mpingauonevu
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 623
- 430
Wakazi wa kigoma mjini wameshangaa kwa nini katibu mkuu wa CHADEMA FR. Wilbroad Slaa kutokuwaeleza sababu za Ndugu Zitto Kabwe kufukuzwa kwenye uongozi wa chama. Wakihojiwa na StarTV kwa nini wamehudhuria kwa wingi mkutanoni wamesema wao wamemlaki Fr. Wilibroad Slaa kama ambavyo wangemlaki kiongozi mwingine wa serikali. Wakitoa maoni yao ya kwa nini wanaamini Ndugu Zitto amefukuzwa, wengi wanaamini ni kwasababu ya vita vya kisiasa kugombea uongozi ndani ya chama.
source:StarTV
My take:
CHADEMA walikubali kumtumia zitto kujenga chama huku wakijua udhaifu wake na haraka yake ya ulafi kutaka madaraka.Kanda ya ziwa na magharibi mwa Tanzania wengi wameingia CHADEMA kwa ushawishi wa kambi ya zitto. Kwa sasa usalama na umoja wa chama ni muhimu sana kuliko kuoneshana umwamba. tuukubali udhaifu wa zitto ili chama kisimame na wakati huo tutafute njia mbadala ya kuufunika umaarufu wa zitto kanda ya ziwa na magharibi ili tutakapomtimua asiwe na athari kama zinazoweza kutokea sasa.
pia CHADEMA wawe makini na siasa za UKWELI ZA UKABILA na ukanda ndani ya chama. Inapotokea kila mchaga na anayetoka mikoa ya kaskazini mwa tanzania ni chadema na kila kiongozi ofisi kuu anatoka kaskazini inatukera sisi wagogo na wengineo. Na inapotokea kila mwenye nia ya kuwa mwenyekiti ikiwa hatoki kaskazini anashambuliwa kuna walakini! inapotokea manispaa kama Arusha madiwani wote kasoro mmoja ni wachaga, hapo kuna walakini. NI KAMA AMBAVYO WACHAGA na wameru WANAJIANDAA SASA KUANZA KUNISHAMBULIA!!!!!