Kiini macho cha Kamati ya January Makamba na Dowans

Whether ni kwa kusukumwa na dhamira ya kweli au kwa unafiki hoja ya Makamba Jr ni ya muhimu. Tatizo ni kwamba hana mamlaka ya kumuamuru WAziri kuwasilisha hoja au kauli bungeni. Kwa hiyo pamoja na uzito wa hoja alizotoa; zitaishia kabatini tu.
 
katumwa huyu wameanza kugeukana wao kwa wao, Bado Chenge na AG nao watatoa yao, si unaona Mkuu JK ameshatoa yake EI haijui DOWANS imeanzisha na nani, hivi pale ikulu hakuna mtu anyejua kujibu hoja muhimu kwa kumweleza mkuu wetu kuwa atawashagaza sana wananchi akisema kuwa hawajui wamiliki wake, hivyo anadhalilisha UWT kwa kuwa hawako makini hata nchi yaweza uzwa bila kujua
Wanajua vizuri wanachofanya they are just playing mind games
 

Huu ndio uendawazimu wenyewe!
Huwezi tu kuandika 'crap' bila kuonesha hoja ambayo hujakubaliana nayo unayohisi ni 'crap'. Jibu hoja kwa hoja, kama huna hoja just shut up!
 
Nimependa hoja ya January! Kama hakuna kitu kingine behind the scene basi wabunge wawe mle mjengoni kwa maslahi ya taifa na kuweka itikadi zao kando. Kwa muda nakupongeza Makamba January.
 
Pongezi kwa January.....japokuwa doubts ni nyingi na wengi tunahisi umetumwa lakini una hoja ya msingi na maswali muhimu sana kwa Mh Waziri.....tunaomba atakapokujibu utushirikishe pia.......:coffee:
 
Ayaaa!!! Naona mnakuja kwa style ingine ili muweze kujisafisha na kutoa majibu ya uongo juu ya DOWANS.
Muulizeni January Makamba ni nani aliyemfadhili kwenye kampeni za ubunge wake mpaka akaweza kumwondoa aliyekua mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini?...Na je aliyemfadhili ni mmiliki au siyo mmiliki wa DOWANS??

CCM nimeshapoteza imani nao siku nyingi ....msidhani tanzania ya sasa ni ile ya miaka ileee unadanganya wananchi wanaendelea kusema ndio mzee!!!!......Nowdays we are watching the game very careful.

Hapo ni sawa na mwanamke anayepokea hela halafu akija upande wa pili anajikosha simtaki yule mwanaume
 
hii ni mpya wala sishangai maana hawa ni vinyonga tu leo hivi kesho lingine kweli nchi yetu wametuibia vingi sana jamani tusirudi nyuma mpa kielewe nahuu ndio anguko la CCm kama KANU ilivyo anguka tumuombe Mungu azidi kuwapatia ukpofu wakuendeleza kukivulunga chama chao ni hatua nzuri sana kwa upinzani CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEE! songa mbele ukombozi uko karibu .:clap2:
 
embu 2we mahakimu na kazi ye2iwe yakutoa maamuzi kulingana na ushaidi atakao toa huyu ndugu makamba januari n 2cwe mahakimu2nao kurupuka kutoa hukumu..thnkers always thnk n nt kuropoka...
 
Mbunge wa CCM aibua siri nzito Dowans, IPTL Monday, 07 February 2011 21:51
AHOJI UADILIFU WA WANASHERIA WALIOITETEA TANESCO
Ramadhan Semtawa
MBUNGE wa Bumbuli, January Makamba, amemwandikia waraka Waziri wa Nishati na Madini kumtaka afafanue bungeni mambo kadhaa yanayohusu wizara hiyo, likiwamo sakata la Kampuni ya Dowans.Sehemu ya waraka huo imeibua jambo kwa mwanasheria wa Tanesco aliyesimamia kesi ya Dowans ambapo mbunge huyu anaeleza jinsi alivyocheza karata pande zote mbili kwa kushauri mkataba dhidi ya kampuni hiyo uvunjwe huku upande mwingine akiisifia na kuiombea mkopo wa Sh 20 bilioni katika Benki ya Stanbic.

