Kigwangalla: Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri, bila utekelezaji ni kazi bure

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,291
"Katiba ya Marekani ya Mwaka 1789 iliandika ‘all men are created equal’ lakini bado miaka 180 baadaye bi. Rosa Park alitakiwa kumpisha kiti dume la kizungu! Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri, bila utekelezaji ni kazi bure.Kwa kuwa hii inatoa haki, usawa na amani, tuiheshimu."

"Kwa kuzingatia Katiba yetu ilipotoka, na uwepo wa mabadiliko makubwa ya mwaka 1984, na jinsi ilivyoweza kutuvusha kwenye kipindi kigumu cha msiba mzito kwa amani, na ilivyoweza kudumisha Muungano wetu kwa kipindi chote hiki, mabadiliko ya Katiba yanaweza kusubiri kidogo kwanza."- Mh. Kigwangalla

1625479446216.png
 
Kigwangallah kafilisika Sana kisiasa, haeleweki anasimamia nini
Ogopa sana mwanasiasa anayetafuta upenyo wa uteuzi hasa kama alishawahi kuonja madaraka makubwa, akaondolewa sasa muda wote moyo wake hauwezi kuwa na utulivu, ni lazima apalangane anavyoona inaweza kumfaa mteuaji akamuona na ndio tatizo la wanasiasa wengi wa kiafrika! Yaani ukiwasikiliza misimamo yao wakati wa meko na sasa ni aibu. Ni njaa tu.
 
Huyo mtekelezaji asipotekeleza atawajibishwa kulingana na sheria na kanuni zitakazokuwa zinamuongoza kwenye hiyo nafasi yake, Kigwangala kichwa maji sana.
 
Jinga kabisa hili jitu. Katiba nzuri huwa inajilinda na inajitetea yenyewe kwa kuwa inakuwa na meno makali Sana.

Ukiona katiba inachezewa kwa namna yeyote ile ujue ina mapengo au ni kibogoyo.

Kigwangalla ni mhutu au mtusi wewe?? Watanzania hatuna unafiki huu
 
"Katiba ya Marekani ya Mwaka 1789 iliandika ‘all men are created equal’ lakini bado miaka 180 baadaye bi. Rosa Park alitakiwa kumpisha kiti dume la kizungu! Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri, bila utekelezaji ni kazi bure.Kwa kuwa hii inatoa haki, usawa na amani, tuiheshimu."

"Kwa kuzingatia Katiba yetu ilipotoka, na uwepo wa mabadiliko makubwa ya mwaka 1984, na jinsi ilivyoweza kutuvusha kwenye kipindi kigumu cha msiba mzito kwa amani, na ilivyoweza kudumisha Muungano wetu kwa kipindi chote hiki, mabadiliko ya Katiba yanaweza kusubiri kidogo kwanza."- Mh. Kigwangalla

Hapo kamnukuu Kabudi. Serikali inajitahidi kila iwezavyo kuuficha moto, lakini hawezi kuuficha moshi. Katiba imewekwa viraka mpaka inachusha, na vyote viraka hivyo ni kandamizi.
 
"Katiba ya Marekani ya Mwaka 1789 iliandika ‘all men are created equal’ lakini bado miaka 180 baadaye bi. Rosa Park alitakiwa kumpisha kiti dume la kizungu! Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri, bila utekelezaji ni kazi bure.Kwa kuwa hii inatoa haki, usawa na amani, tuiheshimu."

"Kwa kuzingatia Katiba yetu ilipotoka, na uwepo wa mabadiliko makubwa ya mwaka 1984, na jinsi ilivyoweza kutuvusha kwenye kipindi kigumu cha msiba mzito kwa amani, na ilivyoweza kudumisha Muungano wetu kwa kipindi chote hiki, mabadiliko ya Katiba yanaweza kusubiri kidogo kwanza."- Mh. Kigwangalla

Very true, au ikawepo likaja lishetani lisiifuate
 
Kingwangala tafakari kwanza kabla ya kuandika.

Katiba iliyopo sana utekelezaji wake unategemea utashi wa rais aliyeko madarakani. Mfano mzuri ni jinsi rais aliyepita aliifinyanga alivyotaka na huyu wa sasa anajaribu kurudisha nchi katika utawala wa sheria. Tunataka katiba ambayo itamlazimisha rais aliyeko madarakani kufuata matakwa ya katiba na si katiba ambayo rais anaamua atakavyo na hawezi kuzuiwa na chombo chochote.
 
"Katiba ya Marekani ya Mwaka 1789 iliandika ‘all men are created equal’ lakini bado miaka 180 baadaye bi. Rosa Park alitakiwa kumpisha kiti dume la kizungu! Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri, bila utekelezaji ni kazi bure.Kwa kuwa hii inatoa haki, usawa na amani, tuiheshimu."

"Kwa kuzingatia Katiba yetu ilipotoka, na uwepo wa mabadiliko makubwa ya mwaka 1984, na jinsi ilivyoweza kutuvusha kwenye kipindi kigumu cha msiba mzito kwa amani, na ilivyoweza kudumisha Muungano wetu kwa kipindi chote hiki, mabadiliko ya Katiba yanaweza kusubiri kidogo kwanza."- Mh. Kigwangalla

Sasa Mh. Mbunge mfano katiba ikasema ili mtu aruhusiwe kugombea ubunge sharti awe na elimu ya shahada. Inamaana nalo hili haliwezi kutekelezeka. Haya katika ikasema waziri asiwe mbunge inamaana hili nalo haliwezi kutekelezeka kweli mkuu. Fikiria kwa umakini hapo.
 
"Katiba ya Marekani ya Mwaka 1789 iliandika ‘all men are created equal’ lakini bado miaka 180 baadaye bi. Rosa Park alitakiwa kumpisha kiti dume la kizungu! Katiba inaweza kuweka ‘statement’ nzuri, bila utekelezaji ni kazi bure.Kwa kuwa hii inatoa haki, usawa na amani, tuiheshimu."

"Kwa kuzingatia Katiba yetu ilipotoka, na uwepo wa mabadiliko makubwa ya mwaka 1984, na jinsi ilivyoweza kutuvusha kwenye kipindi kigumu cha msiba mzito kwa amani, na ilivyoweza kudumisha Muungano wetu kwa kipindi chote hiki, mabadiliko ya Katiba yanaweza kusubiri kidogo kwanza."- Mh. Kigwangalla

Kama akili yake imetuma hivyo sasa kwa nini tuna katiba. Basi hata hii tulivyonavyo tuachane nayo mpaka Siku tutakapojua namna ya kuitumia...
 
Si tuipate kwanza halafu tuone kama haitelelezeki? Wasiwasi wao nini kama sio mbeleko.

Mama anatakiwa aelewe kuwa, kwa tamko lake la majuzi la kuzuia mikutano ya hadhara, CCM mawilayani huko wako ziarani na wanaendelea kukusanya ada za wanachama wapya, this is very unfair.
 
Kigwangala yupo sahihi kiasi. Kwamba, kilichopo kwenye karatasi ni lazima kitekelezwe ili uzuri wake uwe na maana.

Ni lazima kuwe na ‘political will’ ya kuisimamia, kuilinda, na kutekeleza yaliyomo ndani ya katiba.

Mfano mmoja tu: katiba ya sasa inaruhusu watu kufanya siasa ndani ya Tanzania.

Rais Magufuli na Rais Samia wamesema hakuna watu kufanya siasa nje ya majimbo yao tu.

Hiyo ni kinyume na katiba.

Lakini kinachonishangaza, wale ambao wamezuiwa kufanya shughuli za kisiasa nchini, hawaikaidi hiyo amri ya marais Magufuli na Samia.

Kwa nini hao wanasiasa waliozuiwa kufanya shughuli zao hawailindi na kuipigania hiyo haki yao ya kikatiba?

Kwani wakiikaidi hiyo amri ya kufanya shughuli za kisiasa, nini kitawatokea?

Ni mahakama gani hapa Tanzania inayoweza kumpata mtu na hatia ya kutumia haki yake ya kikatiba?

Ni lazima tubadilike kifikra. Tuache uoga. Tuzilinde haki zetu wenyewe!
 
Back
Top Bottom