali.

Alisema alipokuwa anaangalia aliona kijana mmoja amekaribia kumfikia aliyerusha bomu lakini ghafla akapigwa risasi na kuanguka chini na aliyekuwa anafuatia kwa nyuma naye akapigwa risasi akaona anaruka na kudondoka chini huku damu zikivuja.“Lakini mwisho wa yote kijana aliyerusha hilo fuko aliingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi. Mimi nilikuwa chini,” alisema Hilal mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipotembelea majeruhi hospitalini hapo..

Source,:Mwananchi toleo la leo

Maswali ya kujiuliza:

Kama siyo polisi, ni nani alimpiga huyu kijana risasi?! Kwa nini hajakamatwa hata sasa?. JE, kulikuwa na snipers wameandaliwa kumlinda mrusha bomu?!. Kama siyo polisi waliompiga risasi, je hawakumuona huyu sniper aliyepiga risasi watu wawili waliokuwa wakimkimbiza?. Polisi kwa uwingi wao pale uwanjani, je ni kweli walishindwa kumspot huyu mrusha bomu, tangu anafanya hilo tukio mpaka anaingia kwenye gari na kuondoka?.

nimefanya tasmini nimegundua kwamba.majeruhi wengi na waliopoteza maisha ni waislamu.kwa hiyo chadema ni chama cha waislamu?it was critical analysis.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom