Elections 2010 kihaha mjin ilichakachuliwa kulinda ajira za wakubwa...hali bado tete kwa wananchi.

komagi

Member
Nov 1, 2010
62
2
tetesi nilizozipata kwa siku nzima ya jana kufuatia matokeo ya utata yaliyotangazwa kwa mizengwe ubunge kwa jimbo la kibaha mjini ni kama ifuatavyo:
kasheshe ilianzia kwenye kura za maoni za ccm...ambapo alipita mh. s.koka na ikidaiwa alihonga sana. lakin kamati kuu ya ccm makao makuu ilikuwa inampigia chepuo proffesor. wangwe ili agombee jimbo hili la kibaha mjini. lakini waliopiga kura ya maoni wakakomalia kuwa hawataki mtu mwingine zaidi ya mh. koka. kwa kile kilichoonekana kama nguvu ya wanachama waliopiga kura za maoni ni kubwa, ikaamriwa kuwa agombee mh. koka huku kukitotewa angalizo kali kabisa kuwa kama mh. koka hatashinda basi ajira za watendaji wakuu wa wilaya kwa chama na hata serikali zitakuwa mmashakani. hii ikimaanisha mkuu wa wilaya, mkurugenzi na wengineo. hali ilipogeuka baada ya kupigwa kwa kura 31 october ikagundulika mh. koka ameshindwa na kijana machachari wa chadema Mh.Habib Mchange ndipo kasheshe ilipoanzia hapo. ikumbukwe kuwa hili jimbo lipo nyumban kwa mwenyekiti wa chama taifa wa ccm wangefanyaje likiondoka? kilichofuata ilikuwa kwa watendaji husika kuamua kusuka ama kunyoa,kuchakachua matokeo ama kutoa matokeo halisi ili ajira zao zipotee? wakati wakiwa hawajui cha kufanya mnamo saa nne usiku kabla ya kutangazwa matokeo hayo akafika mh. makamba na kushurutisha matokeo yaliyochakachuliwa kutangazwa. mnamo saa tano matokeo yalitangazwa kwa staili ya aina yake, police walikuwa tayari kwa mabomu kibao ya machozi na wakati inatangazwa kuwa mh.koka ameshinda papo hapo kulipigwa mabom zaid ya kumi kusambaza umma waliokuwa wanasubiri matokeo hayo.

my take. hii haivumiliki kama ccm wenyewe wanatangaza demokrasia ili hali wao hawaiwezi demokrasia.
 
Alishinda kwa kura ngapi mgombea wa chadema? je anaushahidi? ataendelea kudai haki yake?
 
1. Rekebisha heading isomeke Kibaha, na si Kihaha!
2.Kilichofanyika Kibaha ni Umafia na udikteta...ndio maana wanapotakiwa kueleza wanatokwa jasho la pua kama mbwa -mwizi!
 
ushahidi anao tena uko wazi kutoka vituo vyote vya jimbo la kibaha mjini na kuna kuna habari za kuaminika ameshaenda mahakaman. nilikuwa najaribu kumpigia simu anipe ufafanuzi kamili lakini simu yake inaonekana iko busy sana.
 
Hii nchi mimi naona inaninyima raha kila siku. Bora nikae kimyaaa wiki nzima kwanza, nitarudi jumatatu.
 
Back
Top Bottom