HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 717
- 971
Ndugu zangu,
Jana nikiwa Arusha metro niliamua kukodi bodaboda na kuomba nipelekwe kwenye mashine ya ATM ya NBC nichukue pesa kwa ajili ya matumizi yangu. Nilipofika kwenye ATM wakati nataka kushuka nikafikiria kwa haraka tu na kuamua kutaka kuchukua picha kasha niiweke kwenye Facebook page yangu facebook.com/hamisi.kigwangalla). Baada ya kufanya hivyo mjadala mkali uliibuka pale na leo nilipoamka asubuhi nikaambiwa mjadala umehamia JF. Pamoja na kujibu hoja mbalimbali zilizowekwa pale na wachangiaji wenzangu nimepata maswali kadhaa ya kujiuliza: hivi kupanda pikipiki ni sifa? Hivi kuwa maskini ni sifa? Nimeona niwashirikishe na wenzangu hapa, tufikiri kwa kupaza sauti kidogo.
Kuwa na gari ama kutembelea gari ni jambo linaloashiria mafanikio kwa wengi, kwa huku kwetu Afrika. Maana kadri chomco cha usafiri kinavyozidi kuwa kidogo ndipo hatari ya kusababisha ajali yenye kuua inavyoongezeka, wataalamu wanaviita vyombo hivi (km baiskeli na pikipiki) kuwa ni ‘vulnerable'. Na mara nyingi ukubwa na usalama wa chombo unaongezeka kutokana na hadhi na kiwango cha uchumi cha mmliki/mtumiaji. Hivyo mwenye hadhi na pesa nyingi anatarajiwa kuwa na chombo kikubwa na salama zaidi, maana kwake usalama ni muhimu zaidi kuliko kufika aendako tu. Ni katika mazingira gani sasa Mwanansiasa Mbunge kama mimi ninapoamua kupanda Bajaj ama Bodaboda wananchi wenzangu waone kuwa ni jambo la kutafuta sifa kisiasa?
Kwa mtu kama mimi kupanda pikipiki siyo jambo la ajabu sana na wala siyo la kuzua mjadala, maana nimekulia kwenye umaskini wa hali ya juu lakini siupendi umaskini na ndiyo maana napambana nao kila kukicha mimi binafsi na katika jamii, na ninapenda kuhakikisha umaskini wa kutupwa hapa Tanzania unatoweka - huo ndiyo mchango ninaoendelea kuutoa ili kulipa fadhila kwa nchi yangu kwa kunipa fursa ya elimu na ya ajira. Kwa sisi tuliokulia kwenye shida za umaskini, tuliowahi kupitia maisha ya mlo mmoja kwa siku, kwenda shule bila viatu, kucheza mpira bila viatu tunaelewa kwa nini tupigane kuondoa umaskini kwa watu wote.
Na wala kupanda pikipiki siyo jambo la ‘kujionyesha', ni umaskini na haupaswi kukubalika – japokuwa kwa kuwa tuko katika hatua za awali za kupambana na umaskini, ni lazima tukubali kipindi hiki ni cha mpito na matumizi ya vifaa kama baiskeli, pikipiki, boti za kusukumwa na mikono, tuk-tuk kama vyombo vya kubebea abiria hatuwezi kuukwepa. Ila hili lisiwe ni jambo eti la kujidaisha kwamba Mbunge kama mimi naishi maisha ya chini sawa na 'ordinary citizen', kwangu mimi ntahoji who is ordinary na who is extra-ordinary, na why these classes? Na je kuna uhalali wowote ule wa kuwa na watu wa kawaida na wale wasio wa kawaida?
Mimi naamini nimepewa fursa hii kwa sababu, na wala si kwa ajili ya kuendelea kuwa na raha bali kwa ajili ya kutoa mchango utakaowapa wengine kama mimi fursa za kuboresha maisha yao. Na siwezi kuwa mtu wa ku-pretend kuwa pamoja na watu wa 'kawaida' kwa faida za kisiasa. Take it or leave it, wengine tuko orijino na tuna sababu za kuwa hivi tulivyo!
Mwisho, napenda kutoa taarifa kwamba, hiyo picha mliyoiona hapa ni ya kwangu na nilipigwa kwa maksudi wala siyo kwa bahati mbaya...na nimeiweka mwenyewe kwenye facebook page yangu kwa malengo ya kuchochea mjadala wa usalama kwenye chombo hiki kinachotumiwa na watu wengi kwa sasa hapa nchini, mijini na vijijini, na wala siyo kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa kupitia kujifanya mimi ni maskini na niko sawa na watu maskini, ukweli uko wazi kama nilivyosema hapo juu kwamba nimezaliwa maskini na siwezi kuendelea kuikumbatia hali hiyo – nitaendelea kupigana kuondokana na umaskini, maana naamini siyo sifa nzuri kuzaliwa maskini, kukua maskini, na kufa maskini! Kuzaliwa maskini haikuwa chaguo langu lakini naamini kufa maskini itakuwa ni anguko langu na uzembe wangu! Tanzania na dunia inatoa fursa nyingi, tuzitumieni kuukataa umaskini. Kuwa tajiri siyo dhambi!
Jimboni kwangu Nzega wananifahamu fika na siwezi kujidai leo nimekuwa motto wa uzunguni wakati mimi ni kijana orijino wa uswazi. Hivyo kwao siyo jambo la ajabu kabisa kuniona nikila mahindi barabarani, kuniona nikinywa nao kahawa ama chai, ama uji, na mihogo ama na viazi – kwa kuwa wanajua hivyo ndivyo vilivyonikuza. Wanajua kwetu hakukuwa na magari ya kifahari, kulikuwa na baiskeli na tela la punda kwa ajili ya kufanyia kazi zetu.
Wakatabahu,
HK.