Kigwangalla na Hoja ya Kutafuta Umaarufu wa Kisiasa Kupitia Kupanda Bajaj ama Bodaboda!

HKigwangalla

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
717
971
Ndugu zangu,

Jana nikiwa Arusha metro niliamua kukodi bodaboda na kuomba nipelekwe kwenye mashine ya ATM ya NBC nichukue pesa kwa ajili ya matumizi yangu. Nilipofika kwenye ATM wakati nataka kushuka nikafikiria kwa haraka tu na kuamua kutaka kuchukua picha kasha niiweke kwenye Facebook page yangu facebook.com/hamisi.kigwangalla). Baada ya kufanya hivyo mjadala mkali uliibuka pale na leo nilipoamka asubuhi nikaambiwa mjadala umehamia JF. Pamoja na kujibu hoja mbalimbali zilizowekwa pale na wachangiaji wenzangu nimepata maswali kadhaa ya kujiuliza: hivi kupanda pikipiki ni sifa? Hivi kuwa maskini ni sifa? Nimeona niwashirikishe na wenzangu hapa, tufikiri kwa kupaza sauti kidogo.

Kuwa na gari ama kutembelea gari ni jambo linaloashiria mafanikio kwa wengi, kwa huku kwetu Afrika. Maana kadri chomco cha usafiri kinavyozidi kuwa kidogo ndipo hatari ya kusababisha ajali yenye kuua inavyoongezeka, wataalamu wanaviita vyombo hivi (km baiskeli na pikipiki) kuwa ni ‘vulnerable'. Na mara nyingi ukubwa na usalama wa chombo unaongezeka kutokana na hadhi na kiwango cha uchumi cha mmliki/mtumiaji. Hivyo mwenye hadhi na pesa nyingi anatarajiwa kuwa na chombo kikubwa na salama zaidi, maana kwake usalama ni muhimu zaidi kuliko kufika aendako tu. Ni katika mazingira gani sasa Mwanansiasa Mbunge kama mimi ninapoamua kupanda Bajaj ama Bodaboda wananchi wenzangu waone kuwa ni jambo la kutafuta sifa kisiasa?

Kwa mtu kama mimi kupanda pikipiki siyo jambo la ajabu sana na wala siyo la kuzua mjadala, maana nimekulia kwenye umaskini wa hali ya juu lakini siupendi umaskini na ndiyo maana napambana nao kila kukicha mimi binafsi na katika jamii, na ninapenda kuhakikisha umaskini wa kutupwa hapa Tanzania unatoweka - huo ndiyo mchango ninaoendelea kuutoa ili kulipa fadhila kwa nchi yangu kwa kunipa fursa ya elimu na ya ajira. Kwa sisi tuliokulia kwenye shida za umaskini, tuliowahi kupitia maisha ya mlo mmoja kwa siku, kwenda shule bila viatu, kucheza mpira bila viatu tunaelewa kwa nini tupigane kuondoa umaskini kwa watu wote.

Na wala kupanda pikipiki siyo jambo la ‘kujionyesha', ni umaskini na haupaswi kukubalika – japokuwa kwa kuwa tuko katika hatua za awali za kupambana na umaskini, ni lazima tukubali kipindi hiki ni cha mpito na matumizi ya vifaa kama baiskeli, pikipiki, boti za kusukumwa na mikono, tuk-tuk kama vyombo vya kubebea abiria hatuwezi kuukwepa. Ila hili lisiwe ni jambo eti la kujidaisha kwamba Mbunge kama mimi naishi maisha ya chini sawa na 'ordinary citizen', kwangu mimi ntahoji who is ordinary na who is extra-ordinary, na why these classes? Na je kuna uhalali wowote ule wa kuwa na watu wa kawaida na wale wasio wa kawaida?

Mimi naamini nimepewa fursa hii kwa sababu, na wala si kwa ajili ya kuendelea kuwa na raha bali kwa ajili ya kutoa mchango utakaowapa wengine kama mimi fursa za kuboresha maisha yao. Na siwezi kuwa mtu wa ku-pretend kuwa pamoja na watu wa 'kawaida' kwa faida za kisiasa. Take it or leave it, wengine tuko orijino na tuna sababu za kuwa hivi tulivyo!

Mwisho, napenda kutoa taarifa kwamba, hiyo picha mliyoiona hapa ni ya kwangu na nilipigwa kwa maksudi wala siyo kwa bahati mbaya...na nimeiweka mwenyewe kwenye facebook page yangu kwa malengo ya kuchochea mjadala wa usalama kwenye chombo hiki kinachotumiwa na watu wengi kwa sasa hapa nchini, mijini na vijijini, na wala siyo kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa kupitia kujifanya mimi ni maskini na niko sawa na watu maskini, ukweli uko wazi kama nilivyosema hapo juu kwamba nimezaliwa maskini na siwezi kuendelea kuikumbatia hali hiyo – nitaendelea kupigana kuondokana na umaskini, maana naamini siyo sifa nzuri kuzaliwa maskini, kukua maskini, na kufa maskini! Kuzaliwa maskini haikuwa chaguo langu lakini naamini kufa maskini itakuwa ni anguko langu na uzembe wangu! Tanzania na dunia inatoa fursa nyingi, tuzitumieni kuukataa umaskini. Kuwa tajiri siyo dhambi!

Jimboni kwangu Nzega wananifahamu fika na siwezi kujidai leo nimekuwa motto wa uzunguni wakati mimi ni kijana orijino wa uswazi. Hivyo kwao siyo jambo la ajabu kabisa kuniona nikila mahindi barabarani, kuniona nikinywa nao kahawa ama chai, ama uji, na mihogo ama na viazi – kwa kuwa wanajua hivyo ndivyo vilivyonikuza. Wanajua kwetu hakukuwa na magari ya kifahari, kulikuwa na baiskeli na tela la punda kwa ajili ya kufanyia kazi zetu.

Wakatabahu,
HK.
 
H.K yale yale ya J.Makamba kupanda bajaji ni kutafuta huruma ya wananchi(wapiga kura)....
 
Ndugu Kigangwalla mi naona tu umeamua kuchokoza mada hasa ukizingatia juma chache zilizopita tulikuwa na mjadala mkali kwa suala kama lako mhusika akiwa Mbunge mwenzio Ndugu January Makamba.

Mbali na kutovaa protective helmet hapa nadhani mjadala utakuwa kwanini upande bodaboda na kujifotoa. Wengi wameona ni kuhadaa Wananchi ya kuwa uko karibu nao, kuwa nawe ni wa kawaida.......mimi nimeona ni matangazo tu, hakuna cha ziada
 
Nadhani kama kiongozi na mtu unayefahamika kwa kiasi, kama wewe kuna baadhi ya mambo hutakiwi kufanya kama vile kupanda bajaji isipokuwa kama unamalengo ya kunasa hisia za watu,kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii nk.

Wewe ni dktari, na mbunge hupaswi kuishi kama wasanii. I can smell ur a one term mp.

Nzega maisha ni magumu,maji hakuna,madawa hakuna,shule duni halafu badala ya kutuomba tukusaidie mawazo ya kuboresha maisha ya watz unakaa kupiga picha na kuziweka facebook.
 
Mkuu huoni Kuwa kupanda pikipiki na sandals bila helmet ulihatarisha usalama wako?

Tuyaache hayo Usalama wa waendesha na wapanda bodaboda Arusha ni mdogo sana! Pikipiki Nyingi huwa na helmet moja tu ya dereva na hili ni kawaida kwa Arusha tofauti na Mikoa mingine Kama Tanga bodaboda huwa na helmet mbili, waendesha magari hasa madereva wa hiace Arusha hawawajali kabisa waendesha pikipiki na baiskeli. Pia waendesha bodaboda ni mbumbumbu kabisa wa Sheria za barabarani Kama mwakilishi wa wananchi utatusaidia vipi je uko tayari kuwasilisha hoja au mswada wa kufanya hili liangaliwe kwa jicho la tatu?

HKigangwalla Coz kwa mwaka huu vijana watatu wa mtaani kwetu wamepoteza maisha tena mmoja wa umri wa miaka 17 tu.. Na hizi helmet feki zimezagaa sana mtaani, Sasa Kama Lengo lilikuwa ni kuibua mjadala wa usalama kuhusu bodaboda usiishie tu kupiga nazo picha take step ahead!
 
You were just seeking cheap publicity and worse enough you had no protective gear which is against the law. Next time think deep before you act.
 
Kwa ujumla mi sioni msingi wa wewe kujitetea, kwani gari lako lilikua wapi? Kama uliliacha Nzega na ukatumia public transport to Arusha sioni shida yoyote wewe kupanda Bodaboda au Bajaj, au uliishiwa mafuta kwenye gari lako then ukaona uende bank na kuchukua vijisenti ili uweke mafuta kwenye gari, bado hapo sioni shida, shida yangu iko hapa; Kama ulipanda kwa nia nzuri tu, suala la wewe kupiga picha na kuitangaza, lengo lako ni lipi?

Ulitaka tukuone we ni mtoto wa masikini mwenzetu au na wewe tuko pamoja kwenye usafiri wetu huu ambao we mwenyewe umesema risk za ajali ni kubwa? Sijaelewa hayo, labda kama waweza kuja tena na kujibu maswali hayo tu.
 
Nadhani kama kiongozi na mtu unayefahamika kwa kiasi, kama wewe kuna baadhi ya mambo hutakiwi kufanya kama vile kupanda bajaji isipokuwa kama unamalengo ya kunasa hisia za watu,kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii nk.

Wewe ni dktari, na mbunge hupaswi kuishi kama wasanii. I can smell ur a one term mp.

Nzega maisha ni magumu,maji hakuna,madawa hakuna,shule duni halafu badala ya kutuomba tukusaidie mawazo ya kuboresha maisha ya watz unakaa kupiga picha na kuziweka facebook.
Ndg. Mabewa,

Ubunge ni kazi ngumu sana na si sifa sana kuwa Mbunge hususan kama una mambo mengine ya kufanya, ni lawama, chuki, fitna, husda, majungu na kashfa kama unavyoona hapa. Binafsi nilipanga kuwa mbunge wa mihula miwili tu kisha nistaafu bila hata kugombea, leo hii nakuambia nina-contemplate kutogombea hata hiyo ya pili tena - so wala usidhani hicho kinanikosesha sana usingizi!

Unapoongea hayo mambo maisha magumu, maji, madwa, shule - hebu nipe muda nifanye kazi kisha 2014 ama 2015 uniulize nimefanya nini, sasa hivi najipanga tu na utekelezaji wa baadhi ya miradi ndiyo kwanza umeanza, sasa usitegemee mambo yatabadilika over nyt.

wakatabahu,
HK.
 
Kwa ujumla mi sioni msingi wa wewe kujitetea, kwani gari lako lilikua wapi? Kama uliliacha Nzega na ukatumia public transport to Arusha sioni shida yoyote wewe kupanda Bodaboda au Bajaj, au uliishiwa mafuta kwenye gari lako then ukaona uende bank na kuchukua vijisenti ili uweke mafuta kwenye gari, bado hapo sioni shida, shida yangu iko hapa; Kama ulipanda kwa nia nzuri tu, suala la wewe kupiga picha na kuitangaza, lengo lako ni lipi?

Ulitaka tukuone we ni mtoto wa masikini mwenzetu au na wewe tuko pamoja kwenye usafiri wetu huu ambao we mwenyewe umesema risk za ajali ni kubwa? Sijaelewa hayo, labda kama waweza kuja tena na kujibu maswali hayo tu.

Ndg. Mazindu,
Kutwa na gari Arusha ama kutokuwa nalo si ishu sana hapa, kwa sababu ningeweza kupanda taxi.
Kupiga picha na kuiweka FB, kama nilivyoeleza hapo juu, lengo lilikuwa kuanzisha mjadala (kama huu unaoendelea) wa safety promotion - nenda kasome post yangu ya FB utaona maelezo yanayoambatana na picha hiyo.

Re,
HK.
 
You were just seeking cheap publicity and worse enough you had no protective gear which is against the law. Next time think deep before you act.
Ndg. Captain,

Which law Sir? I was not riding it...sheria ina mapungufu na hayo ninapaswa kuya-address kama mtunga sheria na nimesema nitafanya hivyo.

Kutafuta Publicity siyo dhambi kwa mwanasiasa kwa sababu ni kazi yake! Sasa unategemea nisipokuwa maarufu nitaendeleaje kuchaguliwa na wananchi? Ni lazima nitafute umaarufu, tena KTY nina timu kabisa ya kunifanyia publicity na inafanya kazi yake vizuri. Sema unatafuta umaarufu kwa jambo lipi haswa...la kujifanya uko sawa na maskini ama kwa kuonesha namna ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii?

Pia publicity ni muhimu kwa sababu inahamasisha democracy na accountability - ambayo tunaihitaji sana kama Taifa linaloendelea.

Tatu, publicity inasaidia kufanya uraghibishi (advocacy) na hatimaye kuleta mabadiliko tunayoyahitaji - hivyo mwanasiasa kama advocate wa maendeleo ni lazima uwe na mikakati ya publicity ili kuwafikia wananchi na hata viongozi wenzako!
Ni nyie msio wanasiasa ndo mnapata tabu sana mnapoona sisi wanasiasa tunatafuta umaarufu - lakini in actual sense ni lazima tufanye hivyo kwa faida yenu wananchi.

Wakatabahu,
HK.
 
Ndg. Mazindu,
Kutwa na gari Arusha ama kutokuwa nalo si ishu sana hapa, kwa sababu ningeweza kupanda taxi.
Kupiga picha na kuiweka FB, kama nilivyoeleza hapo juu, lengo lilikuwa kuanzisha mjadala (kama huu unaoendelea) wa safety promotion - nenda kasome post yangu ya FB utaona maelezo yanayoambatana na picha hiyo.

Re,
HK.

kama ishu ni safety, nenda pia pale kwa mrina au picnic kamata wale wadada wanaofanya biashara ile haramu then piga nao picha , bahati nzuri wewe ni daktari ili uwasaidie kujua uslama wao wakiwa kazini, nitafurahi nikiona picha yako na hao dada zetu.
 
Maana kadri chombo cha usafiri kinavyozidi kuwa kidogo ndipo hatari ya kusababisha ajali inavyoongezeka, wataalamu wanaviita vyombo hivi (km baiskeli na pikipiki) kuwa ni ‘vulnerable’.

nimeiweka mwenyewe kwenye facebook page yangu kwa malengo ya kuchochea mjadala wa usalama kwenye chombo hiki kinachotumiwa na watu wengi kwa sasa hapa nchini, mijini na vijijini.
HK.

Vyema.

Pengine ulikuwa na lengo zuri sana, lakini ulivyoliwasilisha imekuwa sivyo. Kumbuka juzijuzi tu hapa January naye aliweka picha kama yako. Sasa hii ni coincidence au jambo la kutokea?!?

Nikirudi kwenye lengo lako kuu. Hongera sana kwa kutaka kuchochea mjadala wa aina hii.

Lakini ni ajabu sana serikali ya chama chako inaona vyombo hivyo ni fursa ya kutoa ajira kwa vijana. Ndiyo maana imeamua na kutoa au kupunguza kodi katika vyombo hivyo ili vijana wavinunue!!

Sasa kama mbunge, na mtu unaeelewa namna vyombo visivyo salama kwa watumiaji, umeshafanya nini kuishauri na kuisimamia serikali!

Pili, serikali ya chama chako, inafanya nini kutatua kero ya usafiri vijijini na maeneo ya pembezoni mwa mijini?
Wewe kama mbunge umefanya nini katika hilo?
Maana serikali haijaonyesha jitihada za ziada; kwa kuweka mazingira ya kuongeza vyombo hivyo, sidhani kama kuna jitihada za kweli kuboresha usafiri wa uhakika na usalama.

Kwa nini vyombo hivyo visipigwe marufuku? (Hapa inabidi political interests ziwekwe kando). Pigeni marufuku vyombo hivyo nchi nzima; na tumieni rasilimali za taifa katika kuweka misingi ya uwepo wa vyombo vya uhakika na usalama mijini na vijijini. Taifa letu lilipaswa kuwa na barabara za uhakika kila kona sasa.

Kama kweli unataka mjadala huu uchochewe, wasilisha hoja bungeni ya kupiga marufuku vyombo hivyo.
 
"In search of an ATM this evening in dowtown Arusha I boarded 'Kibodaboda'; the following quickly crossed my mind: efficient commuting cheap and affordable to many, income generating to urban as well as rural youth,high risk of deadly accidents - appropriate education and regulation is needed to promote safety!"

Maandishi hayo ndio nukuu ya ulichokiandika katika ukurasa wako wa FB.

"high risk of deadly accidents - appropriate education and regulation is needed to promote safety!"

Hoja na kinachoshindwa kuwaingia watu akilini ni katika hiyo statement niliyoinyofoa kutoka katika nukuu yako, unaweza vipi ku-promote safety ilihali huoneshi jitihada hata ya kuvaa kikinga kichwa "helmet"?
 
Back
Top Bottom