Kigwangalla: Nitakuwa wa kwanza kumuunga mkono Membe urais 2015

Mbona hata Kigwa mwenyewe naskia anautaka Urais? Na keshaanza kupiga jaramba kwa ziara za nje na Rais!
 
Waandishi wa habari wameshindwa kumuuliza Dr Hamis Kigwangalla maswali ambayo nilifikiri ni muhimu wakati anatangaza nia yake ya kugombea urais mwakani.

Mosi, kwa mujibu wa wasifu wake ulioko kwenye tovuti ya bunge, atakuwa hajafikisha miaka 40 CCM itakapochangua mgombea wake wa urais.

Pili, Dr Kigwangalla alinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana mwezi wa tatu akisema kuwa Waziri Membe alikuwa rais kwa asilimia 60 na yeye alikuwa anamuunga mkono.

Kigwangala.jpg
 
Hii ni kutudharau watz maana anajua kama Chama chake Kikimpitisha watz tutampigia kura maana hatujui kipi ni bora na kipi ni bogus........ili mradi tumekula Wali na kupewa kanga.
 
Mkuu kwani si alisema kuwa wakati yuko nje mh. rais alimkaimisha kiti chake kwa muda akaenjoy?
 
Ama kweli mheshimiwa dhaifu ameiharibu taasisi ya Uraisi , mpaka wasionaakili wanahisi wataweza kuongoza Nchi yetu.
 
Hii ni kutudharau watz maana anajua kama Chama chake Kikimpitisha watz tutampigia kura maana hatujui kipi ni bora na kipi ni bogus........ili mradi tumekula Wali na kupewa kanga.

Nimeamini kuwa ccm hawana adabu wala huruma hata kidogo Kwa wa TZ.
 
Hatuna waandishi wa habari Tanzania ......

Mkuu wapo ila ni wachache sana na wengi wamekimbilia huko TMF au kwenye mashirika kadhaa kama maafisa habari ndio kuna maslahi ila huku kwingine ni shidaa mkuu, nilipita hapo ilala siku moja kuna vyuo vyao nikakoma kabisa, nilikaa kwenye kamgahawa kamoja walikuwapo wadada ni wanafunzi wa uandishi, mwanzo mwisho ndani ya dakika 30 walikuwa wanamuongelea mtu anaitwa DIDA, wanaongelea kuachika kwake........mezani magazeti ya udaku, sikuona Mwananchi, Citizen, Nipashe wala gazeti lolote makini.......nikajiuliza hv hawa wakitoka hapa watakwenda kuandika au kuhoji nini, mbona wamekaa kidaku sana.
 
Ukiniuliza Kigwangali kalifanyanini Taifa hadi agombee Uraisi sifahamu wala sijui, zaidi ya kumuona kwenye media tu.
 
Back
Top Bottom