Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Wadau, Serikali imetangaza rasmi kusimamisha usafiri wa reli ya kati kwa muda wa miezi sita. Kama hiyo haitoshi, nimepata taarifa kuwa hata usafiri wa mabasi kutoka Kigoma kwenda Dar na mikoa mingineyo kwa sasa haupo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea nchini hali ambayo imepelekea watu wengi walioenda likizo mwisho wa mwaka kukwama kutokana na mkoa huo kubakiwa na usafiri wa ndege moja tu ya ATCL ambayo hufanya safari zake mara sita kwa wiki.
Mwishoni mwa mwaka ulokwisha- Desemba 2009, nililazimika kuondoka kwa basi kwenda Dar baada ya kuambiwa kuwa usafiri wa ndege hiyo moja ya ATCL imejaa hadi tarehe 11 Januari! Kampuni ya Precision Air ambayo pia ilikuwa na ndege inayofanya safari za Dar-Kigoma-Dar Kila kusimamisha safari zake kwa muda usiojulikana kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.
Ni mabasi mawili tu yaliyokuwa yanasafiri kutoka Kigoma Tanganyika, kwenda Dar es Salaam, Tanzania kila baada ya siku mbili- Adventure Bus na Saratoga Bus kupitia Nyakanazi-Kahama-Singida-Dar ambayo nayo yamesimama.
Njia ya barabara ambayo ilitumika kutoka Kigoma kwenda Tabora nayo kwa sasa haitumiki kutokana na kujaa kwa maji kwenye bonde la Mto Malagarasi.
Peace!