KIGOMA: Zaidi ya abiria 50 wanusurika kifo baada ya basi kutumbukia katika mto Malagarasi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,713
Zaidi ya abiria 50 waliokuwa wakisafiri kutoka vijiji vya mwambao wa kusini katika ziwa Tanganyika tarafa ya Buhingu wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamenusurika kufa baada ya basi aina ya Saratoga walilokuwa wakisafiria kuelekea mjini Kigoma kutumbukia katika mto Malagarasi wakati basi hilo na abiria wengine wakivushwa katika kivuko cha mto huo.

Mashuhuda wa tukio hilo pamoja na nahodha wa kivuko cha MV Malagarasi wamesema basi hilo lenye namba za usajili T 938 AGQ limetumbukia mtoni baada ya kivuko kutia nanga upande wa pili baada ya kurudi nyuma taratibu huku abiria wote wakiwa wameshuka na kwamba hilo ni tukio la tano kutokea katika eneo hilo hivyo wameiomba serikali kujenga daraja ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea.

Akizungumza katika eneo la tukio, kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha na kwamba jitihada zinazofanywa sasa ni wazamiaji kujaribu kulitoa majini basi hilo.
 
jamani mbona kuna daraja la kikwete katika mto huo au nalo lilikuwa hewa duuu Nchi hii
Daraja lipo kama unatoka tabora kuja kigoma ndio hilo lilizinduliwa na liko poa tu, huko ilikotokea hii ajali hakuna daraja huwa wanatumia kivuko kupitisha magari na watu ni mbali na lilipo hilo daraja unalolifikira ww
 
Kabla hujauliza hilo swali bora ungefanya uchunguzi wa jiografia ya kigoma na ukaona coverage ya mto malagarasi, ungefahamu ni barabara ngapi zinakatiza ktk mto huo usingeuliza swali lako.
Ni rahisi kufanya uchunguzi huo kwa kuuliza humu maanake sio rahisi sana kuzijua hizo barabara kwa kuziona wakati niko km karibu 1000 kutoka huo mto.
 
Daraja lipo kama unatoka tabora kuja kigoma ndio hilo lilizinduliwa na liko poa tu, huko ilikotokea hii ajali hakuna daraja huwa wanatumia kivuko kupitisha magari na watu ni mbali na lilipo hilo daraja unalolifikira ww
Asante wicklef sie wengine hatujui coverage ya mto malagarasi
 
Hivi hakuna daraja jipya limmezinduliwa mto malagarasi hivi karibuni?
Daraja lipo nimepita majuzi tu toka Mwanza kwenda Kigoma. Tatizo mtoa taarifa habari yake haielezi gari ilikuwa inatoka wapi, hii ingesaidia kuelewa zaidi.
 
Hivi hakuna daraja jipya limmezinduliwa mto malagarasi hivi karibuni?
Mkuu RRONDO hilo daraja ni barabara ya kuelekea mashariki mpaka Tabora, sasa hicho kivuko kiko kusini mwambao wa ziwa Tanganyika kuelekea vijiji vya Sumbawanga. Kwa wastani ni barabara muhimu pia ila kiuchumi haina faida sana kwa nchi maskini kama Tanzania
 
Mwenyezi awafanyie wepesi majeruhi wote....inshallah.
Nimesha wahikufika eneo tukio lilipotokea, kwa utaratibu ulivyo pale kila abilia lazima ashuke alipie gharama ya kuvukia na dereva pia analilipia gar lake, so ingekua ngum kwa abilia kubaki ndan ya gar wote lazma washuke, labda hasara ni mizigo iliokuwa ndan ya gar, siamin kama kuna majeluhi pale.
 
Mkuu RRONDO hilo daraja ni barabara ya kuelekea mashariki mpaka Tabora, sasa hicho kivuko kiko kusini mwambao wa ziwa Tanganyika kuelekea vijiji vya Sumbawanga. Kwa wastani ni barabara muhimu pia ila kiuchumi haina faida sana kwa nchi maskini kama Tanzania
Asante.
 
Nimesha wahikufika eneo tukio lilipotokea, kwa utaratibu ulivyo pale kila abilia lazima ashuke alipie gharama ya kuvukia na dereva pia analilipia gar lake, so ingekua ngum kwa abilia kubaki ndan ya gar wote lazma washuke, labda hasara ni mizigo iliokuwa ndan ya gar, siamin kama kuna majeluhi pale.
Shukrani mkuu,je dereva na utingo wapo Salama?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom