Kigwangalla asusa Kujadili Bajeti Ngazi ya Kamati kwa Kucheleweshewa Vitabu!

Mnafiki ni wa hovyo kuliko mchawi, na hii habari ooooh tujadili hoja na si watu, hoja inatokana na watu, na hapa hii hoja lazima Kingwangala tumkomalie ni mnafiki wa mkubwa. CCM ni chama chake na serikali ya chama chake ndiyo inayochelewesha, la msingi asubiri hukohuko kwenye vikao vya chama akaanike huu uozo wa serikali ya CCM, vinginevyo atawezaje kukata tawi la mti aliokalia?
Noboka Mkuu, hapa naomba unitoe ushamba wa siasa. Unataka kusema madudu ya chama yasitolewe nje, yabaki ndani ya chama? Unataka kusema madudu ya chama yafichuliwe na wapinzani tu? Ni nani anayejua zaidi yaliyomo ndani ya chama kama wale waliomo ndani ya chama ? Kufanya unavyoshauri, si ndio yale yale ya kulindana?
 
Back
Top Bottom