Kigugumizi goli la Kichuya,na penati waliyonyimwa Mbeya City.

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,348
5,977
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_IMG-20171106-WA0064.jpg

Goli alilofunga Shiza Kichuya kwenye mchezo wa VPL kati ya Mbeya City dhidi ya Simba limezua mjada mkubwa kwa wadau wa soka wapo wanaosema kabla Kichuya hajapokea pasi kutoka kwa Jonas Mkude alikuwa ameotea (Offside) huku wengine wakisema hakuwa ameotea (alikuwa-Onside). Kila mtu amekuwa akiamini kile anachokiamini kutokana na utata uliopo kabla ya goli hilo kufungwa.

Mkufunzi wa waamuzi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Leslie Liunda kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu zaidi lakini katika maoni yake ameshindwa kusema moja kwa moja kama Kichuya alikuwa offside au onside kabla ya kufunga goli.

“Kamera hazikuonesha vyema, offside inaamuliwa wakati mpira unapigwa si wakati wa kupokea mpira. Picha haioneshi vizuri wakati mpira unapigwa nafasi ya Kichuya ilikuwaje, hivyo tunapaswa kukubaliana na maamuzi ya mwamuzi msaidizi (assistant referee)”- ) Leslie Liunda.

Ukiachana na mazingira ambayo Kichya alifunga goli (yanatajwa kuwa tata) mjadala mwingine unaoendelea ni kuhusu mpira ulioguswa kwa mkono na Jonas Mkudeakiwa kwenye eneo la penati, wapo wanaoamini kwamba mwamuzi alitakiwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penati kutokana na kitendo cha Mkude kuushika mpira lakini wapo wengine wanasema mpira ulifuata mkono.

Nipe maoni yako (unachokiamini wewe) kutokana na matukio hayo mawili yaliyotokea kwenye mchezo wa jana Jumapili November 5, 2017 mechi iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine.
 


Angalia hii video kisha omba moderator wafute huu uzi maana kama ni mtu wa mpira unatakiwa uache kulia lia wakati refa kashatoa maamuzi.

Mechi ikishaisha ndo basi tena, watu wanachukua tatu muhimu, we move on
 


Angalia hii video kisha omba moderator wafute huu uzi maana kama ni mtu wa mpira unatakiwa uache kulia lia wakati refa kashatoa maamuzi.

Mechi ikishaisha ndo basi tena, watu wanachukua tatu muhimu, we move on

Ungeweka pia clip ya goli linalojadiliwa ili tujiridhishe kwamba hizo ni kesi sawa.
 
Ungeweka pia clip ya goli linalojadiliwa ili tujiridhishe kwamba hizo ni kesi sawa.
Point yangu ni kuwa maamuzi ya refa uwanjani ndio ya mwisho na hakuna namna, inabidi ukubaliane na hali tu. Kulia lia mitandaoni hakusaidii kitu.

Mbona katika mechi ya Simba vs Yanga last week refa hakutoa penalty baada ya mchezaji wa yanga kuunawa mpira wakati akiwa anataka kupigwa darizi na Kichuya?

Mnasahau haraka kweli binadamu. Maamuzi ya refa ndio ya mwisho.
 
Si kila mchezaji akiwa pekee yake ameotea.
Wachezaji hucheza offside trick pia wachezaji nao huvunja offside hiyo ikiwa inawezekana mfano unapoivunja lazima upite mbele ya beki siyo nyuma yake. Fuatilia ile videos utaona.
 
Mimi nafurahi haya yametokea. Simba wachane na upuuzi wa kusema wanaonewa. Kwa hali hiyo Mbeya City nao waseme wameonewa?
Tunajua ubovu wa waamuzi wetu. Kuna wakati kila timu itanufaika na kudhurika na maamuzi mabovu. Matopeni jifunzeni kuona pande zote za Shillingi.
 
Offside inavunjwa na mfungaji au inavunjwa na aliye offside???vitu vingine tusipende lawama kwa wahamuz lengo la soka la bongo ni kulikuza katika mpila bora na sio ubabaishaji sio ilimrad ushindi hatutofika tunapotaka kwa stly hiyo
 
Kwann kila anaehoji anaonekana ni yanga? Sijaona kiongozi wa yanga alielalamikia Ila najua kiongozi wa simba ndio alibeba TV kulalamika.
 
Simba ndo wanaoongoza kulialia khs waamuzi.Leo wao wanufaika wanachekelea.Siku zingine Povu linawatoka aheri lile la foma gold!
 
Kama
Point yangu ni kuwa maamuzi ya refa uwanjani ndio ya mwisho na hakuna namna, inabidi ukubaliane na hali tu. Kulia lia mitandaoni hakusaidii kitu.

Mbona katika mechi ya Simba vs Yanga last week refa hakutoa penalty baada ya mchezaji wa yanga kuunawa mpira wakati akiwa anataka kupigwa darizi na Kichuya?

Mnasahau haraka kweli binadamu. Maamuzi ya refa ndio ya mwisho.
Mbona unajishuku Mkuu? Mbona sijasema kwamba lile goli si halali? Mbona hata mimi naelewa kuwa uamuzi wa refa ndiyo wa mwisho? Haji Manara ndiye hayajui hayo, tuseme akiiona video clip hiyo ataelewa? Kwani kungekuwa na ubaya kama ungefanya kama nilivyoshauri, kuweka video za goli la Simba vs. Mbeya City sambamba na ile uliyotuwekea ili tujiridhishe kwamba kweli zote zinaainisha kuwa maamuzi ya refa ndiyo ya mwisho?
 
Mhhh soka letu bhana nje nizaid ya uwanjani acheni kucheza mpira nje kinachoitajika ni mpila bora achana na mambo ya club
 
Back
Top Bottom