Katika waraka huo wenye kichwa cha habari, "Yah: Taarifa ya Serikali Bungeni kuhusu Umeme Nchini," Mbunge Makamba ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba anataja mambo hayo kumi ambayo Waziri William Ngeleja, anapaswa kuyafafanua kwa umma kupitia Bunge.

Waziri Ngeleja alipoulizwa kwa njia ya simu alikiri kuupata waraka huo na kuongeza, "Lakini, hadi sasa sijaufanyia kazi. Upo ofisini nimeambiwa umefika."

Wakati Ngeleja akikuna kichwa, Makamba katika waraka huo ambao nakala imeenda kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema:, "Kuhusu shauri la Dowans, Watanzania wameshuhudia kioja cha mawaziri wa serikali kujibizana na kupingana kwenye magazeti kuhusu malipo ya tuzo ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) kwa kampuni ya Dowans."

...Taarifa ya Serikali bungeni kuhusu jambo hili ni muhimu ili kuweka bayana kwa Watanzania kwamba ni wakati gani, kwa njia gani na kwa jinsi gani Serikali inawasiliana na umma ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi na sisi wabunge kuhusu msimamo wa Serikali kwenye masuala mbalimbali."

Mwanasiasa huyo kijana aliongeza, "Mheshimiwa waziri, mnamo tarehe 6 Januari 2011, ulizungumza na waandishi wa habari na kueleza Serikali inajipanga kuilipa Dowans tuzo iliyoamuliwa na ICC."

"Lakini, kwa kuwa mzigo huu ni mzito kwa umma..., kumekuwa na fikra ikiwemo pendekezo la kamati ya wabunge wote wa CCM kwamba ni muhimu kutumia mianya ya kisheria iliyopo kupinga rasmi kutekelezwa kwa hukumu hiyo."

Akionyesha msisitizo katika hilo alisema, kwa kuwa hiyo imekwishasajiliwa Mahakama Kuu nchini na huku kila siku inayopita faini kwa Tanesco huongezeka kwa Sh 17milioni ni wakati wa Serikali kueleza ni lini itapeleka pingamizi la hukumu hiyo.

"Na hatua hii inamuweka wapi Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na tamko lako la Januari 6, 2011 kwamba kupinga utekelezaji wa hukumu ya ICC ni kupoteza muda," alihoji Makamba.

Akikazia katika Dowans, Makamba aliibua hoja akisema, katika viambatanisho vya hukumu ya ICC kama ilivyosajiliwa Mahakama Kuu zipo nyaraka zinazoonyesha mwanasheria aliyeishauri Tanesco kuvunja mkataba na kampuni hiyo akisema haukuwa halali na kusingekuwa na madhara kwa kuuvunja, ndiye huyo pia aliyeishauri Benki ya Stanbic kutoa mkopo wa dola za Kimarekani 20 milioni kwa Dowans.

"Na ndiye huyo huyo aliyeiwakilisha Tanesco kwenye kesi iliyofunguliwa na Dowans, kesi ambayo imetokana na ushauri wake... Na baada ya hukumu, ndiye huyo huyo kwa mujibu wa maelezo yako aliyekuja kutoa ushauri kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuilipa Dowans baada ya hukumu," aliibua hoja hiyo nzito na kuongeza,

"Mheshimiwa Waziri, jambo hili likibaki hivi hivi bila maelezo inaweza kujengeka sura kwamba Serikali ilikosa umakini kwenye jambo hili zima na maadili hayakuzingatiwa... Itakuwa vyema kama taarifa ya serikali ikaeleza ni wanasheria gani waliotumiwa na Tanesco kwenye kila hatua shauri la Dowans."

Katika barua hiyo yenye kurasa tano, Makamba alitaka taarifa hiyo itaje wanasheria walioshiriki kuanzia kwenye ushauri kabla ya kuvunjwa kwa mkataba hadi ushauri baada ya kesi kuamuliwa na kiasi cha fedha walizolipwa kwa kila hatua, na utaratibu uliotumika.

