Kiingereza cha Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako akiwa MUHAS. Inasikitisha

Kuna siku nilikua naangalia channel ya uganda, nikaona chokaraa wakihojiwa kwa kiingereza, na walikua wakiongea kiingereza fasaha kabisa.
 
Kabobea kwenye masomo ambayo lugha sio msingi mkubwa sana na vilevile lafudhi ya kilugha imemkaa sana na inaadhiri matamshi ya kiingereza lakini amebobea kwa alichokisomea
 
Haina shida kwani kasomea kiingereza??Huyo ni Prof. wa HESABU sio kiingereza. Hivyo mimi sioni shida.

Huyo siyo Prof wa Hesabu. Angekuwa wa Hesabu, udsm angekuwa department of mathematics.

Alikuwa anga za Education. Inaweza kuwa maeneo yake ni kwenye ualimu. Yaani ualimu wa walimu.
 
Ng’ere ya mother Ndalichako sio ya Nchi hii aisee. Sijui aliwezaje kuwa lecturer ambapo vipindi vyote lecturer unatakiwa kutema ung’eng’e non-stop
 
Kama ni kweli basi uchawi upo asee. Haiwezekani kabisa huyu akawa exceptional. Ni moja ya mawaziri wa hovyo kuwahi kutokea duniani.
Mwanafunzi akiwa exceptional darasani haimaanishi atakuwa vizuri kila mahali...alitakiwa abaki chuoni afanye research lakini ndio siasa zetu zinavyoenda, ukishakuwa na PhD basi unakuwa kiongozi automatically
 
Kiingereza cha huyo mama kinawakilisha Watanzania wengi sana!

Naamini hata wanaomsema humu kwamba hajui Kiingereza, ukivisikia Viingereza vyao, si ajabu havina tofauti na cha kwake.

Natamani sana siku nivisikie Viingereza vya wana JF….hahahahaa.

I can guarantee you havina tofauti kubwa na cha huyo mama.
...na vinaweza pia chini zaidi kuliko cha Mamaa!
Ogopa WaTz kwa kuona Kibanzi kwenye jicho la mwenzao wakati wana Li Boriti kwenye jicho lao...!!
 
Dah! Najua wapo watakaosema "Kiingereza ni lugha tu, kama lugha nyingine"!

Sawa, ni lugha tu, wala sibishi, sema dah!!! Lakini huku kwenye lugha tayari hakuna ubishi wowote kwamba Da' Joi ni mweupe kweli kweli, na kama isingekuwa anapata hizi nafasi za kuongea, wala tusingejua!!

Je, huo utaalamu wake mwingine ambao hauwezi kuthibitishika kirahisi in public namna hii, na kwenyewe yaliyomo yamo au ndo ule utaalaamu wa kwenye makaratasi?!

Anyway, sie ambao tulisoma soma sayansi kidogo huwa tunasema "language competency isn't our thing"!
 
Huyu mama alianza na ualimu wa primary school
Hapana alitoka form six moja kwa moja. Kuna kaka yake alikuwa anaandika Daily News alikuwa ni columnist wakati akichukua FTC Dar tech wakati huo anaitwa Laurent Ndalichako. Prof ni mkali sana wa hesabu usisikie
 
Alipata PhD in Educational psychology (Major in educational statistics & measurement and evaluation.) Kutoka University of Alberta, m Edmonton, Alberta, Canada ni chuo ambacho ni very prestigious kwa Canada na duniani kiujumla ! Kwa habari za chini chini hakusoma alirushwa kutoka Masters kwenda PhD kwa sababu alikuwa an exceptional scholar
Mfumo wa elimu wa Canada unaruhusu kuruka steps, ni juhudi yako tu
 
Hivi kwanini hawali tizi kwanza hata kwa kujirekodi wakajisikiliza wakarekebisha MAKOSA ndo waje kwenye kadamnasi??????
 
Aibu sana karne ya 21 bado jitu linaangalia kingereza kama sehemu ya mtu kuwa intelligent...
Mleta uzi wee ni wa hovyo sana
Mkuu watu Wana feli interview kwa matamshi ya hovyo ya kizungu Sasa iweje hata wa maPDH nao I we Yale yale
 
Back
Top Bottom