Kigwangalla apinga Spika kuleta madaktari wa India Apollo, apingwa na wenzake!

Hata lusinde hajakosea jamani, michango inayotolewa mjengoni saa zingine unawashangaa waliomchagua, hata pumba zinatumika kuchoma nyama na kuchemsha maji, hizo zao hata sijui huwa ni nini, wapimwe kwa njia yyt ile ijulikane matatizo yao ni nini
 
Nadhani ingekuwa vyema kama wangeahirisha kikao cha sasa cha bunge ili wabunge wote wa ccm waende huko Apollo wakaangaliwe afya zao.. Itakuwa rahici kutibiwa maana vifaa vya muhimu ci vipo kule..
Halafu nakumbuka kuna wakati walipimwa kipimo cha HIV.. Nashangaa hata kutoa majibu na kutuambia kama wao ni Negative wameshindwa..! Hawajui wao ndio kioo cha jamii na raia wa daraja la kwanza nchi hii..
 
Huyu spika vipi? Ukisika ulevi wa madaraka ndio huu kama alivyosema Mwl.Nyerere.
 
Mama Makinda, Kigwangallah saa ngapi atapima waginjwa saa ngapi atapiga porojo za siasa? ni vyema ulivyofanya....[/QUOTE]

Kuna wakati najiuliza hivi wewe ni mtu kweli au Robot?sijapata jibu labda wadau wanisaidie!
 
Kuna wakati najiuliza hivi wewe ni mtu kweli au Robot?sijapata jibu labda wadau wanisaidie!.....[/QUOTE]

Utapata wapi jibu na wewe umejazwa Ubaguzi wa Ujinga?
 
Siamini kama hii statement imetolewa na mtu kama makinda. Kweli ukistaajabu ya musa..............


Madaktari wamegoma kwa sababu wamechoka kugeuzwa mashuhuda (eye witnesses) wa watanzania wanao kufa kwa kukosa dawa na vifaa tiba. Wakati wa mgomo Spika alikataa bunge kujadili mgomo wa madaktari si chini ya mara sita. Bunge limeisha, kapanda ndege kwenda India kucheki afya yake. Sasa ameona wanaofaa kupata huduma nzuri ni wabunge. Watanzania walalao wao ni kulipa kodi na kuzikana! Unforgivable!
 
Anne ana 10% yake ujio wa hao magabachori mnataarifa anastaafu bi.kiroboto 2015 anazichanga ili apumnzike vizuri
 
Namuunga mkono kwa 100% colleague wangu Dr Kigwangalla...hii ni kudhalilisha taaluma, kujiona wao bora na wana thamani zaidi, na matumizi mabovu ya kodi zetu. Sasa mpaka screening ya NCDs uchukue wataalamu toka Apollo!? Maspecialist vijana wenye skills wanagraduate kila mwaka toka vyuo vikuu vyetu wanashindwa kufanya screening ya NCDs! Dharau...

Ukubwa wa Apollo(India) is almost ukubwa wa Regency Hospital hapa kwetu..lakini wana vifaa(which is what Tanzanian doctors miss)..It's insane, unahitimisha kielimu watanzania kibao halafu wanachukuliwa na nchi za jirani!

Then unaleta madaktari toka India..what abt media of communication?..Halafu vifaa?..what does our leaders have in mind lakini?
 
wabunge na vibopa wa tanzania waelezwe kuwa madaktari wa hapa nchini ndio watakaowatibu siku zote!
Huwezi kwenda india bila kupitia mikononi mwa madaktari wa kitanzania,muulizeni zitto ni nani aliyegundua tatizo lake kwa mara ya kwanza kama sio dr juma .
 
Madaktari tunao ila hawana vitendea kazi! CT-scan ya muhimbili imekufa,ubingwa bila vitendea kazi is nothing.

fuatilia uone gharama watakazotaja za kuwaleta hao wahindi uone kama hatununui ct, mri na kujenga clinic yenye vifaa vya kutosha kwa ajili ya check up! Mpango wa mloganzila wa muhas una plan ya kuwa na hivyo vifaa vyote na hospitali maalumu kwa ajili ya viongozi. Wanakwamisha mpango huo kwani watakosa per diem za kwenda na kurudi india na makahaba wao.
 
