Kigwangalla asusa Kujadili Bajeti Ngazi ya Kamati kwa Kucheleweshewa Vitabu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigwangalla asusa Kujadili Bajeti Ngazi ya Kamati kwa Kucheleweshewa Vitabu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Le Grand Alexei, Jun 6, 2012.

 1. L

  Le Grand Alexei Senior Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kucheleweshwa vitabu vya bajeti: Kigwangalla Agomea Kujadili Bajeti Kwny Kamati! : Dr. Hamisi Kigwangalla's Round Table Kucheleweshwa vitabu vya bajeti: Kigwangalla Agomea Kujadili Bajeti Ngazi ya Kamati! : Dr. Hamisi Kigwangalla's Round Table # 5 mins ago

  Kumekuwa na mwenendo mbovu wa kuchelewesha nyaraka muhimu za bajeti ya serikali kwenye kamati kuanzia mwaka wa fedha unaoisha. Mwaka jana vitabu vya bajeti viligawiwa kwa wabunge wiki mbili kabla ya Bunge kuanza, kwa maana nyingine katika kipindi cha kamati kujadili na kuandaa mapendekezo kwa Bunge, kwa maana hiyo wabunge walipewa vitabu leo na kesho wakatakiwa kuanza kujadili na kutoa mapendekezo yao. Mwaka jana baadhi ya kamati ziligoma na hivyo kusababisha Spika kuitaka serikali isirudie kuchelewesha tena namna hiyo. Mwaka huu, hali ni mbaya zaidi; kamati zimepewa vitabu mwisho wa wiki ya kwanza (kati ya mbili) ya kamati. Hali hii ni kinyume na utaratibu wa kikanuni wa Bunge ambapo ingepaswa wabunge wapewe vitabu vya bajeti wiki tatu (siku 21) kabla ya tarehe ya kuanza Bunge Dodoma. Kwa maana hiyo wabunge wangekuwa wamepewa vitabu si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kamati (Ukizingatia kamati hukutana wiki 2 kabla ya Bunge kuanza). Hii ingewawezesha kusoma kwa umakini na kuandaa mapendekezo ya mabadiliko ama ushauri kwenye bajeti hiyo kwa ufanisi unaopaswa.

  Kwa kucheleweshewa vitabu kiasi hiki na kwa kuzingatia ukubwa na wingi wa mavitabu haya ya bajeti ni dhahiri hakuna Mbunge mwenye spidi na uwezo wa kuisoma, kuimaliza na kuichambua bajeti hii kwa ufanisi na tija inayostahiki. Kwa maana hiyo wabunge, ambao ni jicho la wananchi kwenye bajeti na utendaji kazi wa serikali, wamenyimwa fursa ya kufanya kazi yao ipasavyo na hivyo wanalipua lipua ili mradi liende tu! Uchunguzi wangu umegundua kuwa haya yamekuwa ni mazoea. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani mhimili wa Bunge ulivyokandamizwa na mhimili wa serikali (executive) na inaaakisi maovu na uvundo uliokuwepo kwenye serikali kwa muda mrefu bila kurekebishwa ipasavyo; kumbe ni kwa sababu mhimili Bunge ulikuwa usingizini kwa muda mrefu. Kama hii ni kwa maksudi ili kupunguza kelele na kupitisha bajeti kwa urahisi ama ni bahati mbaya nimeshindwa kuelewa, japokuwa kwa kiasi kikubwa ni harufu ya hila na inda inayotawala hali hii.

  Mimi nimeshindwa kuelewa wenzangu wanawezaje kujadili bajeti hizi bila kusoma!

  Ili kuweka wazi suala hili, na ili kuishinikiza serikali na viongozi wa Bunge kuona umuhimu wa kuwahisha vitabu ili kutoa fursa kwa wawakilishi wa wananchi kujadili bajeti kwa ufanisi na tija inayostahili, nimeamua kugoma kujadili bajeti katika ngazi ya kamati na badala yake nitajadili katika ngazi ya Bunge zima nitakapokuwa nimesoma na kuridhika kwamba ninapitisha kitu ninachokielewa. Nawashauri wabunge wenzangu waniunge mkono ili muda wa kujadili bajeti hizi katika ngazi ya kamati usogezwe mbele kwa wiki walau moja ili kutoa fursa ya kufanya kazi ya uhakika bila kulipua.
  Naelewa kuna sababu nyingi zinatolewa, kuwa eti re-shuffle ya mawaziri imesababisha kuchelewa, sawa, lakini hatuwezi ku-compromise ubora wa kazi nyeti kama kupitisha bajeti bila kutoa fursa ya kutosha kwa wabunge kujadili, kuchambua na kushauri ipasavyo.

  Tamko hili limetolewa na Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB), Nzega.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Chama chako kinasemaje? maana hukusain hoja ya kumuondoka PM, kwa madai ya chama kwanza, Je kwa hili chama hakina haja ya kuwahisha vitabu (ma kabuasha) aacha unafiki
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kuna wakati alikandya chadema kususa, sasa ni nini hiki?
   
