Kiherehere cha Mtangazaji na Mchekeshaji huyu ndiyo chanzo cha Mama Mndeme kuhamishwa Mkoa


GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,941
Likes
37,239
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,941 37,239 280
Ni kweli hakuna ambaye alikuwa hajui kwamba huyu Mama Mndeme alikuwa na bonge la ' Bifu ' na aliyekuwa ' Bosi ' wake na ambaye ni Mkuu wa Mkoa aliyeondolewa Bwana Jordan Rugimbana hali ambayo kiukweli kwa 95% ndiyo imepelekea Yeye kuondoshwa hapo hasa baada ya kuonekana kusingekuwa na ' tija ' katika huo Mkoa ambao pia ndiyo Mji Mkuu wa Tanzania wa Dodoma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa kuna ' Mtangazaji ' mmoja wa tv moja ' pendwa ' hapa Tanzania leo siku nzima alipofungua tu Kipindi alianza kuonyesha dhahiri kwamba anafufahia huku akiwa anamcheka Kinafiki na Kidharau Bwana Rugimbana kwamba kaondolewa Ukuu wa Mkoa halafu hapo hapo akawa anatumia muda mwingi ' Kumpamba ' Mama Mndeme ambaye jana alipandishwa kutoka Ukuu wa Wilaya na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ' cheo ' ambacho alikuwa nacho ' Bosi ' wake ambaye walikuwa na ' Bifu ' kali sana.

Cha kusikitisha zaidi nadhani huyu Mtangazaji alikuwa ama hajui au amesahau kwamba hata Watazamaji wao wengi pia ni Watendaji wa karibu na Mheshimiwa Rais lakini na hata Rais mwenyewe huwa anawatizama kila asubuhi hivyo ' ubwabwaji ' wake wa leo huku kila mara akijigamba kwamba huyo Mama ni Mtu wake wa Karibu sana na kwamba hata Yeye amefurahi kusikia kwamba amepandishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa.

Wakati huyu Mtangazaji akiendelea ' Kubwabwaja ' zake kama ilivyo kawaida yake mara akatokea tena ' Mchekeshaji ' mmoja maarufu mno kwa sasa hapa nchini ambaye siku chache tu zilizopita ' Israeli Mtoa Roho ' alimkosakosa kumpeleka Mbinguni ambaye na yeye pia akaanza kumwagia ' misifa ' kibao huyo Mama hadi kuongea mambo mengine ya ' Kibinafsi ' nae hali ambayo kwa Watendaji wa ' System ' wanaoijua vyema Kazi yao walianza kushtuka kisha wakatathmini upya ' uteuzi ' wa huyo Mama Mndeme na kugundua ya kwamba kwa hali iliyokuwepo si vyema akawa Mkuu wa Mkoa huo wa Dodoma japo ni Mtendaji mzuri ila ahamishwe Mkoa mwingine na ndipo wakaenda kwa Bwana Mkubwa / Taita wa Magogoni Feri na kumshauri amuhamishe Mkoa na kweli akapelekwa Ruvuma na yule wa Ruvuma Mzee Mahenge akaletwa Dodoma.

Kilichotokea leo nadhani kinapashwa kuwa ni Funzo kwa Watu wote kwamba hata kama Wewe unajuana au una ukaribu na ' Mkubwa ' fulani Serikalini ila si vyema sana ukaja kutuonyesha Sisi Watu wengine huo ukaribu wenu kwani kuna uwezekano huku kuonyesha Kwenu ukaribu ndiyo ukawa chanzo cha hata Wao kuanza kufuatiliwa ' nyendo ' zao na hatimaye mkajikuta mnawaharibia ' Vibarua ' vyao na wanarudi zao ' Uraiani ' kusota tena.

Na pia nitoe ' Wito ' hasa kwa Wanawake wa Kitanzania kwamba jifunzeni kuwa na Kifua, staha pamoja na uvumilivu pindi jambo fulani jema linapokutokea. Inasemekana mara baada tu ya kutangazwa jana kuwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa huo Mkoa wa Dodoma huyu Mama muda mwingi aliutumia kufurahi huku akishirikiana na ' Mashosti ' zake kupiga ' Vijembe ' vya mbaya wake / adui yake Mkuu wa Mkoa aliyeondolewa Bwana Rugimbana bila kusahau na kutuma meseji kadhaaa za Kimafumbo na Kimajungu huku akisahau kwamba tokea jana alikuwa akifuatiliwa na wenye ' Kazi ' yao.

Haya Mama kila la kheri sasa huko Ruvuma ambako umepangiwa na Wewe Mtangazaji jaribu sana kupunguza ' Kiherehere ' chako cha kujifanya unajuana na ' Wakubwa ' wote wa nchi hii japo najua na hili nalisema waziwazi kwamba kuwa kuna Mwana Mama mmoja ambaye amekuteua kuwa ' Balozi ' wake katika Taasisi yake huko Mkoani Mbeya umemtumia aweze kukufanyia ' upatu ' kwa ' Bwana Mkubwa ' ili uteuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya na niseme tu rasmi usiku huu kwamba huko ' Kujipendekeza ' Kwako kwa huyo Mama ambaye pia ni Naibu wa ' Mhimili ' mmoja wenye nguvu hapa nchini umezaa ' matunda ' kwani muda wowote kuanzia sasa pakitangazwa Wakuu wapya wa Wilaya basi na Wewe pia utakuwepo na hatimaye kuweza kuwaacha hapo katika hiyo tv huyo ' Emolo ' wenu na huyo Mwanadada wa Kikenya asiyeweza kutamka vizuri neno ' Kutengeneza ' na husema ' Kutengeza '.

Nawasilisha.
 
Joselela

Joselela

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
2,744
Likes
2,564
Points
280
Joselela

Joselela

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
2,744 2,564 280
Sio vizuri kuweka siri za taifa, inavoonekana na wewe ni mtu wa system lakini haunaga siri humu JF na wengine wanakufahamu nyuma ya ID fake. NOW YOU ARE FIRED!!

Undugu na urafiki hadi vyeo vya juu ndio maana viwanda kila siku vinateuliwa!!!
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,941
Likes
37,239
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,941 37,239 280
Sio vizuri kuweka siri za taifa, inavoonekana na wewe ni mtu wa system lakini haunaga siri humu JF na wengine wanakufahamu nyuma ya ID fake. NOW YOU ARE FIRED!!

Undugu na urafiki hadi vyeo vya juu ndio maana viwanda kila siku vinateuliwa!!!
Umemaliza au bado kuna mengine umeyabakiza?
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,941
Likes
37,239
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,941 37,239 280
Tena Ruvuma ni Mkoa Mgumu sana
Apeleke huko sasa hayo ' majungu ' yake. Kama alivyoteuliwa ile jana angetulia zake kimya tu na kutoonyesha kumcheka ' Bosi ' wake Rugimbana na kumpiga majungu na mafumbo mafumbo kwa kushirikiana na ' mashosti ' zake nadhani kama sijakosea na kumbukumbu zangu hazijakosea huyu Mama Mndeme leo angeweka ' rekodi ' ya kuwa mwana Mama wa Kwanza nchini kuwa Mkuu wa Mkoa tena wa Mji Mkuu wa Tanzania Dodoma ( Idodomya )
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,941
Likes
37,239
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,941 37,239 280
Kama akipita humu au wadau wake, nadhani atapata somo.
Huyo Mama Mndeme amejiharibia mno ' Ulaji ' wa hapo Dodoma na sasa kapelekwa kwa ' Wagumu ' asilia huko kwa ' Watani ' zangu wakubwa upande wa pili ' Wangoni ' na huko kwa ninavyowajua ' Wangoni ' mziki atauona. Ataogelea sana katika Mto Ruvuma hadi atie ' akili '. Haya Watani zangu upande wa pili Wangoni Mama huyo amekuja huko Kazi kwenu sasa!
 
Chris14

Chris14

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2017
Messages
3,139
Likes
2,125
Points
280
Chris14

Chris14

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2017
3,139 2,125 280
Huyo Mama Mndeme amejiharibia mno ' Ulaji ' wa hapo Dodoma na sasa kapelekwa kwa ' Wagumu ' asilia huko kwa ' Watani ' zangu wakubwa upande wa pili ' Wangoni ' na huko kwa ninavyowajua ' Wangoni ' mziki atauona. Ataogelea sana katika Mto Ruvuma hadi atie ' akili '. Haya Watani zangu upande wa pili Wangoni Mama huyo amekuja huko Kazi kwenu sasa!
Nadhani yuko katika probation period. Time will tell.
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,941
Likes
37,239
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,941 37,239 280
Mkuu ungekuwa lecture ningekutafuta unifundishe jinsi ya kujengana kupangilia hoja. Ni moja ya watu nawaheshimu sana nikiona thread zako huwa siachi kuzisoma.
Akhsante na Shukran sana Mkuu. Maneno yako yamenijenga na kunitia mno moyo. Leo naweza kusema Wewe sasa umekuwa ni Member wa Nne ( 4 ) kuniambia Mimi maneno haya kwani kuna Wenzako wengine Watatu ( 3 ) katika threads kadhaa ambazo nilichangia nao waliweza kuniambia maneno haya kama yako.

Sifa zote na Kuu zimwendee sana Mwenyezi Mungu kwani naamini huu uwezo, haya maarifa na hiki Kipawa alikusudia kabisa ' Kunizawadia ' na pengine alijua ni wapi nitatumia ili nami mawazo yangu yaweze kuwa ' chachu ' ya Kifikra na ya Kimaendeleo hasa katika Jamii ambayo Mimi GENTAMYCINE naishi 24/7.

Nashukuru sana Mkuu na nitajitahidi nizidi kuwa ' maradufu ' ya hivi nilivyo sasa.
 
LOTH HEMA

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Messages
4,389
Likes
1,587
Points
280
Age
34
LOTH HEMA

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2015
4,389 1,587 280
Sio vizuri kuweka siri za taifa, inavoonekana na wewe ni mtu wa system lakini haunaga siri humu JF na wengine wanakufahamu nyuma ya ID fake. NOW YOU ARE FIRED!!

Undugu na urafiki hadi vyeo vya juu ndio maana viwanda kila siku vinateuliwa!!!
Hilo jitu linajua kudadavua siri za watu sana.Sijui ni linani kwa ID yake!
 
Chris14

Chris14

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2017
Messages
3,139
Likes
2,125
Points
280
Chris14

Chris14

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2017
3,139 2,125 280
Apunguze tu uswahili, ushosti na majungu yake na pia atambue ya kwamba Dodoma siyo Ruvuma alikopelekwa sasa hivyo ' agangamale ' hasa.
Kweli kwa hii iliyomtokea mi naichukulia kama mkuu amem-demote. Kama anajitambua aache huo uswahili, ushosti na majungu otherwise hali itakuwa ngumu kwake.
 

Forum statistics

Threads 1,236,093
Members 474,988
Posts 29,246,339