Leo kwenye kikao cha 'briefing' cha wabunge, mbunge wa nzega Mh Dkt. Hamis Kigwangalla amejikuta ktk wakati mgumu alipoamua kuweka wazi msimamo wake kuwa hakubaliani na mpango wa spika wa bunge Mh Anne Makinda kuwaalika madaktari bingwa kutoka hospitali za Apollo kule India kuja kuwacheki afya wabunge.

Kigwangalla alisema: 'Serikali ya Tanzania chini ya Rais Kikwete imefanya jitihada kubwa sana kusomesha wataalam mabingwa hususani kwenye fani za moyo, viungo, meno, mafigo na hawajashindwa kubaini na kutibu magonjwa ya wabunge wa Tanzania mpaka tuite wahindi kuja kubaini lifestyle problems za wabunge wetu, itakuwa ni kuwadharau wataalam wetu, kutumia vibaya pesa za walipa kodi na zaidi ni kujiona sisi ni muhimu na special zaidi kuliko waliotuchagua...mimi napinga mpango huu na ninakushauri Mh Spika usituletee aibu ya kuwa wasaliti kwa wananchi ambao tunapaswa kuwatetea wapate huduma bora za afya...'

Wabunge wengi walionekana wakiguna kuonesha kuwa wanampinga.

Mh Lusinde Livingstone alimpinga akisema 'tusione aibu kutafuta tiba za afya zetu...pengine wengine wanatoa michango ya hovyo hapa kwa sababu wana homa vichwani mwao'

Mh George Mkuchika naye akasema: 'kwa mara ya kwanza frequency zangu zimeoana na za Kigwangalla...hebu limalizeni hili dada yangu Anne, litoe kwenye mpango wako, litatuaibisha...'

Ahsanteni,
Zul.
Mh. Lusinde ni lazima atakuwa na kipaji cha kutukana.
 
Tunahitaji vijana kama hawa. Tatizo wakubwa zao hawatak challenge. Big up Dr Kigwangala.
 
Hii hoja ya kuwaleta magabachori kuwatibu wabunge itawaunguza bora wasikilize ushauri wa Dr. HKigwangalla kwa usalama wao.
 
Last edited by a moderator:
Watanzani hawataki watu wanaowatetea ila wanapenda hawa wanaowaangamiza.Angali uchaguzi wa madiwani wa juzi.Ni wazi sisi watanzania wenyewwe ndio tunawapa kiburi ccm kwa kuwafanya kama chama kisicho na mbadala hapa nchini.

Simple logic ni kwamba, kama unaajiri mtu bila kuonyesha kuwa unaweza kumfukuza kazi wakati wowotwe, kweli unatarajia atakuheshimu?CCM wana hofu gani wakati wana uhakika wa kuendelea kubaki madarakani kwasababu waajiri wao(sisi wapiga kura) tumeridhika nao kupindukia!

Mimi nasema wacha wafanya wanavyotaka kwasababu watanzania sisi ni watu wa ajabu sana.

Huwa najiuliza, hivi kama baba wa taifa,mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, ccm si mama yangu, kwa maana ya kwamba, siku wakifanya kinyume na misingi ya kuanzisha chama hicho, atarudisha kadi ya ccm, sasa sisi watanzania wengine tumeridhika nini na hawa watu!

Kuna wakati huwa najuta kuwa mtanzania, hasa yanapokuja maswla yanayohusu siasa na wanasiasa wa Tanzania na wapiga kura wao.
 
wanaleta bungeni kufanya danganya toto na wakati washajua kbs conclusion itakuwaje.
 
Mh George Mkuchika naye akasema: 'kwa mara ya kwanza frequency zangu zimeoana na za Kigwangalla...hebu limalizeni hili dada yangu Anne, litoe kwenye mpango wako, litatuaibisha...'

Hv kuna MP yeyote anaruhusiwa kumuita Spika "SISTER" mbele ya waheshimiwa wengine!!!!!!!!!!!!!!
Kuna ??? nyng sana hapa.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom