Kiiza alalamika kudhulumiwa ufungaji bora kombe la ASFC

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Hamisi Friday Kiiza amesema kwamba yeye ndiye mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) 2016.

Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo, mshambuliaji huyo wa Uganda amesema kwamba alishangaa jana TFF kumtaja mchezaji wa Ndanda FC, Atupele Green Jackson ndiye mfungaji bora.

“Nimeshangaa sana, mimi ndiye mfungaji bora, nimefunga mabao matano jumla katika mashindano haya hadi tunatolewa Robo Fainali,”amesema Kiiza.



Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza amelalamikia kudhulumiwa ufungaji bora wa Kombe la ASFC

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, amesema alifunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Burkina Fasso mjini Morogoro na mawili mengine dhidi ya Singida United na moja dhidi ya Coastal Union, yote Dar es Salaam.

Akizungumzia madai ya Kiiza, Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Jemadari Said Kazumari amesema kwamba kwa mujibu wa rekodi walizonazo, Atupele ndiye aliyefunga mabao mengi.

“Kwa mujibu wa rekodi zetu, Atupele ndiye mfungaji bora, tena si kwa tu kufunga mabao mengi kwenye mashindano, hata kufunga mabao mengi katika mechi moja. Ndiye mchezaji aliyefunga mabao manne kwenye mechi moja,”amesema Jemadari.

Michuano ya Kombe la TFF ASFC jana imefikia tamati kwa Yanga kutwaa ubingwa, ikiifunga Azam FC mabao 3-1 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Aidha, mbali na Atupele kutangazwa mfungaji bora jana, kipa wa Azam FC, Aishi Manula ameshinda tuzo ya mlinda mlango bora na beki wa Yanga, Juma Abdul ndiye mchezaji bora wa mashindano.


Atupele Jackson baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya mfungaji bora wa Kombe la ASFC jana

Kiiza mbali na kuikosa tuzo ya ufungaji bora wa Kombe la ASFC, pia alizidiwa kete na mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe katika ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
duh labda sijaelewa vzuri " “Kwa mujibu wa rekodi zetu, Atupele
ndiye mfungaji bora, tena si kwa tu
kufunga mabao mengi kwenye
mashindano, hata kufunga mabao
mengi katika mechi moja. Ndiye
mchezaji aliyefunga mabao manne
kwenye mechi moja,”amesema
Jemadari.


Kwa hyo basi mwenye magoli mengi kwnye mech moja ndio mfungaj bora sio? daah kwa hili TFF mjipangee sio hoja kbsa
 
duh labda sijaelewa vzuri " “Kwa mujibu wa rekodi zetu, Atupele
ndiye mfungaji bora, tena si kwa tu
kufunga mabao mengi kwenye
mashindano, hata kufunga mabao
mengi katika mechi moja. Ndiye
mchezaji aliyefunga mabao manne
kwenye mechi moja,”amesema
Jemadari.


Kwa hyo basi mwenye magoli mengi kwnye mech moja ndio mfungaj bora sio? daah kwa hili TFF mjipangee sio hoja kbsa
hili ni janga kubwa......
 
Huyu mwandishi ameandika maelezo mareeefu, ila cha ajabu ameshindwa kutuambia kua huyo Atupele alikua na goli ngapi tulinganishe na za Kiiza. Bila kujua magoli yaliyofungwa na hawa wachezaji itua hamna maana ya kuchangia.
 
Atuambie basi huyo Atupele kafunga magoli mangapi ili tuanze kujumlisha na kutoa tutafute jawabu.... Figisu tupu hapa
 
Hivi kwanini kwenye soccer wanachukulia ubora Kuwa quantity badala ya quality? Yaani anyefunga mengi ati ndiye bora.. .wakati pengine mtu kafunga magoli 10 yote hata hayana mvuto.. ni ile anatengewa tu anamalizia.. Ilhali kuna mtu kapiga goli 6..yaani magoli yanavutia.. Kama yale ya Ibracadabra yaliyokaa ki-kung fu kung fu..au kasomba kijiji kapiga vyenga afu kafunga.. Au kaunga krosi design ya kichwa kama cha Van persie world cup iliyopita..sasa kwanini huyu asiwe ndiye mfungaji bora?
 
Hivi kwanini kwenye soccer wanachukulia ubora Kuwa quantity badala ya quality? Yaani anyefunga mengi ati ndiye bora.. .wakati pengine mtu kafunga magoli 10 yote hata hayana mvuto.. ni ile anatengewa tu anamalizia.. Ilhali kuna mtu kapiga goli 6..yaani magoli yanavutia.. Kama yale ya Ibracadabra yaliyokaa ki-kung fu kung fu..au kasomba kijiji kapiga vyenga afu kafunga.. Au kaunga krosi design ya kichwa kama cha Van persie world cup iliyopita..sasa kwanini huyu asiwe ndiye mfungaji bora?

Tofautisha mfungaji bora na mchezaji bora.

Kama wakiwa idadi ya magoli ni sawa, hapo ndo zinakuja issue za quality.
 
Soma maelezo yangu uelewe mkuu... Mfungaji bora ni yule anayefunga magoli bora sio aliyefunga magoli mengi..hii ndiyo point yangu

Nimeelewa ila nimeshindwa kukumbuka vizuri.

Aliyefunga magoli mengi anaitwaje?
 
duh labda sijaelewa vzuri " “Kwa mujibu wa rekodi zetu, Atupele
ndiye mfungaji bora, tena si kwa tu
kufunga mabao mengi kwenye
mashindano, hata kufunga mabao
mengi katika mechi moja. Ndiye
mchezaji aliyefunga mabao manne
kwenye mechi moja,”amesema
Jemadari.


Kwa hyo basi mwenye magoli mengi kwnye mech moja ndio mfungaj bora sio? daah kwa hili TFF mjipangee sio hoja kbsa[/QUOT
Atupele Ana magoli 5 Kiiza Ana magoli 5, kwa nini Kiiza aseme yeye ndo mfungaji bora??
 
Uongozi wa simba inabidi uingilie kati.
Simba SC watulie tu; kwanza Kiiza walimuokota kijiweni hivyo hana issue ya maana, pili hata mwandishi kamtambulisha Kiiza kuwa ni mchezaji wa zamani wa Yanga bila kuitaja Simba.

Nanukuu:

'Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, amesema alifunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Burkina Fasso mjini Morogoro na mawili mengine dhidi ya Singida United na moja dhidi ya Coastal Union, yote Dar es Salaam'.

Mwisho wa kunukuu.

Kwa utambulisho huo hata Kiiza mwenyewe kaikana Simba na akaona ni heri aitwe kwa jina la mchezaji wa zamani wa Yanga (iliyomuheshimu na kuagana naye kwa Amani) ambapo anapata heshima zaidi kuliko kuitwa mchezaji wa Simba ambayo inamtambua kama mtoto wa kijiweni aliyeokotwa na kujikuta Msimbazi na sasa hahitajiki tena.

What a stinking end of Hamis Kiiza at Msimbazi street!
 
Soma maelezo yangu uelewe mkuu... Mfungaji bora ni yule anayefunga magoli bora sio aliyefunga magoli mengi..hii ndiyo point yangu
Tofautisha mfungaji bora, na goli bora jombaa ..

Mfungaji bora >ni idadi ya magoli mchezaji anayofunga haijalishi ameibia, amefunga na mkono n.k..

Goli bora > goli alilofunga mchezaji na likawa la kipekee baada ya kupigiwa kura.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom