Kigugumizi cha Mkama na Nape-Wanakiuka waliyoyasema na kuwekwa katika tovuti ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigugumizi cha Mkama na Nape-Wanakiuka waliyoyasema na kuwekwa katika tovuti ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gracious, Sep 6, 2011.

 1. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  From CCM Website;
  Imetayarishwa...
  11:28:00 28.06.2011
  Kutoka Gazeti la Habarileo

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo.

  Akifafanua kauli hiyo jana mjini Morogro, Mukama alisema uamuzi wa ngazi za juu wa CCM ukishatolewa kuhusu kuvua gamba watuhumiwa wa ufisadi, hakuna kiongozi atakayepuuza kuutekeleza.

  “Ufisadi unasemwa dhahiri na wananchi kwa kuwataja watuhumiwa hadharani wakiwahusisha ana EPA (Akaunti ya Malipo ya Nje ya Benki Kuu), Dowans, ununuzi wa rada na Richmond … na vikao vya chama vimetoa uamuzi.

  “Kilichobaki ni utekelezaji tu…na hukumu ikishatolewa na Mahakama hakuna njia nyingine isipokuwa kutekeleza agizo hilo,” alisema Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizungumzia madai, kwamba anaogopa kutoa barua za kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi.

  Akihutubia mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaomaliza Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Mukama alisema hataogopa kusimamia kikamilifu uamuzi wa chama hicho wa kuwatosa watuhumiwa hao.

  Alisema vitendo vyao vimesababisha CCM na Serikali ichafuke mbele ya Watanzania.

  Mbali na kuwavua gamba, Mukama alisema CCM pia itashughulikia suala la wafanyabiashara wasio waadilifu wanaojipenyeza ndani ya chama hicho, na itapambana na saratani ya kujilimbikizia madaraka na kukiondoa chama hicho katika utegemezi wa matajiri na wahisani wanaokiweka pabaya.

  Alisema, hakuna mwananchi asiyejua kuwa ndani ya CCM wapo viongozi wenye nyadhifa kubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, Rada na kashfa nyingine.

  Katibu Mkuu huyo alisisitiza kwamba ili kukisafisha chama hicho mbele ya jamii na kukifanya kikubalike katika uchaguzi wowote, ni lazima watuhumiwa hao watoswe ili kurudisha imani kwa Watanzania.

  Mukama alionesha katuni aliyodai imemchora hivi karibuni, akiwa na barua mkononi ikionesha kuwa ameshindwa kutoa uamuzi na kusisitiza kuwa uamuzi huo ni wa chama, hivyo utatekelezwa kama ilivyopangwa.

  Awali katika risala ya wanafunzi hao, walitaka viongozi wote wa CCM kujikita kuwaletea maendeleo wananchi, ili baadaye wapimwe kwa kazi zao.

  Wanachama hao waliwataka viongozi wahubiri amani badala ya kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani na kuwataka watumishi wa Serikali kuachana na siasa wakati wakiwa watumishi wa umma.


  Comments
  -Hivi punde CCM Inahangaika kubadili fikra za watu kuwa kuvua gamba sio kuwatosa watu,tofauti na kauli za mkama kama zilivyo kwenye red words,
  -CCM Imeshindwa kuchukua maamuzi magumu katika muda mwafaka kitu kinachozidi kuishushia hadhi kwa wananchi tofauti na wapinzani wao wakubwa CDM ambao majuzi wamechukua maamuzi magumu ya kuwatosa madiwani.
  -CCM Inazidi kudhihirisha unafiki wake na udhaifu wake kama chama dola kushindwa kuchukua maamuzi kwa wale wanaohusika na rushwa kubwa na rushwa ndogo,wanzidi kuwanyenyekea na kuwapa mda zaidi kama vile wanawaogopa.Ni hatari kwa chama tawala kuwa na misimamo hafifu kama hii(legelege).
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watakula Matapishi yao muda si mrefu!!
   
 3. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  CCM ya Mkama na Nape ni mbuzi kwenye gunia wanauziwa watanzania! Hakuna mabadiliko yoyote CCM waingereza wanasema ukimpaka nguruwe lipstik atabaki kuwa nguruwe tu! Hii ndio CCM watanzania tumeishtukia na Igunga ishtukieni!
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mukama na nape wanataka kuwaaminisha watanzania kuwa sasa kuku anaweza kula kicheche.
   
 5. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #5
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyumba ya kobe ni gamba lake hawezi kulivua labda awe marehemu. Hii ndiyo kanuni ya Chama cha magamba, hawavui magamba yao mpaka chama kife. Ee mola, twakuomba magamba wafe kifo chema wasahaulike milele.
   
 6. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  CCM bwana! Kwishney! Ooh, tutawafukuza Mapacha watatu! Napeeee!!! Sasa ndo uelewe kuwa Mzee wa Suti Tano ni Mnafiki na Kigeugeu.
   
 7. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama swala nikutajwa kwenye kashifa za ufisadi ndio sifa ya kuwa gamba la kuvuliwa ccm,Kikwete anasubiri ni ndani ya hicho chama? Yupo kwenye kashfa ya epa na nyingine nyingi! Halafu RA Kushiriki uchaguzi wa Igunga ndio kichekesho zaidi! Vyp si ilidaiwa kuwa hao mafisadi walipunguza kura za ccm 2010?!
   
