Kigwangala usilete mgogoro Simba, lazima tuwaamini uongozi uliopo

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nimeona baadhi ya wachambuzi maandazi wamepata jambo la kuongelea wiki hii nzima baada ya Kigwangala kuhoji uteuzi wa CEO mpya wa Simba.

Kifupi tu namuomba aache kuleta uswahili na choko choko kwa club ya Simba kwani naamini ukitoa dili zilizomtoa kisiasa, hana uwezo wa kujua masuala ya uendeshaji timu, uongozi na usimamizi wa miradi mikubwa.

Kama tu ameshindwa tu kuimarisha chuo chake, mradi ambao ni uwekezaji wenye faida kubwa na wenye uwezo wa kuajiri watu wengi, atakuwa na mawazo gani ya kuishauri Simba kama sio tu kuanzisha choko choko?
 
Simba itapigwa vita na kila mtu na wakikubali na hizi propaganda hakika itasambaratika, huwezi judge uwezo wa mtu kufanya kazi kabla hujaona uwezo wake!
 
Nimeona baadhi ya wachambuzi maandazi wamepata jambo la kuongelea wiki hii nzima baada ya kigwangala kuhoji uteuzi wa CEO mpya wa Simba.

Kifupi tu namuomba aache kuleta uswahili na choko choko kwa club ya Simba.Kwani naamini ukitoa dili zilizomtoa kisiasa,hana uwezo wa kujua masuala ya uendeshaji timu, uongozi na usimamizi wa miradi mikubwa.

Kama tu ameshindwa tu kuimarisha chuo chake mradi ambao ni uwekezaji wenye faida kubwa na wenye uwezo wa kuajiri watu wengi, atakuwa na mawazo gani ya kuishauri Simba kama sio tu kuanzisha choko choko?
jamaa anamiliki chuo kipi
 
Simba haina uongozi baada ya "NKWABI" mwenyekiti aliyeteuliwa na wanachama kusukumwa nje alipohoji maslahi halali ya Simba! Sasa kuna njaa kali Kaduguda hasemi chochote zaidi ya "ndiyo" boss Mo!
Nyani ni Nyani tu.Haoni kundule. Utopolo kweli una moral athourity ya kuzungumzia Simba wakati mmepakatwa na mwarabu koko wa GSM na msomali pori.
Wanasajili wao tena kwenye sitting room zao huku mkiwa na klabu bila nembo wala ushuzi.
Unafikiri Shija alijiuzulu kwanini?
Sasa hivi GSM wamesema wamesajili ila nyie Utopolo mlipe mishahara. Wakijua hamna uwezo huo ili mzidi kuwaachia klabu.Hiyo ni blackmail.Mmekazia shingo Simba huku nyumba ya mabua inauungua.
 
IMG_6765.JPG

Dah....Mo amewadharu sana!🤣🤣
 
Simba itapigwa vita na kila mtu,na wakikubali na hizi propaganda hakika itasambaratika,huwez judge uwezo wa mtu kufanya kazi kabla hujaona uwezo wake!
Ila apart from propaganda kuna swali la msingi ameuliza, hii pisi ya Mudi ambaye ni mtumishi binafsi wa Mudi hamuoni ataleta conflicts of interest kuwa CEO wa kampuni ambayo Mudi ana hisa na ni muekezaji???
 
Simba sio METL muache ahoji kama hamtaki kuhojiwa anzisheni Club yenu binafsi ndio mfanye vile mnataka ila so long Mo sio majority share holder hawezi kufanya lolote analojisikia na watu wasihoji mtapoteza mashabiki sana
Sisi kama Stakeholders wa Simba wacha tuone hio transformation mnayoifanya, Huko mbele naona Lawama za kutosha
 
Mwenyekiti wasasa wa Simba Kaduguda, aliwahi kuzuia vifaa vya mazoezi vya klabu ya Simba ikiweno mipira, nyavu, koni n.k kwakua ali kua akidai fedha zake alizo wanunulia wachezaji chapati.
Aliamua kufanya hivyo baada ya wanachama kuamua kumtimua kwenye uongozi. Sasa mtu aliye dai pesa za chapati leo ndio mwenyekiti wa klabu. Unategemea Mudi afanye nini? Atakapo amua Mudi ujue alihitaji mjadala.
 
Simba haina uongozi baada ya "NKWABI" mwenyekiti aliyeteuliwa na wanachama kusukumwa nje alipohoji maslahi halali ya Simba! Sasa kuna njaa kali Kaduguda hasemi chochote zaidi ya "ndiyo" boss Mo!

Kwani hisa za mashabiki zimeshanunuliwa?
 
Jamaa aliomba mkopo wa pikipiki ikashindikana. Ikabidi atafute ujiko kwa njia nyingine. CEO ni mtendaji mkuu na alikuwa kwenye Bodi kwa miaka 3 tokea Simba ibadilishe mfumo.Ana uzoefu wa kutosha wa uongozi.
 
Kigwa anahoja ya msingi kabisa
Sema wabongo wengi hata hatuelewi

Hoja ya kingwa ya msingi but ajatoa mbadala,

Alitakiwa aseme wakurugenzi wote wajiuzulu na more atoke then timu itoe Namba za wanainchi kuchangia
 
Back
Top Bottom