Kigwangalla: Hatuzungumzii tena Uchumi wa Gesi, miaka ijayo haitakuwa na maana

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,778
Mbunge wa Nzega vijijini, Hamis Kigwangala amesema uchumi wa gesi hauzungumziwi tena nchini ilhali yeye alidhani ungekuwa neema akikumbuka jinsi walivyozungumza Bungeni Mwaka 2010. Kigwangalla anasema bei ya gesi inazidi kushuka duniani.

Amesema makadirio ya bei ya Gesi miaka 15 ijayo itazidi kushuka na kumpa mashaka kizazi kijacho hakitazungumza aina ya nishati iliyopo leo.

Kigwangala amesema gesi isipotumika ipasavyo leo, itapotea bure na haitakuja kuwa na faida na kuitaka serikali kufikiria namna ya kuitumia gesi kwa namna yoyote ile badala ya kudhani kuna kufaidika zaidi mbele kuliko sasa kwani hata matarajio yalikyokuwepo miaka 11 nyuma sasa hayapo.

 
Amenena ukweli huyu mheshimiwa! Ila angeenda mbele zaidi na kusena ukweli kuwa takribani asilimia 60 ya umeme wa gridi ya taifa kwa sasa unazalishwa kwa kutumia gesi asilimia.
 
Back
Top Bottom