Kiini cha Mgogoro ndani ya CCM ni nini hasa? Je wanaweza kupatana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiini cha Mgogoro ndani ya CCM ni nini hasa? Je wanaweza kupatana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 23, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [h=6]Kwa maoni yako kiini cha mgogoro ndani ya CCM ni nini hasa? Ni watu? maslahi yanayogongana? Nafasi na matamanio ya nafasi? Ni mgongano wa itikadi na fikra? ni kutoridhika au kuridhishana? au hasa ni kitu gani? Kwa miaka zaidi ya mitano sasa tumeona jinsi ambavyo kujengeka kwa pande mbili (au tatu) ambazo zikiwa aidha zimefungamana na watu fulani fulani au zikiwa zimeshikilia fikra fulani. Pande hizi zinaonekana kuwa mbali zaidi kutoka nyingine lakini zote zikiwa zimevaa magwanda ya kijani na njano.

  Umoja wa wana CCM unaonekana katika kuwa katika chama kile kile na kuvaa mavazi yale yale lakini siyo umoja unaotokana na kukubaliana kuhusu mitazamo, itikadi, au mwelekeo - uwe wa nchi au wa chama. Umoja huu wa watu wenye maslahi tofauti unaweza kudumu vipi? Je yawezekana kuwaweka mbuzi na chui kwenye zizi moja na kuamini kuwa watakuwa na umoja ati a. wako zizi moja na b. kwa sababu wote wana njaa? Kwani anachokula mbuzi ndicho anachokula chui? Katika mazingira hayo ni yupi ambaye ataishi kwa wasiwasi wa kudumu juu ya salama yake?

  Kuna umoja gani kati ya Bwana na kijazi wake au Mtumwa na mmiliki wake? Hata kama mtumwa ataishi kwenye nyumba moja na bwana wake na kuingia kwenye gari lake na hata kuvaa nguo za fahari kuliko maskini aliye huru kule nje je ameacha kuwa mtumwa? Je anaweza kudai kuwa ana "umoja" kwa kadiri ya kwamba maisha yake yote yanaamuliwa na yule mtu mwingine? Umoja na amani inayojengwa kutokana na dhulma na ukandamizaji (injustice and oppression) unaweza vipi kudumishwa bila kutenda haki na usawa? Na inakuwaje kama ukandamizaji huo au dhulma hiyo inatokana na nguvu isiyoonekana kwa macho wala kushikika kwa mikono (unseen and an intangible force) lakini ambayo matokeo yake yanaonekana a.k.a ufisadi? Je amani na umoja wa aina hiyo unawezekana kweli bila kushughulikia nguvu hiyo kuu?


  Unafikiri mgogoro huu (ukiwa na chanzo chochote) ndani ya CCM utaisha kwa kujivua gamba au kutangaza kusameheana? Kweli unaweza kumaliza kwa kupigiana kura ya umoja au kuamua kuyaacha 'ya kale' yapite? Ni kweli kuna watu wanaamini kabisa kuwa vikao ambavyo vimefanyika na vinaendelea kufanyika vitaweza kumaliza mgogoro huu? Au utamalizika kiukweli pale ambapo Mkutano Mkuu wa CCM (chombo cha juu kabisa cha maamuzi) kitakapokuja kukaa na kufanya kile ambacho umekwepa kwa miaka sita sasa!? Maana kama vidonge, sindano, chanjo na kufukiza hakufanyi kazi labda yapasa mtu kupelekwa kwenye kitanda cha kisu na kupigwa nusu-kaputi?
  [/h]
  Yawezekana basi mgogoro huu ni mgogoro wa kudumu usiomalizika kwa vikao, vitimbi au vitisho isipokuwa kwa kumeguka kwa CCM na kuamua kuanzia upya?
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji na wewe unavutika na sarakasi za CCM hakuna lolote hapo mie nachukulia kama mchezo wa ze comedy.

  Hakuna kiongozi wa CCM ambaye ana moral authority to say anything NEC au CC badala yake watu wanachotwa akili away from tuhuma za ufisadi zinazowaandama CCM.
   
 3. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Nionavyo, mgogoro huu unahusiana na mategemeo ambayo hayakutimia, kuangushana -letting someone down- kiahadi, kushindwa kazi na kusingiziana, unafiki na kuoneana aibu, kutokubali ukweli wa mambo, ulafi wa madaraka, n.k.

  ...Kwasasa hamna wa kuwapatanisha -watu wanajaribu inashindikana-, ila Mkapa anaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa, kama akishawishiwa na wakamsikiliza.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa ufupi utaona kuwa uamuzi wowote ambao utawaacha kina Chenge na EL katika nafasi zao au ndani ya chama - hata ukitolewa kwa maneno yoyote yale - utakuwa ni ushindi mkubwa sana kwa kina Lowassa. Na utafanya iwe vigumu sana kwa CCM mbeleni kushughulikia nidhamu na maadili kwani kiwango cha kuweza kukosea kitakuwa kimeinuliwa juu sana. Hili litakuwa kweli hata siku Lowassa itokee aje ashike madaraka kwani kipimo ambacho kitatumika kumuokoa yeye anaweza kujikuta anatakiwa kukitumiwa kwa wengine.

  CCM wamebembelezana sana kwenye hili ndio maana mwisho imekuwa ni kama mtu anayejaribu kumuua nyani huku anatazamana naye usoni.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Behold your President 2015: PICHA !
   
 6. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ..........penye blue
   
 7. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nionavyo mimi tatizo la migogoro ndani ya ccm ni uwepo wa old fashioned people na new era, kuna watu wengi sana ndani ya ccm ambao hawataki kubadilika na kwenda na wakati kwa maana kwamba mzee ambae hakuwahi kujifunza computer anataka aende sawa na aliyezaliwa na kukua nayo,kisiasa namaanisha kuwa mfumo wa enzi za mwalimu hauwezi kutumika tena sasa hivyo wazee wengi ndani ya ccm wanatakiwa kuchagua kati ya kwenda na wakati au kuachia ngazi lakini tumeona kwamba wengi wao wameamua kubaki na kulazimisha misimamo yao kwa watu ambao hawazungumzi lugha moja. jambo lingine la kuonyesha old fashion ni kuwa they take challenges or opposition to their views as an insult or an offense since they consider themselves old enough, rich enough and know it all, this is bad. ccm need change but there are few people who recognize the need for change and some not.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kujua matatizo ya CCM ni makubwa kiasi gani basi anzisha biashara ya sumu ya panya karibu na mahali wanapofanyia mkutano NEC. Utapata super profits beyond your imaginations.

  Tatizo la ccm ni lack of courage & visionary leadership.

  Watu, mitazamo tofauti, nafasi na matamanio ya nafasi n.k hivi vyote vimekuwepo CCM (hata ndani ya vyama vingine), lakini lazima kuwepo na mechanism & tools za kuongoza kama si kudhibiti mambo yote haya bila ya kuathiri chama na malengo ya pamoja. Na pale inapotokea mmoja au wawili wanakuwa na mawazo ya pembeni basi ni vema watu hao wakaongozwa kwa taratibu sahihi na zilizokuwabliwa na wengi ili mambo yaendane na kile kilochokusudiwa. Mwl Nyerere aliweza kutengeneza na kusimamia (kwa uthubutu) mfumo wa kiuongozi ili kudhibiti watu, nafasi na matamanio etc lakini baada ya kufa wazee waliobaki na waliokuwa na nafasi ya kusimamia chama walitizama pembeni. Hili ni kosa la kihistoria!

  Nina hakika ukiwauliza wajumbe wa NEC leo hii nini malengo ya CCM kila mmoja atakupa jibu tofauti. Haijulikani chama kinasimamia nini, na kina malengo gani (ukiondoa jambo moja tu kushika madaraka). Sasa, kama chama hakina vision unategemea watu wafanye nini zaidi ya kuota? Na kila mmoja anaamini ndoto yake ndiyo sahihi na lazima wengine waifuate? La kusikitisha zaidi wameweka watoto wadogo kabisa wasio na experience yoyote ya maisha kwenye nafasi za maauzi ya juu. Hawa wana vision gani? NEC is full of day-dreamer political rookies.

  Sasa hivi CCM is beyond reppairs, opportunity ya kufanya ukarabati ilizama baharini siku nyingi. Huwezi kupatanisha wanafamilia walio chini ya paa moja lakini kila mtu anatembea na glass ya maji na sahani ya chakula kwa kuhofia kuwekewa DDT huku wengine wakitembea na funguo za vyumbani kiunoni wakiogopa wizi na uharibufu mwingine!

  Mapatano ya aina yoyote katika hali ya namna hii kwa mtazamo wangu ni cosmetic.
   
 9. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Mgogoro ndani ya ccm ni ubinafsi uchoyo uongo,ulimbukeni na usiri baina yao. Kila mmoja anaogopa kunyosha kidole kwa mwenzake kwani wote ni wachafu kwa hivi wataendelea kugombana mpaka siku nchi itakapoongozwa na chama kingine ndipo bomu litapasuka na ataonekana mbaya na mzuri. Wadanganyika tuendelee kuangalia comedy za ccm mpaka tutakaposema enough is enough lakini when will that happen? You and I don't know!! Wacha waendelee kukwaruzana kupandishana pressure mwisho wa yote ni mapumziko ya milele.
   
 10. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  how do the following laws apply in CCM Mzee Mwanakijiji?

  Never put too much trust in friends learn how to use your enemies

  Plan all the way to the end

  Never outshine your Master

  Conceal your Intentions

  Crush your enemy totally

  Pose as a friend work as a spy

  if you look into this few laws there a some members applying them and some who are not at all aware f this laws and thus they are caught in between not knowing what to do, anybody getting into a game needs to know the reason why that game?how to play it? the rules of the game? the challenges of the game? the solution to the challenges? and such things now who are the young politicians in ccm?i believe many of them its because they simply had a connection such as my daddy was a president or wherever and this kind of people are extremely hopeless.
   
 11. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,354
  Trophy Points: 280
  Swali kuu la kujiuliza wanachama wa CCM wanaunganishwa na nini at this moment in time. Maana chanzo cha CCM ilikuwa ni TANU na hawa wazalendo walikuwa wanapigania uhuru kutoka kwa mkoloni. Je leo hii wanchama wa CCM wanaunganishwa na nini maana sera za chama kimaendeleo azieleweki in my humble opinion naamini kikubwa kwa wengi ni life chances.

  Kwa hivyo inavyotekea migogoro yeyote ndani ya chama anaechukua kundi fulani ujue ni unafiki unaombatana na maslahi yake for the large part. Kwa sababu ki ukweli amna chama duniani kisicho na migogoro lakini vyama vya wenzetu kikubwa ni what direction needs to be taken politically na jinsi ya kuboresha maisha ya watu. Mfano the 'Milliband' brothers wa UK Labour party wamefikia hatua ya kutotembeleana kwa ajili ya kutofautiana jinsi ya kukisogeza chama mbele lakini the main theme ni kwamba maskini ndio priority. Hila wote wana different philosophy of achieving that goal.

  Sasa jiulize CCM wanagombania nini zaidi ya madaraka ya kuweza ku-control dola na kuweza kutuibia lakini amna party philosophical lines. Ndio maana wenzetu wakichukiana wanakubali kwamba matatizo yao yapo based on ideas (therefore public haihitaji kujua migogoro ya ndani, kwakua through democracy wanachama wanchagua kiongozi wanaemtaka na ndio wa kukipeleka chama mbele), where by kwetu tofauti ya wanasiasa ujue ni uchu wa madaraka, ulaji na uwezo wa kuwamaliza wenzako. Hapo ujue tamaa inatawala au tuseme ndio democracy iliyoegemea tamaa, duuh! kaazi kweli kweli.
   
 12. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji

  siasa ni nini?je Tanzania tuna wanasiasa? sifa za mwanasiasa ni zipi? siasa safi ni nini? kuna uhusiano gani kati ya siasa na uzalendo? je CCM kuna wanasiasa? CHADEMA je? naombeni na wengine mnieleweshe pia!
   
 13. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Popote pale binadamu zaidi ya mmoja wakikusanyika wanahitaji kuwa na sheria (rules) za kuwaongoza. sheria hizi lili watu wasizivunje kunakuwa na taratibu (procedures) zinawekwa pia. mwanadamu anayefuata procedures huwa anakuwa na uwezekano mdogo wa kuvunja sheria.

  ili sheria na taratibu zitumike kuleta maendeleo ( yaani kusonga mbele na si kusimama au kurudi nyuma) ni lazima kuwe na wasimamizi thabiti. msimamizi mkuu wa sheria na taratibu ndiyo chanzo kikubwa cha u thabiti wa wasimamizi wadogo. wasimamizi kazi yao inakwenda mbali zaidi na hata kuweza kutambua nini kinahitajika kwa ajili ya mustakabali wa jamii. hivyo wanakazi hata ya kuanzisha na kusimamia mchakato wa kubadili au kuondoa sheria na taratibu ambazo ni butu kwa jamii

  tatizo la ccm kiini chake ni "mmomonyoko wa maadili".
  kutokana na umri wa ccm na sera zake sitarajii ccm kuwa na wafuasi wenye kutii maadili ya chama chao, hii ni kwa sababu sheria zao hazina uhalisia kwa tanzania ya leo.sheria ya nidhamu ya chama, ya kumtetea muovu kwakuwa tu tunamtetea dhidi ya wasio ccm, imepitwa na wakati kwani waovu wanatumia fursa ya kutetewa ndani ya chama na "kupeta na ufisadi". sasa kimsingi hapa pamekosa wasimamizi wazuri, kwamaana kama ccm itakuwa na viongozi makini, wangelikwisha ona na kutabiri madhara ya zile aya za katiba ya chama na utamaduni wa kutetea mtu kwa maslahi ya chama.
  kwa maelezo hapo juu, mgogoro ccm utaisha iwapo;
  1. ccm itapata kiongozi mpya aliye makini atakayeweza kupitia sheria na taratibu za chama na hatimaye kuhakikisha zinafuatwa na kila mwana ccm.
  2.kwa kupatikana kiongozi makini makundi yatakufa, na ccm itabaki moja
  zaidi ni kuwa nchi yetu ni nchi inayotawaliwa na chama kinachoshinda uchaguzi wa raisi kwa kura nyingi. udhaifu wa kiongozi wa chama manake ni udhaifu wa chama, na hatimaye ni udhaifu wa taifa ikiwa chama dhaifu ndiyo kimeshika dola.
  Nakushauri Kaka Mwanakijiji, tuisaidie ccm tulisaidie taifa letu kwa muda huu ( 2010-2015).
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,584
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  Mgogoro huu unatokana na the fact kwamba JK hayuko na msimamo waliokubaliana hapo awali na EL kuwa EL is next on line...JK ni wazi tayari ana chaguojingine kwasababu EL alishasusa na kama ni joto ya jiwe JK keshaionja kwasababu hiyo.

  So sidhani kama atarudi nyuma,ni wazi maybe he is for Membe.

  BTW mbuzi hata kama akitaka kumla chui ataweza?
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kiini hasa cha mgogoro ndani ya CCM kwa mtazamo wangu kimetokana na kushushwa kwa leadership bar, it's so low kiasi kwamba kila kiongozi wa CCM regardless of the baggage they have anafikiri anaweza kuwa mbunge,mwenyekiti, raisi, na ikisndikana sana basi awe waziri. It's too a low level such that unasikia eti watu kama Nchimbi, Mkulo na usikute hata Januari nao wanawania uraisi. Mbaya zaidi ni kwamba nilichokielezea ukichanganya na kutanguliza maslahi binafsi basi matokeo yake ndiyo kama tunayoyaona.
   
 16. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zanguni,hayo ndio matokeoo ya rushwa,Taifa limewekwa rehani na kundi la wezi,kuna wanaotamani sana kuachana na wenzao kwa vile,aidha wametimiza malengo yao ama dhamiri zao zinawasuta kwa wema wa wale wanaowaongoza(watu masikini,waogo na waungwana wa dhamiri zao).wengine ni miongoni mwa kundi Hilo hilo ambao wao nao sasa wanaona imefika zamu yao ya kutawala ili kufikia malengo yao kisiasa na kiuchumi,wanajuana sana hawa wawili,hakuna msafi hata mmoja.kwamantiki hiyo,ili amani iwepo ndani ya chama,lazima huyu nae atimize na kufikia malengo yake.Hapa minyukano inaendelea...Hiyo ndio CCM-Hutaki ondoka....

  Kundi la wapambanaji,Kama ni la kweli,lazima liondoke,na kwakweli ndio wenye nafasi kubwaya kuiongoza nchi hii baada ya 2015.
   
 17. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  MMM. Matatizo ya CCM ni watu,maslahi yanayogongana na matamanio ya nafasi. CCM imebadilika kuwa chama cha siasa na kuwa kampuni ambayo waliomo wanajihakikishia ulinzi/usalama,utajiri na madaraka! Ugomvi baina yao hauwezi kuisha maana wanagombania madaraka,mali na fedha.
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Huo mgogoro uliopo CCM unaujuwa wewe tu?

  Huo mgogoro umetoka wapi? na umeanza lini? kati ya nani na nani? au ndio unataka kuuanzisha wewe?

  Khaa! yatakushinda, usiuseme mgogoro uliotangazwa JF kati ya Mbowe na Zitto ukayatangaze yasiyo kuwepo wala yasiyo kuhusu ndee wala sikio? unanini? huo ndio ukisikia uzabizabina.

  "nyani hatazami kundule..."
   
 19. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hii ndiyo shida chama kujaa watu wa majungu na wanafiki.
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,813
  Likes Received: 36,864
  Trophy Points: 280
  avoid the ignorant." (Qur'an 7:199)
   
Loading...