Kigwangalla: Serikali kupiga Marufuku Matumizi ya Pombe za VIROBA Kufikia Mwezi wa Sita mwaka 2017

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Serikali kuzuia viroba kutengenezwa nchini na kufuta kabisa matumizi ya pombe za aina ya viroba ndani ya nchi yetu. Haya yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu hoja za wabunge kufuatia michango mbalimbali ya wabunge juu ya hoja za Kamati za UKIMWI na Madawa ya Kulevya na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya jamii.

Dk. Kigwangalla alisema, 'haitopita mwezi wa sita Serikali itakuwa imepiga total ban (marufuku) matumizi ya madawa ya kulevya nchini....'

Miezi kadhaa iliyopita Dk. Kigwangalla aliongoza kikosi kazi cha Serikali kilichokuwa kinashughulikia suala la viroba ili kutathmini ukubwa wa tatizo na kupendekeza hatua za kuchukua.

Kikosi kazi kilibaini changamoto nyingi ikiwemo ya uwepo wa viwanda bubu na pombe zinazochanganywa na spirit ya viwandani.

pombe nooma.JPG
 
Dah..viroba kweli ni tatizo mana ni very cheap kwa mlevi yoyote kununua..hivyo kupelekea unywaji ovyo..nivyema vipigwe marufuku...
 
Dah..viroba kweli ni tatizo mana ni very cheap kwa mlevi yoyote kununua..hivyo kupelekea unywaji ovyo..nivyema vipigwe marufuku...
Cheap kuliko gongo?
Ishu ni kwamba mtu aliyekusudia kulewa na hana hela ya bia akitaka kulewa atapata tu pombe kwa hela aliyonayo(hapa naongelea pombe za gharama ya tsh 200~1000)
 
Clouds fm walivyo wanafiki eti leo wakawa wanasifia matumizi ya bia,hawajui bia ilivyo na uraibu mbaya kama marekani ndio huwa inaongoza kwa death rate..
Uliza jinsi pale muhimbili madaktari walivyo busy kutibu wahanga wa pombe Kali! Maini hakuna tena!

Pombe Kali zinaongoza kwa ufeki!
 
Nakumbuka mwaka Jana mwezi flani waziri wa mazingira alisema kufikia January 2017 pombe za viroba hazitakuwepo watatafuta vifungashio vingine ili kutunza mazingira lakini hadi Leo zipo na zinaendelea kuzalishwa ,Sasa huyu naibu waziri wa afya kasema hadi kufikia June 2017 serikali itapiga marufuku utengenezwaji wa viroba ,hizi kiki zingine bhana viroba hata wakizuia ni kazi bure pale tofauti ni vifungashio ila pombe ni Ile Ile watapiga marufuku konyagi ya karatasi wakati ya kwenye chupa ni ile Ile watapiga marufuku Kiroba oriGINal wakati Ile ni K-VANT hizi kiki za wanasiasa bhana zinachosha
 
hivi ishu ya mifuko ya plastiki iliishia wapi? Maana walisema January ndio mwisho lakini hadi sasa imejaa tele mitaani.
 
Back
Top Bottom