Kigwangalla aiagiza TAKUKURU imchunguze Nyalandu, amtuhumu kuipotezea Serikali mabilioni kupitia tozo za hoteli

Kigwangallah anaagiza TAKUKURU? wale alioagiza Rais wahojiwe kwa "kutuibia" madini issue yao imefikia wapi?. Watu waliothibitika kutuibia (Chenge et al) TAKUKURU na CCM yao imewafanya nini todate?
 
Kigwangwala ni mpuuzi......wananchi tunataka mawaziri mfanye kazi zionekane na maisha yetu yabadilike huu upumbavu wa kurushiana vijembe umetuchosha.
Kama Nyalandu ana makosa aliyoyafanya wakati akiwa waziri katika serikali ya awamu ya nne wote wawajibishwe....kuanzia JK,Pinda,Chenge,Magufuli,Muhongo,Makinda,Mwandosya,nk Kigwangwala acha porojo za kijinga chapa kazi.OVER
 
bila mihemko yoyote..hebu elezea hapa Lowasa amefanya kosa lipi?

na kwanini hadi leo hajapelekwa kwenye mahakama ya mafisadi?

Ujue msiwe mnaonge atuuuu kwa sababu Mungu amewapa akili za bure
Mkuu siyo akili ya bure tu bali na midomo ya bure ambayo haina ushirikiano na hiyo akili.
 
Zilipendwa hizo, yaani haiingii akilini mtu akihama chama ndomnaanza kusema alikuwa mchafu.

Fisiemu mmefilisika kwa hoja.
 
na wewe naweeee..badala ya kujiongeza akili zako ndio hapo umegota

mambo mengine ni common sense tu..Jiulize why Nyalandu?

Hakuna mtu anakataa hatua kuchukuliwa kwa walioingiza nchi hasara

Lakini zinapaswa zichukuliwe hatua na sio kuonea watu kwa sababu tu wameikataa CCM

Ila common sense inasema...mtu mwenye uhakika na usafi wake ndiye mwenye guts za kutoka CCM
Acha vyombo vya sheria vifanye kazi yeke.....kama hausiki ataachiwa huru.

Umesahau hotuba za Chadema kule bungeni hasa Nasari na Msigwa za kumtuhumu Nyalandu.?

Au Chadema mnasakama watu walio ccm tu wakihamia Chadema mnasema mnawatetea..

Huu ni mda muafaka Chadema kuunga mkono juhudi za TAKUKURU ili Tuhuma dhidi yake zidhibitishwe....

Chadema acheni ukigeugeu.....kwa ujinga huu ccm itatawala miaka mingi ijayo.!
 
Kama ana tuhuma apelekwe mahakamani.
IMG-20171110-WA0025.jpg
Atawasha Feni sasa Hivi....
 
Acha vyombo vya sheria vifanye kazi yeke.....kama hausiki ataachiwa huru.
kuna mtu yeyote ..so far..amezuia vyombo kufanya kazi yake? anyway..ngoja tuwaone nyie mnaodhani kama kuna hata hivyo vyombo hasa kuhusu masuala ya Rushwa...bro umelogwa na nani? hii yote ni kwa sababu ya slaa tu?



Huu ni mda muafaka Chadema kuunga mkono juhudi za TAKUKURU ili Tuhuma dhidi yake zidhibitishwe....

Chadema acheni ukigeugeu.....kwa ujinga huu ccm itatawala miaka mingi ijayo.!
TAKUKURU hii hii iliyoshindwa kumchukulia Hatua DC Mnyeti aliyekamatwa na Rushwa red handed..You must be joking bro...kabisa yanii
 
mimi sina mda wa kuelezea hayo yote mkuu nimekuekea link hapa unaweza kufatilia vizuri kwa utulivu kabisa bila mihemko.

hujajibu swali langu bro...mimi nimekuuliza why hadi leo serikali ya magufuli haijamfikisha mahakamani?

Unajua kesi za jinai nchi hii ni jukumu la nani>?
 
Dah hizi tuhuma zenyewe mbona nyepesi? Mimi nilidhani anatuhumiwa kusafirisha twiga kwa ndege au kutoa vitalu kwa rushwa. Kwa kuwa amezijibu na ni rahisi kwake kuthibitisha utetezi wake sasa tuhuma zimekuwa kushindwa kusign sheria? Kwani sheria si anasign raisi au mimi sielewi? Na pia hiyo ya kutumia helikopta ya muwekezaji, yaani hiyo ndiyo ya yeye kuikomalia? Kama kuna vithibitisho vya rushwa vinavyohusiana na utumiaji wa ndege hiyo, nadhani kuna vyombo husika vya kufanyia uchunguzi na Waziri wa Maliasili siyo wa kutoa hayo maagizo. Sanasana ni kutoa tu ushirikiano kwa vyombo hivyo kama atahitajika. Anyway, muda pia ni rasilimali na upo very limited, unapoutumia kufanya mambo ya ovyo na kulipiza visasi, utapata wapi muda wa kufikiria na kufanya mambo ya maendeleo?
 
mkuu wewe huelewi usemacho..Nani anatakiwa kumfikisha mtu mahakamani kwa makosa ya Jinai?

Kwa sheria za Tanzania.

Ivi bro una akili hata ya kuvukia barabara?
Yeyote mwenye ushahid anatakiwa apeleke sehem husika kwa ajili ya hatua zaid.chadema imezunguka miaka nane na ushahid wa ufisadi wa lowasa,je hawakujua kuwa kuna sehem husika inatakiwa wapeleke ushahid wao kuisaidia SERIKALI?Vipi ule ushahid chadema bado wanao ili hata Mimi mwananchi nije nichukue nipeleke sehem husika?
 
hahahahahahahahhaahhaahahahahhaha...CCM vichekesho kweli

eti tuhuma kwa nyalandu

na wala sio tuhuma kwa Maghembe..wala sio kwa Maige....wala sio kwa Kagasheki


Hhahahahaha

Kweli mnachekesha

Nyalandu amehudumu miaka 2 tu wizarani pale..na hajatoa kitalu chochote cha uwindaji...

Hakusaini ndio ,.....kwani mlitaka mje kumwingiza kingi kwamba na yeye ni sehemu ya uchafu

Ukiona mtu anaihama CCM ujue amejitafiti na ni msafi kweli kweli

Manake wanaoshindwa kutoka CCM ni majizi kweli kweli
Dah! Yaani hapo umeongea kama mkulu mwenyewe. Unakumbuka ile mijizi ya Acacia? Nao waliitwa wanaume kweli kweli...!
 
Kwa ufupi
Waziri huyo amemshukia Nyalandu akidai kuwa ameipotezea Serikali mabilioni

By Daniel Mjema, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala amemlipua waziri wa zamani wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018, Dk Kigwangalla ameiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.

Dk Kigwangala amesema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

Mbali na tuhuma hiyo, pia alimtuhumu kutumia helkopta ya mwekezaji mmoja raia wa kigeni, kipindi cha kampeni zake za kugombea urais 2015, wakati kampuni ya raia huyo ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.

Hata hivyo wakati Kigwangala akitoa tuhuma hizo tayari Nyalandu alishasema kuwa tuhuma ambazo zimeanza kuibuliwa mitandao dhidi yake si za kweli bali zinalenga tu kumchafua.

Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni alishangaa iweje ziibuliwe sasa zaidi ya miaka miwili tangu aachie uwaziri.

Naona kwa Kaghasheki kafungwa break
 
Back
Top Bottom