Kigwangala: Uingizwaji wa mifugo na matrekta umesababisha uharibifu wa mazingira

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,506
WAZIRI%20wa%20Maliasili%20na%20Utalii%2C%20Dk.%20Khamis%20Kikwangala.jpg

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa juzi kwenye mitandao ya kijamii na ofisi hiyo ikisainiwa na Waziri huyo jana, ilieleza kuwa uingizwaji wa mifugo na matrekta umesababisha uharibifu wa mazingira.


“Ninatoa ilani ya siku saba kwa mifugo, matrekta na vyombo vingine kutoka nje ya Tanzania kuondolewa mara moja ndani ya Pori la Loliondo kuanzia siku ya leo (jana),” alisema.


Aidha, alisema baada ya muda huo mifugo na vyombo vingine vitakavyokamatwa ndani ya pori vitataifishwa.


Hifadhi ya Taifa Serengeti (Senapa), ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini kati ya hifadhi 16 inapakana na pori hilo, inakabiliwa na changamoto kubwa ya mifugo ya Watanzania na raia wa Kenya inayolishwa hifadhini.


Uchunguzi uliofanywa na Nipashe Septemba, mwaka huu, ulibainisha kuwa mifugo inazidi kuongezeka kuingia hifadhini licha ya kuwapo adhabu ambayo imezoeleka na kuwa rahisi kulipwa kiasi cha Senapa kuamua kutaifisha mifugo inayokamatwa.


Akizungumza na Nipashe, Septemba mwaka huu, Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Mtango Mtahiko, alisema takwimu zinaonyesha mwaka 2014 hadi 2017, mifugo 154,944 iliingia na wafugaji 2,284 walitozwa faini kwa makosa ya kuingiza mifugo kwenye hifadhi za taifa.


Naye, Mhifadhi Mkuu wa Senapa, Willium Mwakilema, alisema changamoto ya mifugo iko mashariki mwa hifadhi ya Serengeti, katika Pori Tengefu la Loliondo (LGCA) ambako kuna ongezeko kubwa la wakazi wenyeji kwa kuzaliana, ukuaji wa miji hasa ya Wasso na Loliondo.


Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, eneo la kata saba za Loliondo lina watu 46,340 na mifugo 645,230 na eneo la kilomita za mraba 1,500.


Alisema takwimu zinaonyesha kipindi cha mwaka 2014 hadi Juni 2017, mifugo 9,971 ilikamatwa na kutozwa faini ya Sh. milioni 228,205,000.


Aliainisha kuwa ni mwaka 2014 mifugo 1,954, mwaka 2015 ilikuwa 1,841, mwaka 2016 ilifika 2,430 na mwaka huu Januari hadi sasa 3,746.


Chanzo: Nipashe


 
Nchi hii acha kabisa....40% ni mapori tengefu na hifadhi.....hao wananchi watengewe sehemu zao rasmi za kufuga.....na wengine za kilimo!! Kuna ile tume ya matumizi bor ya ardhi sijui wameanzia wapi tangu wapewe hiyo kazi...awamu hii sijasikia mipango yao...mud mfupi na mrefu!!
 
Back
Top Bottom