Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Naibu Waziri wa Afya, Daktari kijana na mwanaharakati wa muda mrefu katika kutetea haki za madaktari (ameshiriki mengi) ametoa kauli akitaka maelezo kuhusu kukosekana chanjo na amefikia hatua ya kuhoji hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliokwamisha ndani ya wizara na hata Hazina.
Bahati mbaya sana suala analozungumzia limeshafanyiwa kazi na mtendaji wa hazina amethibitisha kwamba muda mrefu walishatoa Shilingi Bilioni 1.6 kwenda Wizara ya afya kwa ajili ya chanjo.
Naibu Waziri alipaswa kujua kuwa fedha hizo zilishaingia wizarani kwake na zilishaanza kazi.
Lakini wakati wenzake wanashughulikia suala hilo, yeye aliulizwa Instagram akasema hajui na atafuatilia lakini badala ya kufuatilia katika ofisi yake, anatoa matamko tata mtandaoni.
Pengine anafanya hivyo baada ya kuona watu wanahoji mtandaoni, lakini angefanya hivyo kwa kuwa na taarifa za uhakika na za wakati na asingeanza kulaumu hazina na kuhoji hatua dhidi ya watumishi wa hazina ambao wana waziri wao.
Naona kama Kigwangala ameanza kujisahau na kujiona kama ni Waziri Mkuu ama Rais (aligombea kuteuliwa na CCM awe mgombea uraisi). Alifanya hivyo kuliagiza Jeshi la Polisi kukamata watu kwa sababu tu aliulizwa swali na mwandishi kwamba ameshindwa.
Kwa uwezo alionao, ni vyema Naibu Waziri akajikita katika kufanya kazi kwa umakini zaidi ikiwa ni pamoja na kusoma majalada ya masuala anayotaka kuyatolea matamko kuepuka kutoa taarifa ambazo zinakinzana.
Bado kama kijana anayo nafasi nzuri ya kujirekebisha na kuongeza umakini wa kushiriki vikao na kusoma majalada badala ya kufunika muda wa kazi aliotumia kufuatilia biashara zake za ununuzi wa pamba kwa kisingizio cha kwenda kufanya ukaguzi wa vituo vya afya.