MANYORI Jr
JF-Expert Member
- Mar 25, 2012
- 462
- 343
Ikiwa imepita siku moja tangu kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2019, moja ya masomo yaliyopelekea matokeo mabovu ni English Language.
Somo la lugha ya Kiingereza linalea takribani masomo 7 na lenyewe likijilea katika yale masomo 9 ya msingi kwa shule za sekondari.
Hii inadhihirika pale "you no, this were, ok or yes" zinapowapelekea wadogo zetu kushindwa kueleza mawazo yao katika maswali kutoka kwenye masomo yale 7 na Kiingereza kama somo la 8.
Serikali, kwa nafasi yake, inaweza kukabiliana na changamoto ya ufaulu sekondari kwa kuajiri rasimali watu (walimu) wa somo la lugha ya Kiingereza kwa kuwa hata uhalisia watu hawa ni adimu na hawatoshelezi mahitaji.
Zaidi ya hili somo la lugha ya Kiingereza ndilo changamoto mama katika changamoto zinazoukabili mfumo wetu wa elimu hasa sekondari na hata ngazi za juu.
Ni dhahiri kuwa panahitajika hatua madhubuti ili kuinusuru elimu ya taifa letu.
Kama watoto watakaa 'kambi' bila lugha ya Kiingereza, hii ni sawa na mganga bila tunguli.