Kijana akamatwa kwa kughushi nyara za Serikali na kuwauzia watu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,902
2,000
6b3c0ad318b1bb8dadee727927a2a081


Jeshi la Polisi Mkoani Njombe linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ford Abel mwakatundu (28) mkazi wa Makambako mkoani humo kwa makosa ya kukutwa na nyaraka za serikali.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Salum Hamduni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kijana huyo anashikiliwa kwa makosa hayo kinyume na taratibu za kisheria.

“Mnamo Aprili 22 majira ya saa 12:30 huko Makambako alikamatwa, Ford Abel Mwakatundu mwenye umri huo mkazi wa Mwembetogwa Makambako kwa kosa la kughushi nyaraka mbali mbali za serikali ikiwemo leseni za kuendesha magari,Tin Number, Bima za Magari pamoja na nyaraka za Sumatra zinazohusiana na Safari za Mabasi na Magari madogo ya biashara,”Amesema Kamanda Hamduni

Aidha, ameongeza kuwa nyaraka hizo alikuwa akighushi na kuziuza kwa watu mbali mbali kwa kiasi cha Tsh. 100,000/= kwa lengo la kujipatia kipato.

Hata hivyo, Kamanda Hamduni ameongeza kuwa upelelezi bado unaendelea na atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Njombe, Musib Shaaban ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia za kutumia njia za mikato kutafuta kipato kwa kuwa njia hizo zimekuwa zikikwamisha juhudi za serikali.
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,943
2,000
Kijana akamatwa kwa kughushi nyara za Serikali na kuwauzia watu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom