Kigwangalla, hakikisha kila kampuni kubwa ya utalii(Tours Companies) inapewa lengo la kuleta watalii 10 Chato, ikishindwa ipewe msukosuko

Hivi Mmarekani ataacha kwenda kuona mlima Kilimanjaro na Ngorongoro Creator umshawishi kwenda Chato?
Kwanza maoni yenu ndiyo yatawapeleka watalii huko Chato! Yaani waone na wajiridhishe kwanini wewe hutaki Chato iwe na vivutio vya kitalii! Hilo tu litavuta watalii wa nje na ndani. Ngorongoro na kilimanjaro viko Tanzania tu lakini utalii upo dunia nzima sehemu zisizo kuwa na vivutio hivyo ulivyo vitaja! Au wewe ulifikiri nchi zote zina Ngorongoro Crater na Mt. Kilimanjaro? Siyo! Wengine wana nyoka tu, wengine ndege, samaki, umasikini wa watu, hali ya hewa, jua kuchomoza na kuzama. Huko Chato - Kuona trafik light moja barabarani. Pia kuona alipozaliwa Raisi wa kipekee Tanzania etc.
 
Nashauri kwamba,njia mojawapo ya kuitambulisha mbuga hii ni kulazimisha kila kampuni kubwa ya utalii ipeleke japo watalii kumi kwa mwaka huko Burigi- Chato.

Kama kuna kampuni 2000,watalii 20000

Kampuni ikigoma vyombo vya dola,TISS,TRA,TTB,Polisi, Wizara ya Maliasili na Biashara ziwahenyeshe either kwa kuwapa madai mazito ya kodi,kutishia kuwanyima leseni,au wakurugenzi wake wahojiwe kila siku na vyombo vya dola

Nawasilisha

Kigumu chama cha mapinduzi!!!
mbona umechelewa ! huo mchakato tayari umeanza na kila kampuni ishapewa barua
 
Back
Top Bottom