Alienda mbali akisema, katika kuondoa Watanzania wasiwasi ambao wanaamini Tanesco ilishindwa kwenye kesi hiyo ya Dowans kutokana na upungufu wa weledi kwa wanasheria walioiwakilisha kwenye kesi hiyo, "Nashauri taarifa ya Serikali ieleze utaratibu uliotumika kuwapata wanasheria walioiwakilisha Serikali na Tanesco kwenye mashauri yaliyofunguliwa."

Amtaka atoe maelezo kesi mbili za IPTL
Mbunge huyo alisema anamsihi waziri atoe pia maelezo kuhusu kesi mbili zinazohusiana na mkataba wa uzalishaji wa umeme wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Makamba anataka waziri aeleze mchakato wa kesi hizo zilizofunguliwa na Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong dhidi ya Serikali na Tanesco kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kesi za Uwekezaji (ICSID).

Makamba alifafanua, "Kesi hizo ni ICSID No ARB/10/20 dhidi ya Tanesco iliyofunguliwa Oktoba Mosi, 2010 na ICSID No ARB/10/12 dhidi ya Jamhuri ya Muungano iliyofunguliwa Juni 11, 2010, zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa umma na zinaweza hata kuigharimu Serikali pesa nyingi kuliko zinazodaiwa katika kesi ya Dowans."

Alisema taarifa ya Serikali bungeni kuhusu kesi hizo mbili itasaidia Watanzania kufahamu:, "Nini kinadaiwa dhidi ya Tanesco na Serikali pamoja na maandalizi ya Serikali kushinda kesi hizi ili kuepukana na marudio ya zahama ya Dowans."

Katika kuonyesha msisitizo, mbunge huyo, alimtaka waziri kama ataona inafaa awajulishe Watanzania sababu za Serikali kutotoa taarifa za kesi hizo mbili muhimu kwa maslahi ya umma hadi sasa.

..Ahoji matamko sita ya Serikali kumaliza tatizo la umeme

Akizungumzia zaidi ahadi na matamko ya kumaliza tatizo la umeme, Makamba alisema tangu mwaka 2006 hadi sasa zimetoka ahadi na matamko sita ya Serikali ya kumaliza tatizo la mgawo wa umeme nchini, lakini hadi sasa bado mgawo unaendelea.

Makamba aliweka bayana kwamba, ingawa kila kunapotokea mgawo kumekuwa na maelezo na sababu mbalimbali, lakini ahadi hizo mara nyingi zimekuwa zikijirudia na kuongeza:, "Wewe (Ngeleja) mwenyewe umetoa ahadi kadhaa za kumaliza tatizo hili, lakini ahadi hizo hazikutumia."

Alisema matokeo ya hali hiyo ni wananchi kupoteza imani na uwezo wa Serikali yao kutatua tatizo la umeme nchini na hata matatizo yao mengine na kuonya:, "Kuna gharama kubwa kwa wananchi kupoteza imani na Serikali yao."

"Mimi naamini kwa dhati kabisa, kama Serikali ikitoa tamko la dhati kabisa bungeni linalobainisha kwa kina na uwazi sababu za ahadi hizi za mara kwa mara basi tutakuwa tumepiga hatua kwenye kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali yao," aliongeza.

IPTL inavyoigharimu Serikali
Akikazia katika IPTL, alisema mtambo unaozalisha umeme wa kutumia mafuta mazito aina ya HFO unaigharimu Serikali mabilioni ya shilingi kwa mwezi licha ya kuzalisha umeme chini ya nusu ya uwezo wake, kutokana na uhaba wa na bei kubwa ya mafuta.

Mbunge huyo alisema kutokana na gharama hizo kubwa, Serikali imeamua kulipia gharama zote za kubadilisha au kukarabati mitambo hiyo ambayo si mali yake bali IPTL ili itumie gesi asilia badala ya mafuta mazito ya HFO.

"Mwaka 2006, Serikali iliingia mkataba na Kampuni ya Alstom Power Rentals kuzalisha umeme mkoani Mwanza kwa kutumia mitambo ya mafuta, kutokana na shida na gharama ya upatikanaji mafuta na kuyasafirisha mpaka Mwanza, mtambo huo haukutumika kuzalisha umeme hata siku moja ndani ya miezi 12 ya mkataba, zaidi ya saa 20 tu kwa ajili ya majaribio kabla ya mtambo kukabidhiwa kwa Serikali," alisema na kuongeza,

"Kwa kifupi ni kwamba kampuni hiyo ililipwa kiasi cha dola za Marekani 1.7 milioni (takriban Sh 2.5bilioni), kwa mwezi za bure, bila kuzalisha umeme wowote. Ili wananchi waone kwamba Serikali yao ina uchungu na rasilimali za umma, nashauri taarifa ya Serikali ieleze hatua za uwajibikaji kwa hasara hii ya takriban dola 20 milioni."

Mzimu wa mikataba ya umeme Tanesco imekuwa ikiitikisa nchi ambayo mwaka 2008, ilisababisha Baraza la Mawaziri la kwanza la Serikali ya awamu ya nne kuvunjwa, baada ya Kamati Teule ya Bunge kubaini mkataba kati ya Kampuni ya Richmond na shirika hilo ulikuwa na walakini.

Mwananchi 8 Feb 2011

a real smart crap!!!
 
what makes it being crap?
Unataka mpaka CDM wakisema ndio manakubali?
tunapingana kwa hoja sio chuki binafisi zisizoweza kujenga nchi yetu

remind us of a day when CCM and it's affiliates stood up and said something genuine and useful.

this is mind game at it's most baby.

hatujaisahau ile namba ya Finland ----- +3588976578
 
Unaifahamu job description ya msaidizi wa hotuba za rais??????? Je unafahamu january sasa ana dhamana ya wananchi wa bumbuli??
aache upuuzi wake.
Yeye si alikuwa ikulu, inamaana hakuwahi hata kusikia hiyo dili wakati inapita? Kwa nini hakushauri wakati huo? Anaona hali imebadilika sasa hivi ndo anatafuta sapoti ya umma kama walivyofanya uvccm. Wanatakiwa washauri kabla sio kusubiri watu waanzishe ishu ndo wao wadandie.
 
Kama kweli Makamba ameandika haya na atayafuatilia basi kuanzia leo nitakuwa shabiki wake kwenye hoja zote bungeni. Huyu anajua siri nyingi za serikali kwa sababu alikuwa kwenye jumba.
CCM ilipata heshima kubwa katika serikali ya awamu ya nne kipindi cha miaka 5 ya kwanza baada ya wabunge wake kutokuwa na msimamo moja na serikali. Hata sasa wabunge wa CCM ambao watawakilisha maslahi ya serikali badala ya yale ya wanainchi wake watakuwa na wakati mugumu watakaporudi kuomba kura tena.
 
Hakuna kitu huyu katumwa na CCM

Huyu ni mwizi

SAMAHANI MLETA MADA UNAWEZA KUPELEKA HII KITU KWA MICHUZI?? MAANA HAPA SIO MAHARI PAKE!!!
 
remind us of a day when CCM and it's affiliates stood up and said something genuine and useful.

this is mind game at it's most baby.

hatujaisahau ile namba ya Finland ----- +3588976578


mKUU UMENIKUMBUSHA HUYU JAMAA NA SHAMTE HAWANA TOFAUTI, LISA JE??
 
embu 2we mahakimu na kazi ye2iwe yakutoa maamuzi kulingana na ushaidi atakao toa huyu ndugu makamba januari n 2cwe mahakimu2nao kurupuka kutoa hukumu..thnkers always thnk n nt kuropoka...

nakuunga mkono mkuu comred,,,
 
January Makamba hana lolote baali anapiga siasa tu na kutafuta umaarufu. Yeye ni mmoja ya wababaishaji ndani ya Chama Cha Mafisadi-CCM.
Hii ni kujaribu kutengeneza mazingira ya kuwafanya Watanzania wawe na Imani na CCM which is too late. Yote hii ni danganya toto.
Upinzani wa kweli na hoja za mashiko ziko CHADEMA.
 
huyu dogo anatafuta uwaziri kwa nguvu sasa ameamua kudil na ngeleja waache wapambane yetu macho
 
Back
Top Bottom