Kigwangala afanya mkutano wa hadhara jimboni kwake, vipi katazo la Polisi ni kwa wapinzani tu?

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
DSC_0487.jpg

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka wananchi wa Jimbo lake kuwa na Imani naye kwani yeye ni miongoni mwa “Majembe” ya Rais wa awamu ya tano, Mh. Dk. John Pombe Magufuli hivyo kwa Wananchi wa jimbo hilo kuchagua mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani wameramba dume na watapata fursa mbalimbali kama walivyoahidiwa kipindi cha kampeni.

Dk. Kigwangalla amebainisha hayo katika ziara yake ya kushukuru wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kwa kumuwezesha kumchagua kurudi Bungeni kwa kura nyingi na pia kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani

“Ndugu zangu wananchi wa Kata ya Milambo Itobo na wale wa Kata ya Magengati …Leo narejea hapa kuwashukuru kwa kunichagua kwenu. Nashukuru sana kwani kula zenu zimeweza kuniwezesha mimi kwa mara nyingine tena kurejea Bungeni na kuweza kuwawakilisha nyie katika vikao vya maamuzi hasa vile vya kimaendeleo. Na kutokana na uchapaji wangu wa kazi hata Rais ameniona mimi ni jemba na amenipatia moja ya nafasi za Uwaziri.

ameniteua kwenye Baraza lake la Mawaziri. Napenda kuwapongeza sana na pia naomba niwafikishie salama za Rais kwa kuweza kumpatia kura nyingi sana za NDIO…” Alieleza Dk. Kigwangalla katika mkutano huo wa wazi ambao watu mbalimbali walipata wasaha wa kushuhudia mkutano huo wa kutoa shukrani ambapo pia alitoa misaada mbalimbali ambayo aliahidi yeye mwenyewe kwa moyo wake hasa kwa vijana.

Aidha, Dk. Kigwangalla aliwaomba wananchi wa Vijiji vya Kaloleni kuwa na subira kwani atahakikisha Umeme wa gridi ya Taifa inapita katika vijiji hivyo na kupata umeme wa uhakika ambapo kwa sasa tayari ameliombea hilo na litatekelezwa muda wowote kuanzia sasa.

Mbali na hilo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kuwa na subra kwa kipindi hiki kwani barabara inayoanzia kwenye barabara kuu ya lami ya Tabora kuingia Inagana mpaka Milambo Itobo ambayo hipo chini ya Tanroad, inatarajiwa kukarabatiwa na itakuwa msaada kwa wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao wanajishughulisha na shughuli za Kilimo ikiwemo ulimaji wa vitunguu kwa wingi, Tumbaku, Pamba na Mpunga.

Mbali na kutoa ahadi hizo kwa wananchi hao, Pia Dk. Kigwangalla aliahidi kutoa shilingi Laki tatu kwa vijiji vya Kaloleni, Usagali na Inagana kwa ajili ya kuchangia maswali ya dini

Dk. Kigwangalla pia mbali na kutoa shukrani kwa wapiga kula wake hao, pia alipata wasaha wa kusikiliza kero za wananchi huku akipokea kero zao hizo ambapo ameeleza kuwa atazifanyia kazi

Wananchi waliuliza maswali mbalimbali ikiwemo kupata matibabu licha ya kujiunga na mfumo, barabara mbovu, Umeme.
 
View attachment 366179

Ndiyo!
 
Tusibiri labda mamlaka husika itamchukulia hatua Kali za kinidhamu na kisheria.
 
Acha tu nikuite usiyejua ulichokiandika, Wakuu wa wilaya na mikoa wanawakataza wanasiasa wa mikoa mingine kwenda wilaya zao?
Mbunge gani wa CHADEMA kaomba mkutano wa hadhara Jimboni kwake kanyimwa?PM Majaliwa kasema wazi kabisa kuwa Mbunge anahaki ya kuitisha mkutano Jimboni kwake muda wowote ule

CHADEMA Mbunge wa Arusha Mjini anataka aitishe maandamano Mwanza
Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe anataka kufanya mkutano Mbagala Dar
Warudi ktk MAJIMBO yao na hamna zuio lolote

Tufanye kazi jamani!Siyo kila saa siasa
 
aliomba kibali cha polisi?, inawezekana polisi hawana taarifa hiyo ndilo jibu pekee ninalotegemea.
 
Sasa kufanya mkutano jimboni kwako kuna shida gani!!!? Tatizo linakuja pale mbunge wa jimbo lingine kuanza kuzungukia majimbo ya wengine huko ni kutafuta nini kama sio kujazana chuki na visasi.
Kwa kutumia sheria ipi
 
Mbunge gani wa CHADEMA kaomba mkutano wa hadhara Jimboni kwake kanyimwa?PM Majaliwa kasema wazi kabisa kuwa Mbunge anahaki ya kuitisha mkutano Jimboni kwake muda wowote ule

CHADEMA Mbunge wa Arusha Mjini anataka aitishe maandamano Mwanza
Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe anataka kufanya mkutano Mbagala Dar
Warudi ktk MAJIMBO yao na hamna zuio lolote

Tufanye kazi jamani!Siyo kila saa siasa
mikutano ya kisiasa ni mpaka 2020 hilo tangazo limhusu nani???
 
Mleta mada punguza mihemko,unajifanya huoni kuta za huo ukumbi zilivyonakshiwa kwa rangi zuri na ukumbi una viyoyozi vya kutosha?Acha kupotosha watu,huo ni mkutano wa ndani na ulifanyika katika hotel maarufu hapa Nzega vijijini.
 
Mbunge gani wa CHADEMA kaomba mkutano wa hadhara Jimboni kwake kanyimwa?PM Majaliwa kasema wazi kabisa kuwa Mbunge anahaki ya kuitisha mkutano Jimboni kwake muda wowote ule

CHADEMA Mbunge wa Arusha Mjini anataka aitishe maandamano Mwanza
Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe anataka kufanya mkutano Mbagala Dar
Warudi ktk MAJIMBO yao na hamna zuio lolote

Tufanye kazi jamani!Siyo kila saa siasa
Utakua unaumwa! Hivi neno zuio la kutofanya siasa hadi 2020 lina maana gani? Alichofanya kigwangala pamoja ni jimboni kwake sio siasa ni nini?
 
Hivi Kwa Hiki Unachokitetea Huoni Hata Aibu??. Muda Mwingine Sio Lazma Uchangine.
 
Utakua unaumwa! Hivi neno zuio la kutofanya siasa hadi 2020 lina maana gani? Alichofanya kigwangala pamoja ni jimboni kwake sio siasa ni nini?
Jibu hoja
Ulisoma tangazo la PM?
Weka hapa Mbunge wa upinzani jina lake kaomba mkutano Jimboni kwake kakatazwa

CHASO sijui
BAVICHA sijui
Wana majimbo gani hawa?
 
Back
Top Bottom