Kigwangalla ampiga vijembe Bashe baada ya kumshinda uchaguzi wilayani Nzega | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigwangalla ampiga vijembe Bashe baada ya kumshinda uchaguzi wilayani Nzega

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chikakatata, Oct 2, 2012.

 1. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=5]Hivi ndiyo alivyoandika kwenye ukurasa wake wa FaceBook:--

  "Hamisi Kigwangalla
  [/h]4 hours ago
  "Uchaguzi Mkuu wa CCM Wilaya ya Nzega umemalizika salama na tumepata viongozi mahiri. Ni imani yangu tukiwapa ushirikiano wa kutosha CCM sasa itakuwa moja, imara na yenye kusonga mbele. Hongereni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Nzega kwa kung'oa kwa kiasi kikubwa vigogo na waasisi wa siasa za ufuasi na wenye kufanya siasa za kumridhisha mtu mmoja tu, pia kwa kuwakwamisha wengi wa wafuasi wa siasa hizo na kuingiza majembe ya ukweli! Mmedhihirisha pesa peke yake si kigezo cha kushinda uchaguzi, mmefanya kweli. Nawashukuruni nyote kwa kufuata na kutumia ushauri wangu kwamba tujenge CCM moja imara, kusiwe na watu wa Kigwangalla na wala wa Selelii, kuwe na wanaCCM wamoja...mlinipa faraja ya ushindi na pale mliponibeba juu juu niliogopa kwamba msije mkawa mmedhamiria kwenda kunitupa, ila nakushukuruni sana hamkufanya hivyo badala yake mlishukuru kwa ushauri wangu..."

  "Mara baada ya fununu za matokeo ya uchaguzi kuwa wazi kuna watu wawili maarufu walizimia, na walipozinduka waliangua vilio na hawajaonekana Nzega tena...tunawapa pole na kuwatakia quick recovery huko waliko! Huo ndiyo ushindani...na sisi tunawaambia kuwa wasihofu kitu watatendewa haki siku zote katika chama hiki na katika uongozi huu. Malengo yetu ilikuwa ni kuondoa watu wa hovyo, wachumia tumbo na wanaofanya kazi kwa maelekezo ya mtu mmoja tu na sasa kuweka watu makini na mahiri watakaokisimamisha chama, hata kama itamaanisha kuniadhibu mimi pale itakapobidi...Chama Kwanza, Mtu baadaye! Hakuna mtu maarufu na wa maana ndani ya CCM kuliko CCM yenyewe. Nimesikia wanataka kuikimbia nchi, tunawasihi wasifanye hivyo, waendelee tu kuwa waadilifu na waaminifu kwa chama na kwa nchi na ipo siku mambo yao yatawanyookea tu!"   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  UNAJUAJE Mwananchi ??? Haukufuatilia ??? WOTE WALIENGULIWA NA CC - DODOMA
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kumbe huyu mshikaki huwa ana busara. za kisiasa. God bless u
   
 4. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anajitahidi kiasi chake kuwa mwanadiplomasia naona pia nimesikia juzi akikanusha kuhusika na kumtishia bashe bastola na ameahidi kuwaeleza wananzega kuhusu hilo tukio
   
 5. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hilo nalifahamu vizuri sana, baada ya wao kuenguliwa na nec wote walipanga safu zao na inavyoonyesha hapa ni kwamba watu wa Kigwangalla ndiyo walioshinda nafasi zote nyeti na hapa anampiga vijembe mwenzake
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kigwangalla kaongea vizuri sijaona vijembe vyovyote.
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  Kwahiyo REKEBISHA kiswahili CHAKO; KUWA KIGANGWALLA alichaguliwa... Kumbuka Mwenyekiti J.K

  KIkwete alisema Wanotaka kuhama wahame alimaanisha KIGANGWALLA sababu ya kiduduku chake cha

  kutaka kufanya mkutano baaada ya siku 2 sababu jina lake liliondolewa... MWAMBIE UBUNGE ana Mwaka

  MMOJA na NUSU baada ya hapo AJARIBU UDAKTARI kama kweli anauweza... KIKWETE HAMTAKI TENA...

  ni KIGEUGEU...
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  huu ujinga na mipasho ya huyu mwanasiasa anayejiita msomi na kuwa na tabia kama shilole zinanikera sana
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kwani kikwete baada ya 2015 bado atakua na nguvu?
   
 10. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na ile kusema alizimia baada ya mgombea wake kushindwa na kudai anataka kwenda nje ya nchi ni nini?
   
 11. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani atasoma salamu hizo yeye mwenyewe naye si mjumbe hapa ?
   
 12. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  amezungumza vizuri sana, anazungumzia wafuasi wa lowasa, kuwa kumbe hata pesa ya lowasa kuna mahali haifanyi kazi kama nzega
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Halafu kuna watu wanasema tunataka viongozi vijana... kadizooo!!!
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  OH YEAH; atakuwa bado MWENYEKITI WA CHAMA KITUKUFU CHA CCM... MPAKA 2017

  umesahau na ni mama Salma ndie aliyempa hicho cheo cha UBUNGE.... alishika MKIA unakumbuka ?
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  YEYE ni MJUMBE wapi ? Sasa HIVI AMECHANGANYIKIWA... Anahitaji zaidi ya pyschogist

  kwasababu amevunda
  Alitaka Kumwingiza Mkewe CCM-NEC na Mkewe ana kazi NZURI

  ya UDAKTARI AMREF... Sasa Unaona Walikuwa Wanataka wale PESA ZA BURE

  KIVULINI...

   
 16. C

  Concrete JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mbona kuna gazeti leo(sikumbuki jina) limereport kwenye heading yake kuwa Bashe kashinda nafasi fulani ndani ya chama, sijajua ni nafasi gani(labda mkutano mkuu)
   
 17. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  doh :doh::doh::doh::doh::doh: nilisahau kwamba sultani ndiye anayeamua nani awe wapi
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Oh Yeah... Na Kijana amechezea neema... anakuwa MBWATUKAJI lakini inakuwa rahisi kusahau alikotoka...

  NDIO MATATIZO YETU... Sasa BAHATI na NEEMA ikifungika ni MILANGO YOTE; alikuwa anadonyoa

  WAPINZANI na
  kuikera CCM bila kupinga MAHESABU... Ndio Ubaya wa SIASA zetu - UKIDONDOKA

  CHALI ndio BASI tena... kuna stages NYINGI KURUDI kwenye SIASA... Unamkuta KIJANA anatembea

  Barabarani anaongea MWENYEWE haujuni ni kwa nini na ELIMU YAKE...
   
 19. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  unfortunately ulichosema ndio ukweli wenyewe......... dogo amenyea karibia kila kambi, haeleweki na siajabu hajielewi
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  Yeah, Hajielewi... Sasa Baada ya Jina kukatwa Anatangaza kwenye FB kuwa WAPINZANI WOOTE MACHO na

  MASIKIO Yalikuwa DODOMA na ni IMANI yake CCM itashinda kwa NGUVU 2015; Upinzani Hauna lolote...

  Halafu jana na leo anajenga MAKUNDI ndani ya CCM kuteuana ili watu Wenye UHUSIANO na MPINZANI

  wake
  Wasipate UJUMBE wa CCM-NEC; Haya anaweka MAKUNDI NDANI YA CCM... Badala ya kuwa kimya

  na Kuonyesha HESHIMA iliyomponza aondolewe ni Mwaka Mmoja na Nusu Umebaki Uchaguzi wa Ndani ya

  CCM
  Kuchagua Wabunge Unaanza... Unadhani kwa sasa hivi JINA lake halipo; Sidhani MWENYEKITI

  atamteua... NDIO HAO VIJANA KIKWETE ALIOTAKA WAONGOZE CHAMA na SERIKALI ??? NAONA

  KASHTUKA...
   
Loading...