KIGOMA; Waziri wa Maji ameagiza kuondolewa kwa msimamizi wa mradi mkubwa wa maji

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Messages
5,249
Points
2,000

real G

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2013
5,249 2,000
Waziri wa maji Mhandisi Isaac Kamwele ameagiza kuondolewa kwa msimamizi wa mradi mkubwa wa maji katika kata ya Nguruka wilayani Kigoma Erick Suma baada ya mradi huo uliokuwa ukamilike mwezi Disemba mwaka jana kutokamilika hadi sasa.

Kamwele.jpg


Waziri Kamwelwe ambaye ametembelea mradi huo amesema msimamizi huyo wa mradi alimdanganya rais alipotembelea mradi huo mwezi wa saba mwaka jana kwa kutoa ahadi ya kukamilika kwa wakati mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni tatu .

Aidha ameongeza kwamba licha ya msimamizi huyo kulipwa fedha zote anazodai kwa mujibu wa mkataba lakini kazi inakwenda taratibu na kuathiri maisha ya wananchi.

Chanzo: EATV
 

Forum statistics

Threads 1,380,809
Members 525,887
Posts 33,780,503
Top