Kiini cha machafuko Songea hadhara - Polisi yawakuta watuhumiwa hirizi na barua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiini cha machafuko Songea hadhara - Polisi yawakuta watuhumiwa hirizi na barua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 24, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Habari tulizozipata wakati tukienda mitamboni zinasema, kwa mara nyingine, jana saa 12 jioni, polisi mjini Songea walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwaokoa watu wawili waliokuwa wakipigwa na wananchi wakiwatuhumu kwamba ni majambazi wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya wananchi.

  Watu hao ambao walijeruhiwa vibaya walikamatwa na wananchi katika eneo la Mkuzo nje kidogo ya Manispaa ya Songea baada ya kujitambulisha kwa wenyeji kwamba wao walikuwa wakitatafuta shamba la kununua, huku mmoja wao ambaye ni mwanamke akitoroka na kukimbilia kusikojulikana.

  Kutokana na kuwatilia mashaka, wananchi hao waliwazingira na kuwaweka chini ya ulinzi kisha kuwafikisha nyumbani kwa kiongozi wa Serikali ya mtaa wa Mkuzo, John Moyo na baadaye walianza kuwapiga baada ya kutokea utata katika maelezo yao.

  Kuona hivyo moyo alipiga simu polisi ambao walifika na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi, hivyo kuwaokoa watuhumiwa hao kisha kuwakimbiza katika hosipitali ya mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya matibabu.

  Watuhumiwa hao ambao wametambuliwa kwa majina ya Gervase na Juma, walikuwa wakivuja damu katika sehemu kadhaa za miili yao na polisi walipowafanyia upekuzi waliwakuta wakiwa na hirizi na nyaraka zilizoandikwa kwa lugha ambayo haikuwa rahisi kusomeka.
   
 2. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  suspicion...thats what kills this great nation
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  upo mama!?!! long time no see.....

  :focus:
   
 4. S

  Steve1 Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Iv dunia ya leo bado wa2 wanasujudu ndumba?
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Imani za kishirikina zikiendelezwa ipo kazi kusonga mbele, na tutaelndelea kuuana bila huruma.
   
Loading...