Kigwangalla amechanganyikiwa, hakujiandaa na anguko lake la kisiasa

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,183
2,000
Kigwangwala ni moja wanasiasa vijana machachali wa zama hizi ambaye safari yake ya kisiasa uhenda ndio imemalizika.

Naona anatumia nguvu kubwa sana kujaribu kuweka mambo sawa kulinda jina lake, anashinda Twitter akijisafisha. Mara utamuona Instagram akijisafisha. Ametembea baadhi ya media kujisafisha. Juzi kaita wazee wa jimboni kwake kujisafisha. Well and good ila the damage is done.

Kuna matukio matatu ambayo yamechangia kumporomosha kisiasa.

Jambo la kwanza, ni kuingilia masuala ya uhendeshaji wa Simba. Hapa aligusa hisia za wanasimba walio wengi wanamuona kama anataka kuwarudisha nyuma so popote watapopata chance ya kumpiga watamtandika kweli kweli.

Pili, kutoka hadharani baada ya kifo cha Magufuli na kuanza kupromoti chanjo ya COVID 19. Hapa aligusa hisia za wafuasi na mashabiki kindakindaki wa Magufuli waliona kama ni msaliti. Wengi walikuwa wanamuuliza ulikuwa wapi kusema hapo nyuma? Lakini pia ili kundi la chanjo lina mizizi sio tu kwa waliompenda Magufuli bali mpaka kwa watu wa imani na mitazamo ya kiafrica hao wote aliwagusa pabaya. Wanasiasa wabobezi hutowasikia wakitoa maoni kuhusu chanjo.

Tatu na lililopigilia msumali wa ndoto za kisiasa za Hamis haswa kwenye kusaka influence kwa vijana ni ishu ya ripoti ya CAG ambayo iligusa moja kwa moja sio tu wizara yake bali ofisi yake kama waziri. Hapa HK walimmaliza.

Mchanganyiko wa haya matukio matatu umempotezea Kigwangwala weledi wa kisiasa.

Inawezekana Kigwangwala alikuwa sahihi kwenye kila jambo hapo ila shida yake kubwa jamaa anakosa namna nzuri ya kuwasilisha mambo yake.

Pia sio mtu mwenye subira, hawezi kusubiri wakati sahihi wa kuzungumza jambo na hii ndio weakness yake kubwa. Ni mtu mwepesi sana kuwa provoked.

Namalizia kwa kusema Kigwangwala amefata njia ya January Makamba. Vijana machachali wa kisiasa walioangukia pua sababu ya kutojua kucheza na wakati.

Ajali zao za kisiasa zinaweza zikawaacha walemavu milele.
 
mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,183
2,000
Nukta yako ya kwanza na ya pili naipinga kwasababu alikuwa sahihi kuelezea hisia zake ila hiyo ya tatu naweza kukubaliana na wewe.
Ndio maana nasema kuwa sahihi ni jambo moja ila kisiasa muda sahihi wa kuzungumza ni jambo muhimu sana.
 
Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,458
2,000
Nukta yako ya kwanza na ya pili naipinga kwasababu alikuwa sahihi kuelezea hisia zake ila hiyo ya tatu naweza kukubaliana na wewe.
Kikubwa alichomaanisha jamaa
Ni kuwa alitakiwa hatumie HEKIMA kubwa katika kufikisha hayo maswala
Sababu yalikuwa yanawagusa wananchi na yeye kama kiongozi Mwanasiasa ilipaswa atumie BUSARA katika uwasilishaji
Sababu ukishakuwa maarufu au kiongozi unatakiwa uchague sana maneno ya kuongea na wakati upi ni sahihi na yupi wa kumlenga
Sababu utakapoongea utasikika na wengi na hao wengi si wote wataelewa vile wewe ulivyokuwa unamaanisha au kukusudia
Wengne wataelewa namna BONGO yao itakavyochakata na wengne watakuelewa nini unamaanisha
Ndio maana hata Mama samia alivyoanza alikuwa moto kuzungumza yaliyo moyoni mwake mpk watu wakaanza kumuona kivingne
lkn wakawahi wakamkumbusha yeye sasa namba 1
Hvyo akapunguza akawa anatumia HEKIMA na BUSARA ya uongozi na akawa anajua wapi azungumze hili na wapi azungumze hivi ndivyo KIONGOZI uliyepewa DHAMANA unavyotakiwa

Na ndio Sifa kuu ya uongozi
HEKIMA BUSARA UOENDO kwa unaowaongoza UKARIMU katika uzungumzaji na hata kujizuia HISIA zako katika kuwasilisha mikakati yako ya kimaendeleo 7bu unaongoza jamii mchanganyiko ya makabira yote dini zote wanasimba wanayanga wanyonge matajiri mashetani wachawi nk

Ukiweza hayo unakuwa kiongozi bora wa mfano
 
Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,033
2,000
Ukizingua....Tunazinguana
tqx5ff.jpg
 
Genius!!
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,264
2,000
Hiyo hoja yako ya kuihusu simba, naona ni hoja dhaifu kabisa! Na kwa mtazamo wangu, haikustahili kabisa kuwekwa kuwa sababu namba moja!
 
zege la nyasi

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
587
1,000
Tatizo hajakubali kukosa vyote.....
Upo sahihi kuanzia 1,2 na 3.....
Inaonyesha n kiongozi asiye na msimamo binafsi....
 
Ridomil gold

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
613
500
Kigwangwala ni moja wanasiasa vijana machachali wa zama hizi ambaye safari yake ya kisiasa uhenda ndio imemalizika.

Naona anatumia nguvu kubwa sana kujaribu kuweka mambo sawa kulinda jina lake, anashinda Twitter akijisafisha. Mara utamuona Instagram akijisafisha. Ametembea baadhi ya media kujisafisha. Juzi kaita wazee wa jimboni kwake kujisafisha. Well and good ila the damage is done.

Kuna matukio matatu ambayo yamechangia kumporomosha kisiasa.

Jambo la kwanza, ni kuingilia masuala ya uhendeshaji wa Simba. Hapa aligusa hisia za wanasimba walio wengi wanamuona kama anataka kuwarudisha nyuma so popote watapopata chance ya kumpiga watamtandika kweli kweli.

Pili, kutoka hadharani baada ya kifo cha Magufuli na kuanza kupromoti chanjo ya COVID 19. Hapa aligusa hisia za wafuasi na mashabiki kindakindaki wa Magufuli waliona kama ni msaliti. Wengi walikuwa wanamuuliza ulikuwa wapi kusema hapo nyuma? Lakini pia ili kundi la chanjo lina mizizi sio tu kwa waliompenda Magufuli bali mpaka kwa watu wa imani na mitazamo ya kiafrica hao wote aliwagusa pabaya. Wanasiasa wabobezi hutowasikia wakitoa maoni kuhusu chanjo.

Tatu na lililopigilia msumali wa ndoto za kisiasa za Hamis haswa kwenye kusaka influence kwa vijana ni ishu ya ripoti ya CAG ambayo iligusa moja kwa moja sio tu wizara yake bali ofisi yake kama waziri. Hapa HK walimmaliza.

Mchanganyiko wa haya matukio matatu umempotezea Kigwangwala weledi wa kisiasa.

Inawezekana Kigwangwala alikuwa sahihi kwenye kila jambo hapo ila shida yake kubwa jamaa anakosa namna nzuri ya kuwasilisha mambo yake.

Pia sio mtu mwenye subira, hawezi kusubiri wakati sahihi wa kuzungumza jambo na hii ndio weakness yake kubwa. Ni mtu mwepesi sana kuwa provoked.

Namalizia kwa kusema Kigwangwala amefata njia ya January Makamba. Vijana machachali wa kisiasa walioangukia pua sababu ya kutojua kucheza na wakati.

Ajali zao za kisiasa zinaweza zikawaacha walemavu milele.
Bwana huyu sijui jimboni kwake wote anao waongoza hajui
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom