Kigoma: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza Bandari ya Kagunga ambayo imekamilika tangu 2017 kuanza kutoa huduma

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipa wiki mbili kuanzia jana (Ijumaa, Desemba 18, 2020) Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ihakikishe kwamba ifikapo Januari Mosi mwakani Bandari ya kimkakati ya Kagunga iliyoko katika Kata ya Kagunga wilayani Kigoma iwe imeanza kutoa huduma.

“Leo nimekuja hapa kuona bandari, hii bandari ilikamilika mwaka 2017 imekaa tu, nyumba zimejaa popo tu na mle ndani kumejaa takataka na mmefagia jana baada ya kusikia mimi nakuja, hovyo kabisa nawauliza hapa wanajikanyaga tu tuna mtumishi hapa hakuna mtumishi amekuja jana badaa ya kusikia nakuja hovyo kabisa hawa.”

Alitoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Desemba 18, 2020) baada ya kukagua mradi wa bandari ya Kagunga iliyopo kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika, wilayani Kigoma. Waziri Mkuu amechukizwa na kitendo cha bandari hiyo kushindwa kutoa huduma licha ya kuwa imekamilika.

Waziri Mkuu alisema mbali na bandari hiyo ya Kagunga kuanza kazi Januari Mosi, 2021, pia ameagiza soko la kisasa la Kagunga nalo lianze kazi siku hiyohiyo ili kuwawezesha wananchi wa Kagunga waanze kufanya biashara na kuinua kipato chao.

Pia, Waziri Mkuu alishangwaza na kuchukizwa na kitendo cha Meneja wa Bandari kutoka Makao Makuu ya TPA ambaye hajawahi kufika katika bandari hiyo na haijui. “Kama kweli wewe ni Meneja wa Bandari Tanzania bandari zako huzijui na unamiaka chungunzima unafanya kazi gani, hovyo kabisa.”

Waziri Mkuu alisema mradi wa ujenzi wa bandari hiyo ulikamilika 2017 ukihusisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na la mizigo, nyumba ya kuishi mtumishi na jengo maalumu lakini hakuna mtumishi katika bandari hiyo ambayo ujenzi wake uligharimu shilingi bilioni 3.8.

-- PMO
 
kwani unakimbizwa na nani mkuu,si ungetulia tu utupe habari kamili
 
Uwajibikaji . Pale pale angeteua wakazi wa eneo awape na ajira. maana wao ndio wana uchungu na eneo lao.
 
Waziri Mkuu alichofanya Kagunga ni kutema tu Mkwara mbuzi..

Bandari zote kwa sasa zinaendeshwa na Mtu mmoja tu bila shaka kwa maelekezo kutoka Chamwino, huyo Mtu mmoja asiposema jambo hakuna kitu kinafanyika, hata Waziri Mkuu Hana la kumfanya..

The man is too powerful, hakuna cha Bodi wala Waziri wa Uchukuzi wenye Uwezo wa kumfanya lolote, He works on orders Straight from State House
 
tangu 2017 huo ucheleweshaji ulikua unafanywa na serikali ya wapinzani au??

Hakuna lolote hizi ni zile zile senema za Bongo Movie...

TPA kuna madudu mengi na ubadhilifu mkubwa sana. Wanajua siku nyingi lakini hakuna hatua zozote.

Huko kwenye mafuta tu ni balaa, na hata zile kelele za wakati ule sijui mitambo ya kuthibiti wizi likafungwa lkn watu wanaharibu, chokonoa na mambo yanaendelea kama zamani..!! Tunapoteza bilions
na biĺions.
Tume kila siku actions hakuna.

Huyo mhaya hapo, sidhani kama anatofauti na hao walitaka piga Almasi.

Rais wa wanyonge kweli hujui ya wapiga deal mafuta hapo au ?
Tumbua huyo banyamulenge TPA iwe safi
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipa wiki mbili kuanzia jana (Ijumaa, Desemba 18, 2020) Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ihakikishe kwamba ifikapo Januari Mosi mwakani Bandari ya kimkakati ya Kagunga iliyoko katika Kata ya Kagunga wilayani Kigoma iwe imeanza kutoa huduma.

“Leo nimekuja hapa kuona bandari, hii bandari ilikamilika mwaka 2017 imekaa tu, nyumba zimejaa popo tu na mle ndani kumejaa takataka na mmefagia jana baada ya kusikia mimi nakuja, hovyo kabisa nawauliza hapa wanajikanyaga tu tuna mtumishi hapa hakuna mtumishi amekuja jana badaa ya kusikia nakuja hovyo kabisa hawa.”

Alitoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Desemba 18, 2020) baada ya kukagua mradi wa bandari ya Kagunga iliyopo kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika, wilayani Kigoma. Waziri Mkuu amechukizwa na kitendo cha bandari hiyo kushindwa kutoa huduma licha ya kuwa imekamilika.

Waziri Mkuu alisema mbali na bandari hiyo ya Kagunga kuanza kazi Januari Mosi, 2021, pia ameagiza soko la kisasa la Kagunga nalo lianze kazi siku hiyohiyo ili kuwawezesha wananchi wa Kagunga waanze kufanya biashara na kuinua kipato chao.

Pia, Waziri Mkuu alishangwaza na kuchukizwa na kitendo cha Meneja wa Bandari kutoka Makao Makuu ya TPA ambaye hajawahi kufika katika bandari hiyo na haijui. “Kama kweli wewe ni Meneja wa Bandari Tanzania bandari zako huzijui na unamiaka chungunzima unafanya kazi gani, hovyo kabisa.”

Waziri Mkuu alisema mradi wa ujenzi wa bandari hiyo ulikamilika 2017 ukihusisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na la mizigo, nyumba ya kuishi mtumishi na jengo maalumu lakini hakuna mtumishi katika bandari hiyo ambayo ujenzi wake uligharimu shilingi bilioni 3.8.

-- PMO
Kumbe ni kweli wapinzani walituchelewesha yaani wakati wa utawala wao walishindwa kabisa kuendesha hii bandari? Hadi leo chama chetu pendwa Ccm wanaanza mchakato wa kuhakikisha inafanya kazi? Hii nchi ina vituko sana
 
10 Jun 2019
Kagunga, Kigoma
Tanzania

Mandhari ya bandari ya Kagunga

Muonekano wa miundombinu ya gati(jetty), ofisi, ghala ya kuhifadhia (wharf) n.k ktk bandari ya Kagunga mpya ya kisasa mkoani Kigoma ambayo ilijengwa ili kuhudumia nchi tatu

Kasanga, Rukwa
Tanzania

Bandari ya Kasanga mkoani Rukwa ni sehemu ya miradi mkakati ya TPA

Ujenzi Bandari ya Karema wagharimu mabilioni ya shilingi kiTanzania

Ghala (wharf), Quay , reli , barabara kujengwa ktk bandari hii ya kiMkakati wa kuunganisha bandari ya Momba nchini Congo DR inayoangaliana na bandari ya Karema nchini Tanzania, bandari zote hizo zipo ktk mwambao wa ziwa Tanganyika
 
Daa! Issue imekuja wakati mbaya sana. Watu wako likizo wanakula kuku taraaatiiibu, halafu: "Tarehe moja ianze kufanya kazi" Hivi hapo inakuwaje?
 
Miradi hii isiyo kuwa na visheni / maono ya changamoto nyingi ziluzopo ili kuleta faida kwa nchi ni picha halisi ya awamu hii kujaribu kufanya mengi makubwa kwa wakati mmoja bila mpangilio ingawa wameipachika jina kubwa Miradi ya Kimkakati.

Miradi mingi mikubwa imeanzishwa kwa pamoja huku kila mradi ukiwa na changamoto zake za kipekee husika, bandari zingine zinazojengwa hazina barabara wala reli kuunganisha bandari hizo na miundombinu ya usafiri na hivyo kukosa mvuto kwa wafanyabiashara kuzitumia.

Meneja TPA afikishwa Mahakamani kwa kumiliki Nyumba 23, Magari 7

Published on 19 Apr 2018
Leo April 19, 2018 Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prosper Kimaro amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 zisizolingana na kipato chake halali. Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Bilioni 1,178,370,334, zilizopo maeneo ya Temeke DSM na magari 7 yenye thamani Shilingi Milioni 307,364,678.20. Kimaro amesomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja. Wakili Vitalis amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa amelitenda kosa hilo kwa miaka tofauti kati ya 2012 na 2016.

Source: millard Ayo
 
Pwani, Tanzania

Bandari kavu ya Kwala, Pwani

Hii ni mara ya kwanza kwa mojawapo ya bandari za kimkakati ya Bandari ya Kwala iliyopo mkoani Pwani kupokea kontena ambako inamaanisha kuanza rasmi kwa bandari hiyo iliyojengwa ili kusaidia kupunguza mlundikano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na kuchochea Bandari za Kigoma, Kagunga, Karema zilizopo Ziwa Tanganyika na zile za ziwa Victoria kupokea mizigo ya wafanyabiashara wa ndani na nchi jirani za maziwa makuu za Rwanda, Burundi, Congo DR, Sudan ya Kusini na Uganda .

