Kigwangalla ashambuliwa Twitter kwa kuwadharau wenye Digrii na wapo mtaani

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,841
Screenshot from 2017-01-30 14-39-32.png
Hamis Kigwagalla kakiona cha moto baada ya ku tweet inawezekana vipi mtu ana digrii na hawezi kujiajiri.

Watu wamecharuka na kuona ni aina ya dharau baada ya yeye kula kilaini huko serikalini na kusahau msoto watu wanaopata mtaani na bahasha zao za kaki.

-------------------------------------------
Tuna uhaba wa madaktari lakin mtu kaacha udaktari kaenda kwenye ubunge na sio kwenye ujasiliamali, ulisikia wapi Tanzania tuna uhaba wa wabunge?
 
Yeye ana digrii zaidi ya moja lakini hakuwahi kujiajiri,na bado kaajiriwa mpaka leo.

Atuambie,hao wanaofanikiwa kujiajiri wanaanzaje au nchi zao zinawasapoti vipi?

Tunamuona Trump anavyotaka kurudisha miradi na viwanda vikubwa marekani ili watu waajiriwe na wajiajiri.

Wakati trump akitaka fedha ya marekani ichochee uchumi na ajira,sisi za kwetu tumezificha benki kuu,tumeziondoa kwenye mabenki,sasa hawa vijana watajiajiri vipi wakati mikopo ya benki sasa ni migumu?
 
Kigwangwala hakuandika barua ya kuomba kazi.kateuliwa na anaweza kutenguliwa siku yoyote.Wabongo hampendi kuambiwa ukweli.Ni kweli huwezi kuwa na degree ukalala nyumbani kusubiri ajira ya serikali
Aligombea ubunge kwa appointment letter ama??? Kumfanyia visa bashe asigombee 2010 ilikuwa ndo mipango ya kujiajiri ama??
Kujiajiri kupo sema mazingira gani rafiki yamewekwa na serikali na taifa kwa ujumla kuna incentives for local investors, kuna mikopo nafuu, kuna government subsidies, trade protectionism from imported products??

Mfano nimejiajiri kutengeneza movie at the sane time mnaruhusu mamovie ya kinigeria na kikorea kujazana hapa Tanzania hapo ntapata faida kweli?? Misamaha ya kodi kwa wazawa mnatoa kma mnavyotoa kwa wale wachimba madini wazungu??? Sio mnakuja na lugha nyepesi tu wakati mko kwenye AC ya ofisi za ghorofani
 
Back
Top Bottom