KIGWANGALLA: Serikali haitaruhusu tena usafirishaji wa Wanyampori kwenda nje

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema Serikali haitaruhusu tena usafirishaji wa wanyama pori hai kutoka Tanzania kwenda nchi nyingine

Waziri Kigwangalla amesema wanaenda kubadilisha sheria ili kupiga marufuku kabisa biashara hii

Ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa ni wakati akijibu zuio la kuuza vipepeo nje ya Tanzania linaisha lini
 
Hii ni kauli mpya au ilishatolewa huko nyuma? Zuio ni jipya au ni kuendeleza lililokuwepo.
 
Kingwangala Vipi ule mpango wa kutaka kumfungulia mashtaka Nyalandu kwa kupeleka wanyama pori nje?
 
Uko kijijini kwetu wakulima wanasumbuliwa na nyani kwa kula mazao yao. Sasa nyani huyo akisafirishwa njeya nchi anauzwa walau kwa dola . Wizara ya kilimo inaua ndege wanao haribu mazao wakati huo huo msafirishaji akiuza hao ndege nje atapata hela za kigeni. Tuna nyoka wengi ambao wengi wa aina ya nyoka hao ni hatari kwa binadamu na wakiuzwa nje si tunapata hela za kigeni? Hii mijusi ambayo inatukela majumbani huko nje wanahitaji sasa kwa nini isiuzwe kusudi nchi ipate dola? Hawa wafanya biashara wanasafirisha panzi, ng`e, tandu, mavunja jungu nk kuna hasara gani tunaipata wakati serikali inapata kodi na kufaidika na hela za nje?Kama mtanzania unaingia hasara gani kwa kuuza viumbe kama hivyo?
Sasa unakataza kusafirisha wakati huo huo unaruhusu kuwinda na kuua wanyama pori. Hiyo sio double standard?
Hii biashara ilisaidia sana Watanzania kwa kupata ajira na kuingizia kiapato serikali. Serikali itabidi iangalie vizuri faida na hasara itakayoipata
 
Back
Top Bottom