Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,675
Mkazi wa Kibirizi Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Ndelagakula Romedafee (23) akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Kigoma kwa kumbaka mtoto wa kike.
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Mkazi wa Kibirizi Manispaa ya Kigoma/Ujiji , Ndelagakula Romedafee (23) kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtoto wa kike wa miaka minne baada ya kumrubuni kwa kumpatia Sh. 100.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, David Ngunyale baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kumtia hatiani.
Hakimu Ngunyale alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.
"Kutokana na mshtakiwa kufanya unyama huu wa kubaka mtoto mdogo hivi, mshtakiwa unatakiwa kuondolewa katika jamii na kupelekwa gerezani ili ukajifunze kuwa raia mwema katika maisha yako," alisema Hakimu huyo wakati akitupilia mbali utetezi uliotolewa na mshtakiwam huyo ili mahakama isimpe adhabu kali.
Awali upande wa mashtaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi wanne ambao bila kuacha shaka walithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alimbaka mtoto huyo.
Shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri ambaye ni mlalamikaji (mtoto huyo), alidai kuwa akiwa nyumbani kwao mshtakiwa huyo alimrubuni waende dukani akampe Sh. 100.
Tulipofika dukani mshtakiwa alinipa Sh. 100 nikajua kwa sababu tulikuwa tunakaa naye nyumba moja sikuwa na wasi wasi naye, tulipokuwa tunarudi nyumbani alinipeleka kwenye korongo, alinishika kwa nguvu na kunivua nguo zote kisha kunibaka,alidai na kuongeza kuwa:
Ndipo nikapiga kelele naumia naumia huku nikiwa nimechafuka kwa vumbi wakati mshtakiwa alivyokuwa ananigalagaza huku akinibaka."
Aliendelea kudai kuwa baada ya muda mfupi walitokea wasamalia wema wawili wakamkamata mshtakiwa huyo na kuwapeleka naye kwa baba yake.
Alidai baada ya kufikishwa kwao, mshtakiwa huyo alipelekwa kituo cha polisi ambako naye alipewa PF3kisha baba yake akampeleka Hospitali ya Mkoa Kigoma ya Maweni kwa matibabu.
Akijitetea mahakamani hapo baadaya kupewa fursa , Mshtakiwa huyo aliiomba impunguzie adhabu akidai baba wa mtoto huyo anamchukia ndiyo maana alimpeleleka mahakamani hapo.
Awali ilidaiwa na Mwanasheria wa Serikali, Robert Magige kuwa Aprili 4, mwaka huu mchana katika maeneo ya Kibirizi, mshtakiwa alitenda kosa hilo.