 8. N

  Nipe tano Senior Member

  #8
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Nina WASIWASI MAGWANDA YANAMALIZA AKILI ZA WAVAAJI MAANA VINYESI MNAVYZUNGUMZA HAPA mhhhh HATA AIBU HAMSIKII? ILIPOTANGAZWA DHANA YA KUJIVUA GAMBA KELEL KIBAO ZILIPIGWA, NA KUPANIA MIDOMO KAMA MAMBA HAPA OOOOH AHTOKI MTU, HAYO YA VUVUZELA LA CCM, MARA NEPI HUYOOOO NKA. KAONDOKA ROSTAM MKAINAMA KAMA MWANAUME KAKATWA KORODALI ZAKE, GHAFLA KAMA MWANAUME ANAYEINGIZWA KIDOLE MMEKURUPUKA TENA NA HOJA SIZIZO NA KICHWA WALA MIGUU....ANGALIENI MAGWANDA HAYOOOOOOOOOOOO. OHOOOOO
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Kazi wanayo hao.
   
 10. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na J'Mosi Rostam Aziz mmoja wa watu waliotakiwa kujivua gamba ataongoza kampeni Igunga, Ona mnataka kufukza watu then mnawanyenyekea kupata msaada kwao
   
 11. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180

  Watu wenye busara wanatumia hoja kujibu hoja na sio kutumia maneno machafu kujibu hoja,nathubutu kusema kuwa hii akili ya kimagamba yenye kutumia masaburi zaidi itawaponza.

  Tunachosema hapa,kama mnajua kuwa hawa watu ni wachafu,ni wezi,mafisadi ,mameiba na wanawachafulia sifa,Kwa nini mnazidi kuwapa mda,ooooh,eti wajifikirie.Leo jamaa akiiba kuku atajuta atakamatwa mda uleule ataswekwa ndani na kesi itasomwa haraka sana.

  Je magamba wanataka kutuambia katika utawala wao,mbaya zaidi ni yule anayeiba kuku na si hawa wezi wakubwa????. Kama huu ndio utawala wa kimagamba,basi ni uthibitisho tosha kuwa sio chama kinachoweza kutukomboa.Magamba mmcechoka,hamna kipya.Saizi mnatumia nguvu ya dola mliyonayo.

  Kuna uwezekano mkubwa hata vijana walioko kule magamba wako kimaslahi zaidi,yaani mategemeo ya kupewa u DC,u RC n.k.

  Angalizo
  Watanzania wa sasahivi hawadanganyiki.They are in the point of No return.Nina uhakika hata kama EL(Richmond) na AC(Vijisenti ) wataondoka magambani.Chama hiki hakitaaminika tena.Kwa sababu they are all corrupted.
   
 12. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  You are very right.Chama makini lazima kiwe consistent.Mmemfukuza mtu kwa kutokuwa mwadilifu,leo mnamtumia mtu huyo asiye mwadilifu kupiga kampeni tena.Ni sawa sawa na kula matapishi yako mwenyewe.

  Tatizo CCM Wanatumia uelewa au tuseme elimu ndogo ya watanzania kuwadanganya.Lakini hili litafikia mwisho tu.Mzee wa suti 5 ana kashfa kibao,Mzee mkapa pia ana kashfa,Mwinyi-Nani hajui alivyouza kipande cha nchi(Loliondo) kwa falme za kiarabu,Nyerere tu ndo alikua mwadilifu.

  We need change,though change can be costful.Sehemu yote mabadiliko huwa yana maumivu yake.
   
 13. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Leo ndio wanabebwa na mabango makubwa kwenye front page kuwa wao ndio nguzo za sisiem AIBU kubwa kwa Nape na Mkama
   
 14. C

  Concrete JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  @Kujivua gamba ilikuwa ni falsafa ya kisanii & never come to work in realistic. Kifupi itakiacha chama cha mapinduzi kwenye matatizo makubwa sana ya ndani kwa ndani (eg. Makovu, Visasi, Kutokuaminiana,Makundi,Aibu kubwa nk.) @Inasikitisha kuona wanasiasa chipukizi ndani ya CCM wakikubali kutumiwa kuhubiri siasa hiyo mbovu (eg.Nape Mnauye, Mwigulu Nchemba) hivyo kufupisha maisha yao ya kisiasa (Political carrier). @Ni vipi vikao vya juu vya chama (NEC, CC) vishindwe kuchukua maamuzi ya kuwavua uanachama watuhumiwa wa ufisadi, kisha iwape muda (siku 90) wapime na wachukue maamuzi ya kuachia ngazi wenyewe!! Kwa mtu mwenye akili timamu haya ni maigizo, vichekesho&mzaha. Sasa tena tunasikia mmoja wapo atakuwepo Igunga (Rostam) kusaidia kampeni za CCM. Kwa ujumla inakera & kutia kinyaa .Lets wait & watch the cinema...
   
Loading...