 4. Y

  Yetuwote Senior Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amemaliza maandamano aliyoahidi? sijui ni leo?
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Kakosa uwaziri anajamba tu!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  [h=2]Kigwangalla tokea akose uwaziri kachanganyikiwa anajifanya anasoma PHD wakati anatumia majina ya watu[/h]
   
 7. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Alisemaga CDM ndio wasusaji na kuwasema vibaya sasa na yeye amekuwa CDM?
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kuukosa uwaziri bado kunamsumbua akilini
   
 9. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  sijawahi kuona watu wa maana kama akina Mwanakijiji wakitukana, nadhani by great thinkers, huyu ndiyo mmoja wao; lakini wewe Mangungo 'smalltime thinker' and maybe you are the opposite of smart...
   
 10. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  kwani nilitegemea kuupata ama ni nyie mliokuwa mnaweweseka kuhusu mimi kupewa uwaziri?
   
 11. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  sijawahi kusema hvyo, wewe ni mwongo ukizeeka utakuwa ...............
   
 12. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  watu wengine mna wivu sana. kuhusisha kusoma kwangu Ph.D na haya masiasa yenu ya kitoto ni fallacy. sasa inahusika vipi hapa? acha wivu bro. Kama unaweza kusoma Ph.D na wewe nenda kasome tu its a good thing, ofcoz kama una uwezo! Maana ile ni uanazuoni na siyo blah blah kama hizi siasa unazofanya hapa, maana hata wewe unafanya na unajiona una hoja kweli, pengine ukijifananisha na mimi unajiona uko juu sana na mimi ni mchovu sana...kumbe ukute wewe hata kugombea tu huo ubunge hujawahi kujaribu, ukute hata kuchukua risk ya kuacha kazi tu na kuanzisha biashara yako hujawahi kufanya, hata ku-indulge in a challenge ya ku-pursue Ph.D hujawahi....
   
 13. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Bora mimi, hivi wewe ungeishia nini?...
   
 14. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kigwangala, acha kujibishana na watu ambao badala ya kujadili mantiki ya hoja yako ya kususia hiyo bajeti kwa sababu ulizozitoa, wao wanaanza kutukana tu. Wewe ni kiongozi wa jamii kwa ngazi ya kitaifa, jaribu kuepuka mipasho isiyo na tija kwako. Jikite zaidi kwenye kutetea hoja yako ya ususiaji. Ikiwezeka usaidie kuwaelewesha ugumu wa kujadili bajeti bila kusoma.
   
 15. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  This is a TRUTH and 100% a FACT to most JF members who blow the trumpet of critique.

  It is simple to condemn, critize, etc and most fool do
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,445
  Likes Received: 19,812
  Trophy Points: 280
  Kigwa achana na kujibu matusi ya watu wapotezee ...
   
 17. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  unajua kuna watu wa hovyo sana humu JF na wamezoea kuona wakitukana viongozi na viongozi wakiwaacha, sasa mimi huwa siwaachi kwa kuwa nimo humu na ninajibu hoja kwa hoja, tusi kwa tusi (japokuwa situkani moja kwa moja ) kama wao. Hakuna anayejibu hoja ama hata kuchangia. Jambo nililopost kwenye blog yangu ni la msingi sana kwa mustakabali wa Taifa lkn leo hapa watu wanaleta hoja za kitoto (kisa eti kiongozi mzuri na shujaa ni yule anayeleta vurugu, anayepinga serikali muda wote nk). Mimi imejifunza uongozi kabla hata sijaenda shule na ninajua kufanya mambo yatakayowafurahisha na yatakayowachukiza ninaowaongoza lakini siku zote kwa kuwa nina ethics za uongozi siwezi kufanya maamuzi ya hovyo kwa kuwa nataka kusifiwa, nitafanya yale ya ukweli - yakiwafurahisha sawa, yakiwachukiza sawa, na huo ndio uongozi shupavu na unaofaa---kuwa na ujasiri wa kusema ukweli muda wote
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,445
  Likes Received: 19,812
  Trophy Points: 280
  Sio kila kitu tubishe ..kwa siku moja ama mbili mtu atasomaje na kuelewa kilichomo? Na inawezekana ndio maana kuna madudu mengi yanapitishwa san=babu ya ujanja ujanja kwenye sehemu nyeti na za muhimu ..hapa naona kigwa kakataa kuwapa ushirikiano tunamdhihaki ila kafanya jambo la msingi
   
 19. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  A single qn to HK and other social media Policians; why are you increasingly mendering JF? If you managed to come and respond to both, senseble and stupid critiques then why failed to personally bring this realese as you did in other networks?
   
 20. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  sure. hapa wengi hawafanyi 'critique' bali 'criticism'; maana critique ni ya kuanazuoni zaidi na ni nzuri maana mnachambua kwa kina pros and cons na siyo kukosoa one sided tu
   
Loading...