Kiini cha vurugu Zanzibar ni Udini si tu Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiini cha vurugu Zanzibar ni Udini si tu Muungano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Raiamwematz, Jun 1, 2012.

 1. Raiamwematz

  Raiamwematz Senior Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  HATUWEZI kuamini kwamba kiini cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki hii, Unguja visiwani Zanzibar ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Kimsingi, Muungano hauna umbile linaloweza kuonekana na kwa maana hiyo, Muungano hauwezi kushambuliwa kwa kuchomwa moto au kuupiga mawe. Muungano ni muundo wa kifikra na kisheria, unaotenganisha au kugawa mamlaka baina ya pande zilizoungana lakini katika taswira ya umoja.
  Kwa hiyo basi, suluhu ya kutatua kero za Muungano au kujadili uwe katika muundo gani haitokani na vurugu za aina yoyote bali suluhu inapatikana kwa kushindana kwa hoja. Ni nguvu ya hoja ndiyo inayotibu kasoro zinazoweza kujionyesha katika Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar.
  Na hata wito wa upande mmoja wa wananchi kutaka kujitenga na Muungano, unapaswa kusukumwa kwa nguvu ya hoja. Wito wa dhati wa kutaka kujitenga haupaswi kusukumwa kwa vitendo vya vurugu. Tena vurugu zenye mwegemeo wa kidini.


  Ni kwa mtazamo huo, tunaamini kwamba vurugu za Zanzibar si ishara ya kero zinazotokana na Muungano. Kiini cha vurugu za Zanzibar ni watu wa dini moja kukosa uvumilivu kwa watu wa dini nyingine, ingawa dini yao wenyewe bila shaka hairuhusu uhalifu wa aina yoyote dhidi ya watu wengine.
  Kwa hiyo, vurugu za Zanzibar kiini chake ni chuki binafsi ya watu fulani waliomo ndani ya kikundi kinachoitwa Uamsho. Ni chuki ya watu fulani ndani ya kikundi hicho ambayo haina utetezi wowote ndani ya dini ya wanakikundi.


  Hata kama kwa bahati mbaya Zanzibar ikijitenga kama ambavyo ndoto za wafanya vurugu hao zitatimia, bado kwa matakwa ya busara visiwa hivyo vitahitaji kuendeshwa kwa kushirikisha watu wengine nje ya eneo hilo.

  Na kwa kweli, watu hao wa nchi nyingine maana yake ni watu wa dini nyingine. Tumekwishakuona kwa mfano, nchi zenye viongozi wakuu wenye mwegemeo wa kidini zinavyoendesha uchumi wake kwa kushirikisha nchi zisizo za kidini.


  Kwa vigezo vyote, vurugu za Zanzibar msingi wake ni ubaguzi wa kidini. Vigezo hivyo ni pamoja na hatua ya wafanya vurugu kuchoma makanisa. Kama kweli walilenga kufanya uharibifu usiojenga taswira ya ajenda yao ya siri ya ubaguzi kwa nini hawakuchoma nyumba za ibada za dini yao?


  Ikumbukwe kuwa, hata kwa upande wa Tanzania Bara kuna maeneo yenye wakristo wengi na asilimia ndogo sana ya Waislamu. Lakini pamoja na tofauti hiyo, Wakristo walio wengi wameonyesha mfano mzuri wa kuvumilia na kuheshimu dini za wenzao kama ambavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka.


  Na kwa hiyo, tungependa kwa upande wa Zanzibar kuendeleza moyo wa subira na uvumilivu kwa watu wa dini tofauti. Tungependa Wazanzibar wachache wenye ubaguzi wa kidini angalau kuheshimu mawazo ya Wazanzibar wenzao walio wengi ambao waliridhia Katiba mpya ya Zanzibar kutoifanya Zanzibar kuwa visiwa vyenye mlengo wa kidini.

  Source: Raiamwema: Raia Mwema - Kiini cha vurugu Zanzibar ni Udini si tu Muungano
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Tumechoshwa na hizi mada za kiuchochezi,

  MOD tafadhari futeni hii post na mpigeni BAN huyu mtu.
   
 3. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,519
  Likes Received: 10,437
  Trophy Points: 280
  wewe ndio upigwe ban mdini mkubwa we. Raia mwema inasomwa na viongozi wote Tanzania na akina Msekwa wanaweka makala zao mle na haipigwi ban na serikali. Ficha udini wako.
   
 4. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 5. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndio maana mpaka umri huo bado hujui mbele wala nyuma, yote hii ni sababu ya kufatilia viuchonganyishi tu. Ukuda dot Ushankupe

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...