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa treni hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki bandarini hapo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, alisema kuanza kwa bandari kavu ya Kwala ni hatua muhimu katika kumaliza changamoto ya msongamano inayoikabili Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam umekuwa ukisababisha malalamiko kutoka kwa wateja na kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kusimamia mradi huo hadi kufikia kuweza kupokea treni ya behewa.

“Bandari hii inafungua ukurasa mpya na mwanzo wa operesheni za kuondoa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam zoezi ambalo pia litapunguza kuingia kwa malori ya mizigo katikati ya jiji hivyo kupunguza foleni za magari na kulinda miundombinu ya Barabara zetu,” alisema Nditiye.

Alisema amefarijika kuona kazi kubwa iliyofanyika ikiwemo ujenzi wa sakafu ngumu katika eneo kwa ajili ya kuhudumia makasha, ujenzi wa mitaro ya kuzuia mafutiko, miundombinu ya awali ya umeme, maji, Tehama, ulinzi, zimamoto, nyumba za watumishi na ofisi.

Aidha aliiagiza Bodi na Menejimenti ya TPA kuhakikisha bandari hiyo inatumika vizuri na kukamilisha ujenzi kwa kuzingatia vigezo vyote vya ubora.

Pia alitoa changamoto kwa uongozi wa Wilaya ya Kibaha na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kutumia uwepo wa bandari hiyo ya Kwala kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Profesa Ignas Rubaratuka, alisema mradi huo ni matokeo ya dhamira ya dhati ya Serikali ya awamu ya tano kupunguza msongamano ndani na nje ya Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema mradi huo ni utekelezaji wa dhana ya hapa kazi tu ulioanza kufuatia maelekezo ya Serikali baada ya kuona eneo hilo linafaa zaidi kuliko lile la Kisarawe.

Profesa Rubataruka alitoa wito kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania kutumia bandari zilizopo kwani utendaji na usalama umeimarika zaidi.

“Tumeweza kurudisha heshima ya bandari kwa kuongeza ufanisi na kuimarisha usalama na bado tunaendelea na kuboresha bandari za Tanga, Dar es Salaam na Mtwara ili kuweza kuongeza ufanisi zaidi na kuvutia wateja wapya na kurudisha wale wa zamani ambao walituhama,” alisema.

Akielezea utekelezaji wa mradi wa Bandari Kavu ya Kwala, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusidedit Kakoko alisema unatekelezwa kwa awamu katika eneo la hekta 60 ambazo ni sehemu ya hekta 500 za eneo lililotwaliwa na Mamlaka hiyo katika Kata ya Kwala.

Alisema mradi huo ulioanza Februari 2017 unatekelezwa na Mkandarasi Suma JKT kwa gharama ya jumla ya Sh bilioni 47 na unatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu.

Mhandisi Kakoko alieleza kuwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo ilihusisha ufyekaji wa eneo la hekta 120, kulisawazisha, kujaza kifusi, kujaza matabaka ya changarawe na ujenzi wa reli kilomita 1.3 kutoka kituo cha Kwala hadi bandarini hapo.

Awamu ya pili ilihususha kunyanyua tuta kumwaga zege na kuweka reli tano zenye urefu wa mita 500 kila na kuzungusha ukuta wenge urefu wa Kilomita 3.2.

Kakoko alisema awamu hiyo pia inahusisha uwekaji wa miundombinu ya huduma za umeme, maji, mawasiliano na vizima moto pamoja na ujenzi wa nyumba za muda za watumishi na ofisi.

Alisema hadi sasa mkandarasi ameshalipwa Sh bilioni 20.5 sawa na asililimia 45 huku mradi ukiwa asilimia 70 ukitarajiwa kukamilika Julai.

Alisema awamu ya tatu itafuata ambayo ni ujenzi wa barabara ya kilomita 15.5 kwa kiwango cha changarawe ikiwa ni hatua za awali za kuijenga kwa kiwango cha zege. Barabara hii inaunganisha bandari kavu ya Kwala na barabara ya Morogoro eneo la Vigwaza.

Kakoko alisema pia bandari hiyo itaunganishwa na reli ya kisasa ya SGR ambayo itatumika kupeleka kontena mikoani na nje ya nchi.

Aliongeza pia kuwa ujenzi wa bandari hiyo ya Kwala utahusisha sekta binafsi ambao wapewa maeneo ya kuweka ICD’s ndani ya eneo hilo ambapo miundombinu itakuwa inamilikiwa na TPA.
Source : Bandari Kavu Kwala yaanza kupokea mizigo | Mtanzania
 
Back
Top Bottom