Kiini cha Tatizo na Suluhisho la Utoro wa Wabunge - Kwa Mheshimwa Spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiini cha Tatizo na Suluhisho la Utoro wa Wabunge - Kwa Mheshimwa Spika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Jul 24, 2012.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika.

  Pole kwa majukumu mazito!

  Kiini cha tatizo la utoro, na suhisho, ila ufanye kwa data/takwimu ambazo unazo kwenye taasisi yako.

  ->Ukiangalia statistics zako za mahudhurio ya wabunge kwa muda mfupi tu... utapata jibu lake. Ila kwa kuwa hujaangalia hili naomba nikuombe ufanye yafuatayo:-
  1. Angalia trend ya mahudhurio ya vikao vya bunge kuanzia vinapoanza hadi vinapomaliza... najua utapata patern kwamba kadri siku zinavyoenda wabunge wanapungua kuhudhuria.
  2. Angalia trend hiyo hapo juu kwa vikao vya majuma mawili na vile virefu yaani vya bajeti, utaona vya majuma mawili mahudhurio sio mabaya sana kivile.
  3. Angalia trend ya miaka mitatu hadi mitano iliyopita, ukipenda hata wakati wa kipindi cha Mr. Speed & Standard.
  4. Angalia trend ya michango ya kuongea vs michango ya maandishi... ipi mingi? jibu unalo... things has changed wabunge siku hizi wanapenda kuchangia kwa maandishi... hata wao wanaboreka kusema.

  -->Utakayogundua ni haya:-
  1. Kadri vikao vinakuwa virefu wabunge wanachoka... hivyo wana-sepa! Hata ingekuwa mimi siku 70-90 huku dodoma nafanya nini? Sina shughuli nyingine?
  2. Kwa kuwa wabunge siku hizi wana-prefer kuchangia kwa maandishi nini kifanyike.... tizama hapa chini.

  --->Soluhisho ya mahudhurio mabovu....
  1. Punguza urefu wa vikao... peopla are not ready to sit somewhere for 70-90 days..... kama ni-hela wanazoangalia wape the same money kwa muda mfupi utaona vikao vitakavyokuwa effective....
  2. Hata wabunge wengine wanachoka salamu za shukrani.
  3. Kama harusi zinavyoanza kuboa na utaratibu wa bunge sharti ubadilike kuendana na wakati... kuna wakati mtabaki wenyewe.
  4. Kwani kwa nini kiti kinakaliwa na watu wanne sijui watano? kwani wenye mh. spika uko Dodoma kwa siku zote 70-90? Si una-sepa mara kwa mara? ila tu kwa kuwa wewe.... unawanaokaimu nafasi yako ndio maana hautoni tatizo?

  Wasalamu
   
Loading...