Kigwangalla apinga Spika kuleta madaktari wa India Apollo, apingwa na wenzake!

Zulqarnayn

Senior Member
Oct 17, 2011
107
50
Leo kwenye kikao cha 'briefing' cha wabunge, mbunge wa nzega Mh Dkt. Hamis Kigwangalla amejikuta ktk wakati mgumu alipoamua kuweka wazi msimamo wake kuwa hakubaliani na mpango wa spika wa bunge Mh Anne Makinda kuwaalika madaktari bingwa kutoka hospitali za Apollo kule India kuja kuwacheki afya wabunge.

Kigwangalla alisema: 'Serikali ya Tanzania chini ya Rais Kikwete imefanya jitihada kubwa sana kusomesha wataalam mabingwa hususani kwenye fani za moyo, viungo, meno, mafigo na hawajashindwa kubaini na kutibu magonjwa ya wabunge wa Tanzania mpaka tuite wahindi kuja kubaini lifestyle problems za wabunge wetu, itakuwa ni kuwadharau wataalam wetu, kutumia vibaya pesa za walipa kodi na zaidi ni kujiona sisi ni muhimu na special zaidi kuliko waliotuchagua...mimi napinga mpango huu na ninakushauri Mh Spika usituletee aibu ya kuwa wasaliti kwa wananchi ambao tunapaswa kuwatetea wapate huduma bora za afya...'

Wabunge wengi walionekana wakiguna kuonesha kuwa wanampinga.

Mh Lusinde Livingstone alimpinga akisema 'tusione aibu kutafuta tiba za afya zetu...pengine wengine wanatoa michango ya hovyo hapa kwa sababu wana homa vichwani mwao'

Mh George Mkuchika naye akasema: 'kwa mara ya kwanza frequency zangu zimeoana na za Kigwangalla...hebu limalizeni hili dada yangu Anne, litoe kwenye mpango wako, litatuaibisha...'

Ahsanteni,
Zul.
 
Madaktari tunao ila hawana vitendea kazi! CT-scan ya muhimbili imekufa,ubingwa bila vitendea kazi is nothing.

Namuunga mkono kwa 100% colleague wangu Dr Kigwangalla...hii ni kudhalilisha taaluma, kujiona wao bora na wana thamani zaidi, na matumizi mabovu ya kodi zetu. Sasa mpaka screening ya NCDs uchukue wataalamu toka Apollo!? Maspecialist vijana wenye skills wanagraduate kila mwaka toka vyuo vikuu vyetu wanashindwa kufanya screening ya NCDs! Dharau...
 
Hii nchi ina maajabu mengi sana.Pamoja na kujifanya wako daraja la juu lakini kwenye KIFO na wao huwa hakuna ujanja kama mwananchi wa kawaida(wanavyotuita)
 
yaani wahindi wanaletwa hapa kupima afya za wabunge...hii serikali kweli ina hela...siku ziishe huyu makinda aondoke coz anazidi kujiaibisha na kuliaibisha bunge
 
Mh Lusinde Livingstone alimpinga akisema 'tusione aibu kutafuta tiba za afya zetu...pengine wengine wanatoa michango ya hovyo hapa kwa sababu wana homa vichwani mwao'

Kweli Lusinde ana mtindio wa ubongo! apelekwe mirembe ASAP.
 
Jamani hivi kweli tunaipeleka wapi hii nchi yetu?nadhani kuna viongozi hawana uchungu kabisa na rasilimali za nchi hii,kiufupi hakuna haja ya kuleta wataalam Madaktar from India kwani hapa Tanzania hayo yanawezekana.Lusinde ana kichaaa nadhani yeye na bi Kiroboto.Tuipende nchi yetu na tujiepushe na matumiz mabaya ya pesa JK amka mbona unakua kama umetoka Msoga Leooo.
 
Kigwangwala anapoint kubwa sana hapa,Hii ni aibu,wanaweza kumtumia hata Kigwangwala mwenyewe maana ni Bingwa huyo!!!
 
Hahaha Lusinde ni janga moja kubwa sana, huyu jamaa sijui huwa anafikiria au anawaza!!
 
Mh Lusinde Livingstone alimpinga akisema 'tusione aibu kutafuta tiba za afya zetu...pengine wengine wanatoa michango ya hovyo hapa kwa sababu wana homa vichwani mwao'

Kweli Lusinde ana mtindio wa ubongo! apelekwe mirembe ASAP.
Unakosea kumwita Mh! hastahili kuitwa neno hilo zoba kama huyo. Ubongo umeachana na fahamu huyo!

 
Dr. Kigwangallah is damn right. Hongera sana Kigwangallah kwa kusimamia ukweli. Halafu hivi huyo Lusinde aliu pataje Ubunge in the first place?!

Mimi nafikiri kuna nuts fulani kichwani mwake ziko lose aende akamuone Professor Kaaya pale Muhimbili.

Pamoja na matatizo yoote tuliyonayo Watanzania yaani Spika Makinda ameona huo mkakati wa kuwaleta Wahindi kupima Afya za wabunge ndiyo kipaumbele? Haya ndiyo matatizo ya kuahagua SPIKA kwa gender badala ya kuangalia uwezo wa mtu. Kweli CCM ni janga la kitaifa
 
Back
Top Bottom