Kigwangalla: Katibu Mkuu wa CHADEMA ana kashfa ya kuongoza migomo ya madaktari Tanzania

....suala lingine linalobishaniwa hapa kuhusu nani alishiriki mgomo upi ni vizuri kuwekana sawa; mgomo ambao Kigwangalla na pengine Mashinji alishiriki ni wa mwaka 2005 na sio huu wa majuzi ambao ulihusisha Ulimboka kutekwa nk. Ni vizuri kujua kuwa mwaka 2005 wakati wa mgomo huo Dr. Ulimboka na Hamisi Kigwangalla (ambao ni clasmates) walikuwa interns na Mashinji wakati huo alikuwa ni MMed student.
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli regardless Dr. Mashinji ni Katibu Mkuu wa CDM ama la; na ukweli wenyewe ni kuwa hakuwahi kumaliza Mstarters of medicine ya Anaesthesia. Hata hivyo sababu za kutomaliza kwake hazimuondolei sifa zake nyingine. Ushauri wa bure ni yeye mwenyewe kuandaa CV yake ''official'' ili kuondoa mikanganyiko. Nimeona kwenye vyombo vya habari kuna upotoshaji ambao (kwa maoni yangu) unatokana na uelewa mdogo wa waandishi wa habari na tafsiri potofu ya kiingereza. Mfano, Kuna gazeti limeandika alikuwa mtaalamu mshauri kwenye mradi wa dunia .....wakitafsiri neno Global programme.
Andaa wewe ulete hapa mana si Unaijua au na wewe ni walewale
 
Muislamu Kigwangala aliongoza Mgomo mpaka watu wakapoteza maisha. Leo Rais akimtumbua tutasema ahaa mbona waislamu wanatumbuliwa wakati kosa alilolifanya ni la wazi kabisa
Mpaka utaje dini yake ndiyo uungwe mkono!
 
kipindi hicho nilikwenda Mh2 wadi ya Mwaisela nikakuta utepe kwenye mlango wa kuingilia, nilipouliza nikaambiwa kuna shughuli maalum. Ile kuchungulia ndani nikaona zinakusanywa maiti zisizopungua kumi. nilipopata upenyo wa kuingia ndani nikawauliza wagonjwa waliobaki bila matumaini, wakanijibu, "maiti nyingine ni za toka juzi, hizo ulizoona ni awamu ya tatu tangu asubuhi. kesho njoo ushuhudie maiti zetu".
katika hali kama hiyo, anapojitokeza mtu kujisifia kusababisha matatizo yote hayo na bado akabaki madarakani!. only in Bongo
 
Andaa wewe ulete hapa mana si Unaijua au na wewe ni walewale
Wale wale wakina nani? tuache mihemuko na tuchangie kama watu wazima. katazame tena wasifu wake ulivyoandikwa, Mmed ni miaka mitatu hakumaliza. Niesema hapo juu, sababu za kutomaliza hazimuondolei sifa yeyote kwa kuwa hakushindwa (kufeli) kumaliza...
 

Zikiwa zimepita siku mbili toka kupatikana kwa Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA Dk Vincent Mashinji, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ameibuka na kuwapa pole CHADEMA kama walimchagua Katibu Mkuu wao kwa kuangalia historia yake. Kupitia Account yake ya Facebook Dk Hamisi Kigwangalla anakiri wazi kuwa Dkt. Mashinji ni msomi...


Katoa pole eti kwa CHADEMA kama inavyosomeka hapo juu,

Na Stan Katabalo angekuwa hai angewapa pole CCM kumchagua Kinana kuwa katibu wao mkuu, hapo hapo kakili kwamba Mashinji ni msomi,hata Stan Katabalo angekili kuwa Kinana alikuwa ni mtu kati katika kuuza ardhi ya Loliondo, pia angakili kuwa Kinana ni jangili.

Na Mzee Nyerere angekuwa hai angewapa pole CCM kwa kumpa ubunge Aden Rage.


CV ya Kinana iko CHINA,SOMALIA HONGKONG MPAKA BRAZIL.
Dr. Kigwa ukiwapa pole wenzio na wewe utapewa ya kwako
 
Hayo yote yanazidi kumjenga kisakioloji dr machinji azidi kuwa imara zaidi.
 
kisa cha kutoa pole ni nini? historia gani mbaya ya majinji hahaha asavali mneweka picha nimemfaham huyu kigwangala
 
kwa wale vijana wa Lumumba muliokuwa mmeanza kumshambulia katibu mkuu wa CHADEMA kuwa aliongoza migomo ya madaktari iliyopelekea vifo vya watanzania, nadhani bosi wenu Dr kigwangalla ameweka wazi kuwa katibu huyo hakuwahi kuwa mbele ya Jambo hilo badala yake kigwangalla na wenzake ndo waasisi wa vuguvugu hizo.
 
  • Thanks
Reactions: Awo
Hamisi Kigwangalla

Ndg. Dkt. Mashinji is a friend, brother and colleague. Hakuwahi kutuokoa mimi na Dkt. Ulimboka na hakuwahi kuongoza mgomo, sema alishiriki mgomo ulioongozwa na mimi na Dkt. Ulimboka.

Kiukweli, ni mwanasiasa mzuri, msemaji, msomi mzuri (tumesoma naye MBA chuo kimoja), sina hakika kama alimaliza masomo ya Ubingwa maana alinyanyaswa na Supervisor wake, akasusa akaamua kujiunga masomo ya
MBA, na sina hakika sana kuhusu 'msimamo usiotetereka'. Maana baada ya vitisho vya 2005, aliyumba sana na tulimtenga na ku-aVoiD kumualika vikao vya CC ya mgomo.

Hivyo, kama kigezo kilikuwa ni hii Historia, pole kwa CHADEMA.
Mwambie akamalizane na dr. Mwaka kwanza, this war is far above his head. Nakuwaga na was was sana na uwezo wa kufikiri wa Huyu dr.....
 
Hili baraza la mawaziri la magufuli limejaa kashfa tupu, nashindwa kuelewa wanaomsifia wanatumia vigezo gani wakati baraza la mawaziri lote karudisha/ karudishiwa majipu matupu.
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli regardless Dr. Mashinji ni Katibu Mkuu wa CDM ama la; na ukweli wenyewe ni kuwa hakuwahi kumaliza Mstarters of medicine ya Anaesthesia. Hata hivyo sababu za kutomaliza kwake hazimuondolei sifa zake nyingine. Ushauri wa bure ni yeye mwenyewe kuandaa CV yake ''official'' ili kuondoa mikanganyiko. Nimeona kwenye vyombo vya habari kuna upotoshaji ambao (kwa maoni yangu) unatokana na uelewa mdogo wa waandishi wa habari na tafsiri potofu ya kiingereza. Mfano, Kuna gazeti limeandika alikuwa mtaalamu mshauri kwenye mradi wa dunia .....wakitafsiri neno Global programme.
Na hii ni ID yako nyingine.
 
Wale wapiga filimbi kwamba walioshiriki mgomo waliua Watanzania jitokezeni kama mlivyomkurupukia Dr. Mashinji maana mwenye kustahili kaja. Mwambieni Magu amtumbue jipu Kigwangalla maana anajisifu kwa kuongoza harakati za mgomo na kushinikiza mauaji ya Watanzania waliokosa huduma hospitalini tena kibaya zaidi ni wale Watanzania ambao Mhe.Magufuli amesema amejitoa kafara kwa ajili yao.
 
Nakujua. Nawe wanijua. Chamani na maishani. Una makandokando mengi. Kuanzia jina,elimu,ubunge hadi unaibu uwaziri ulionao. Yaani,unaishi nyumba ya vioo. Utauweza ugomvi wa mawe unaouanzisha?

Kumchokoza Katibu Mkuu wa CHADEMA ni kuwachokoza wote chamani mwao. Wao ni wasemaji wa lolote. Wakikurudi,usikimbilie msaada wa chama au vyombo vya dola. Umejipanga na kupangika? We haya tu!

Mkuu Kigwa,umefikia wapi na akina Dr. Mwaka na lile geti la Wizara yako? CHADEMA wakijibu mapigo,endelea. Usikimbie!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom