Kigwangalla ateta na Mabalozi wa nchi mbalimbali kuhusu utayari wa Tanzania kupokea watalii

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1593067775679.png

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Tanzania imejipanga na iko tayari kupokea watalii kutoka katika mataifa mbalimbali ikiwemo nchi ya Sweden na Israel ambazo raia wake wamekua wakitembelea vivutio mbalimbali vya utalii vya Tanzania. Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallstig na Balozi wa Israel kwa Tanzania, Oded Joseph ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake na mabalozi wa nchi mbalimbali ambazo ni masoko makuu ya utalii kwa Tanzania.

Dkt. Kigwangalla amewaeleza mabalozi hao kuwa mikutano anayoifanya na mabalozi wa nchi mbalimbali inalenga kulinda uhifadhi na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu hatua zilizochukuliwa na Tanzania kufungua Sekta ya Utalii wakati huu wa janga la Corona na kuwaomba mabalozi hao wawahamasishe na kuwashawishi raia wa nchi zao na makampuni ya utalii yaendelee kufanya biashara ya utalii na Tanzania. Amewaeleza mabalozi hao kuwa Tanzania imekwisha fungua anga na kuruhusu ndege za abiria za kimataifa kutua hali iliyochangia kufunguka kwa Sekta ya Utalii Tanzania kutokana na utayari, mazingira salama na maandalizi mazuri ya kupokea na kuhudumia watalii watakaowasili nchini wakati huu wa janga la Corona.

Dkt. Kigwangalla amewaeleza mabalozi hao kuwa Tanzania imezindundua mwongozo wa Taifa wa uendeshaji wa shughuli za Utalii unaosimamia usalama na afya za wadau wote wanaojihusisha na sekta ya utalii wakati huu wa janga la Corona.

Aidha, amewahakikishia mabalozi hao kuwa mifumo ya huduma za afya nchini imeimarika na iko tayari kuhudumia watalii watakaokuwa wakiwasili kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii akibainisha kwamba Tanzania ina hospitali za kisasa, maabara za upimaji zenye vifaa vyote na huduma za dharula kwa watalii watakaoshukiwa au kuonesha dalili za ugonjwa wa Corona. Kwa upande wao mabalozi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa hatua na juhudi anazozifanya kuendeleza uhifadhi nchini na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi. Katika juhudi zake za kuhamasisha na kufungua sekta ya utalii Waziri Kigwangalla ameshakutana na kuzungumza na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Ujerumani, Israel, Sweden, Netherland na Finland.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Tanzania imejipanga na iko tayari kupokea watalii kutoka katika mataifa mbalimbali ikiwemo nchi ya Sweden na Israel ambazo raia wake wamekua wakitembelea vivutio mbalimbali vya utalii vya Tanzania.
KIngwangwala anapoteza muda. Haya mataifa yamesema raia wake watakaokwenda nchi ambazo hazikuchukua hatua yeyote dhidi ya Corona wakirudi kwao watafungiwa, na huenda raia wakapigwa marufuku kwenda nchi hizo. Kwa hiyo watalii wataenda Kenya., ambako Tanzania ilifikiri kwa kutochukua hatua ingebeba watalii wa Kenya

Tanzania ilijifanya ngangari wa kutoshughulikia Corona sasa inawatokea puani.
 
Mnawaita mabeberu yet you waste tax payers money to bend....na kuwalilia !
Mlijifanya kichwa ngumu.... mkajisifia sana kwa hatua feki za kuficha data.

Sasa hawa washawaambia watu wao huku noma... wasitie timu !
Now, who's the fool here ?
Wapelekeni wale wabunge wa ndioo na nyungu zao wakatalii...si washalipwa..
 
Hapo wanamuona ni kama zombie tu!!

Akiulizwa COVID-19 Status ipo vipi; jibu hawezi kuwa nalo!

Anyway, atajibu "the situation is under control"

Akiulizwa new cases ngapi; hawezi kuwa na jibu NEVER EVER na kama yupo smart, hatathubutu kusema hakuna new cases!

Wakati ule tulikuwa tunasema hakuna kosa kubwa kama kuacha kutoa takwimu kwa sababu hakuna mtu utakayemwambia COVID-19 imeisha kutokana na maombi halafu asikuone wewe ni mjinga uliyevuka hata mipaka ya ujinga wenyewe!!
 
View attachment 1488306

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Tanzania imejipanga na iko tayari kupokea watalii kutoka katika mataifa mbalimbali ikiwemo nchi ya Sweden na Israel ambazo raia wake wamekua wakitembelea vivutio mbalimbali vya utalii vya Tanzania. Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Ulf Kallstig na Balozi wa Israel kwa Tanzania, Oded Joseph ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake na mabalozi wa nchi mbalimbali ambazo ni masoko makuu ya utalii kwa Tanzania.

Dkt. Kigwangalla amewaeleza mabalozi hao kuwa mikutano anayoifanya na mabalozi wa nchi mbalimbali inalenga kulinda uhifadhi na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu hatua zilizochukuliwa na Tanzania kufungua Sekta ya Utalii wakati huu wa janga la Corona na kuwaomba mabalozi hao wawahamasishe na kuwashawishi raia wa nchi zao na makampuni ya utalii yaendelee kufanya biashara ya utalii na Tanzania. Amewaeleza mabalozi hao kuwa Tanzania imekwisha fungua anga na kuruhusu ndege za abiria za kimataifa kutua hali iliyochangia kufunguka kwa Sekta ya Utalii Tanzania kutokana na utayari, mazingira salama na maandalizi mazuri ya kupokea na kuhudumia watalii watakaowasili nchini wakati huu wa janga la Corona.

Dkt. Kigwangalla amewaeleza mabalozi hao kuwa Tanzania imezindundua mwongozo wa Taifa wa uendeshaji wa shughuli za Utalii unaosimamia usalama na afya za wadau wote wanaojihusisha na sekta ya utalii wakati huu wa janga la Corona.

Aidha, amewahakikishia mabalozi hao kuwa mifumo ya huduma za afya nchini imeimarika na iko tayari kuhudumia watalii watakaokuwa wakiwasili kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii akibainisha kwamba Tanzania ina hospitali za kisasa, maabara za upimaji zenye vifaa vyote na huduma za dharula kwa watalii watakaoshukiwa au kuonesha dalili za ugonjwa wa Corona. Kwa upande wao mabalozi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa hatua na juhudi anazozifanya kuendeleza uhifadhi nchini na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi. Katika juhudi zake za kuhamasisha na kufungua sekta ya utalii Waziri Kigwangalla ameshakutana na kuzungumza na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Ujerumani, Israel, Sweden, Netherland na Finland.
Anatafuta watu wa kupiga nao picha.

Watalii, kama walivyo wawekezaji, hawahitaji kuambiwa kwa maneno na Serikali kuwa mahali fulani ni salama bali wao wenyewe ndio wanaofahamu wapi kwa kwenda kutokana na ranking inayofanywa na mashirika ya kimataifa, na pia yale mnayoyatenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom