Kiingereza kinampa shida mkuu wa mkoa Arusha, aogopa mikutano ya kimataifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiingereza kinampa shida mkuu wa mkoa Arusha, aogopa mikutano ya kimataifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpinga shetani, Feb 7, 2012.

 1. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Imebainika kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, anakiogopa sana kiingereza kiasi cha kujitahidi kuiepuka mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika mjini Arusha.

  Mkuu huyo amekuwa akipata shida sana kusoma speech alizoandikiwa kwa lugha hiyo ngeni katika baadhi ya mikutano aliyoalikwa kuifungua na hivi sasa ameamua kuikacha jumla.

  Hakuna dhambi kwa kiongozi kutojua lugha ya malkia lakini mtu akipewa eneo la kimataifa kama Arusha kigezo hicho kwa kweli ni muhimu maana kuna taasisi nyingi za kigeni hapa hii ikiwa ni pamoja na jiji kuwa mwenyeji wa mikutano mingi ya kimataifa.

  Lakini watu wake wa karibu wanasema suala si kiingereza tu. Hata kusoma speech ya kiswahili kwa mtiririko ulio tulia huwa ni taabu kwake.

  Hata hivyo Mulongo ambaye inadaiwa aliletwa mkoani hapa maalum kuja kumdhibiti mbunge wa Monduli anatekeleza jukumu hili kwa ufasaha ila kama atashinda ndicho hakijulikani.

  Ki utendaji pia Mulongo ni mzuri kwani amefanikiwa kuwatimua maofisa wala rushwa na watendaji hovyo katika taasisi na ofisi za umma mkoani hapa. Hii ni pamoja na madai kuwa amekuwa akifanya hivyo kisiasa zaidi.
   
 2. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  duh!? Sasa ameletwa na nani kuja kumdhibit EDWARD
   
 3. King2

  King2 JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Apige kiswahili tu.
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  kikazi nimemkubali,juzi kati alileta jamba jamba pale mt.meru hospital pakabadilika.hilo la lugha ngoja tusubiri wanaomjua wa comment
   
 5. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Inadaiwa hata Kiswahili taabu!
   
 6. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ​aliyemteua naye ni kilaza
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  arusha kuna sehemu nyingi sana za english course!
   
 8. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sasa kazi ipo..mkuu wa mkoa ni Yes Sir, No Sir......
   
 9. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Kwani majukumu ya mkuu wa mkoa nini!
   
 10. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Haiwezekani mkuu wa mkoa akawa zekuku endi zebata.
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Haaaa can somebody guess,eh which which eh,what globale womingi was? Ok ubah eh it it it iz it iz,ok kwa kiswahili!
   
 12. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  punguza majungu mkuu,kusoma mkuu wa mkoa aingie chaka,je kuongea si ndo itakuwa balaa
   
 13. senior citizen

  senior citizen Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aende pale kimahama jengo la mollel... Atapata tiba ya tatizo lake...
   
 14. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Kama aliyemteua ni walewale wa to manufacture teachers what can u expect from him??soon worms will feast in their hollows!
   
 15. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Dah!! Mkuu wa mkoa unalo ndugu yangu,
  anyway endelea kupiga kazi kwani wengi wanaojua hivi viingereza ndio wameendelea kutuletea mabalaa na matatizo mengi, ona migomo ya madaktar sasa wasio hatia wanakufa,
  we inshu ya kizungu isikupe taabu sana hata kiswahili piga mbele zao ,watataka tu,
   
 16. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Aende English course kama kuna ugumu aajiri mkalimani.
   
 17. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hata lugha mama (kijita) taabu!
   
 18. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 736
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 60
  Kisheria Tanzania inatambua Kiswhahili na Kiingereza kuwa lugha rasmi.Kwa Mkuu wa Mkoa anatakiwa awe na mkalimani ,by the way pale Arusha International Conference Center si pana vifaa ambavyo vinatafisiri lugha nyingine?
   
 19. N

  Ndole JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hana haja ya kujisumbua na kingereza bwana piga kiswahili au kijita tu watatafsiri wenyewe huko.
   
 20. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Simtetei lakini siamini, labda mtoa mada atusaidie kwa kutuambia kwamba ni mkutano gani, ulifanyika lini na ulihusu nini ili tufuatilie video pale IACC ili tuzione na tuthibitishe hilo.
  Kwa kuwa bongo siasa kila sehemu tunaweza tukajikuta kwenye mtege wa maadui zake ikumbukwe kwamba kuwa mkuu wa mkoa sio single nyepesi hivyo majungu yanaweza kuwa ni mtaji rasmi.
   
Loading...