Kigoma: Zahanati yafungwa baada ya Muuguzi aliekuepo kupata ujauzito wananchi wahaha kupata huduma!

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Uvinza. Wakazi wa kijiji cha Chakulu, kata ya Uvinza wilayanii Uvinza wamelalamika kukosa huduma za afya baada ya zahanati wanayoitegemea kufungwa kwa zaidi wiki moja, hali inayosababisha usumbufu kwa wananchi.

Hatua hiyo imekuja baada ya zahanati hiyo kuwa na wahudumu wa afya wawili, huku mmoja akiwa likizo ya uzazi na mwingine kutoka mara kwa mara anapohitajika kwenye vikao, hivyo kulazimika kuifunga zahanati hiyo.

Wakizungumza Ijumaa, Juni 25, 2021 kwa nyakati tofauti, wananchi walisema kwa zaidi ya wiki wamekuwa wakipeleka watoto kutibiwa katika zahanati hiyo, lakini wanakuta imefungwa.

Mkazi wa kijiji cha Chakulu, Lusia Maige alisema hali imekuwa mbaya, kwani wamekuwa wakisumbuka kwa kulazimika kutembea umbali wa saa moja kwa kutumia baiskeli akiwa na mtoto mgongoni na kisha kukosa huduma. Alisema hali hiyo inatokana na zahanati hiyo kuwa na mhudumu mmoja kwa sasa, hivyo kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati na kurudi nyumbani mapema.

“Tumekuwa tukitumia siku nzima njiani na kurudi nyumbani bila kupata huduma kwa muda wa wiki moja sasa, kwani kila tukienda tunakuta zahanati imefungwa na tunaambiwa mhudumu amekwenda kwenye kikao,” alisema Maige.

Mkazi wa Chakulu, Joyce Charles alisema hata zahanati hiyo ikiwa wazi mhudumu ni mmoja, hivyo kuna wakati anachoka kutoa huduma kwa kuwa anahudumia watu wengi ndani na nje ya kijijini hicho. “Tunaomba watuongezee wahudumu wa afya, aliyepo ni mmoja huyo huyo ajigawe wodi ya wazazi, watoto na wajawazito. Unakuta inafika muda wa kufunga saa tisa jioni mtu anarudi nyumbani bila kupata huduma. Hili jambo linaumiza, kwani unakuta mtu ameua siku nzima na hajapata huduma ya aina yoyote,” alisema Charles.

Mhudumu wa afya ngazi ya jamii, Chausi Charles alisema kuna wakati wanalazimika kubandika tangazo kwamba hakuna huduma hadi siku fulani.

Hata hivyo, alisema wananchi wanapokea taarifa hizo kwa shingo upande, kwani wanatoka mbali na wanapokosa huduma kusababisha baadhi ya wananchi kukata tamaa na kushindwa kufika kwa ajili ya chanjo na kliniki hasa kwa wajawazito.

“Tangu Jumatatu ya wiki hii zahanati haijafunguliwa na wananchi wamekuwa wakirudi nyumbani, leo ndio amenipa maagizo wakija wagonjwa niwaambie waje Jumanne ya wiki ijayo kwa ajili ya huduma za afya ndio siku atakayokuwepo rasmi,” alisema Charles. Kaimu mwenyekiti wa kijiji cha Chakulu, Hussein Saidi alisema kijiji chake kina vitongoji vitatu ambavyo ni Kagembe, Kitali na Lukaki na vitongoji shikizi ni Ilunde na Tandala ambapo kuna takribani wakazi zaidi ya 30,000 wanaotegemea huduma za afya katika zahanati ya Chakulu.

Alisema Serikali ya kijiji iliongeza majengo kwa kuwahamasisha wananchi kufyatua tofali 15,000 na mchanga kwa ajili ya kuongeza majengo mengine, ikiwemo wodi ya wazazi na nyumba za wahudumu baada ya zahanati hiyo kuwa na jengo moja.

Alisema kuna kipindi wagonjwa wanakuwa wengi katika zahanati hiyo, hivyo inawalazimu kwenda kuchukua wahudumu wa afya katika zahanati ya Uvinza kuongeza nguvu, ili wagonjwa wote watibiwe kwa wakati na tayari wameshatoa taarifa hizo halmashauri ili kuongezewa wahudumu wa afya wengine.

CHANZO : MWANANCHI
 
Kigoma nasikia wachawi ni wengi na kuna waganga wengi wa kienyeji Si waende huko kuliko kuhangaika na hio njoo leo njoo kesho kutwa!?
 
Serikali imeajiri kidogo sasa hivi, huenda wakapata mtoa huduma
 
Mahitaji nchi nzima kada ya afya ni ngapi.
Waliotangazwa niwangapi.
Mtaani hatuna wataalam
Zahanati zimejengwa
Tunataka maendeleo ya watu au ya vitu
 
Uvinza. Wakazi wa kijiji cha Chakulu, kata ya Uvinza wilayanii Uvinza wamelalamika kukosa huduma za afya baada ya zahanati wanayoitegemea kufungwa kwa zaidi wiki moja, hali inayosababisha usumbufu kwa wananchi...
Inasikitisha sana, na pia inatia aibu
 
nchi nzima watumishi wa Afya 2000 ni sawa na kukoroga sukari kwenye bahari ya hindi
Wameanza kuajiriwa baada ya muda mrefu kidogo.....

Mwakani kutakuwa na mwendelezo....

#KaziInaendeleaKwaKasiYaKutisha
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom