Kigoma washangaa kutokuelezwa sababu za kufukuzwa Zitto

mpingauonevu

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
622
500
Wakazi wa kigoma mjini wameshangaa kwa nini katibu mkuu wa CHADEMA FR. Wilbroad Slaa kutokuwaeleza sababu za Ndugu Zitto Kabwe kufukuzwa kwenye uongozi wa chama. Wakihojiwa na StarTV kwa nini wamehudhuria kwa wingi mkutanoni wamesema wao wamemlaki Fr. Wilibroad Slaa kama ambavyo wangemlaki kiongozi mwingine wa serikali. Wakitoa maoni yao ya kwa nini wanaamini Ndugu Zitto amefukuzwa, wengi wanaamini ni kwasababu ya vita vya kisiasa kugombea uongozi ndani ya chama.
source:StarTV

My take:
CHADEMA walikubali kumtumia zitto kujenga chama huku wakijua udhaifu wake na haraka yake ya ulafi kutaka madaraka.Kanda ya ziwa na magharibi mwa Tanzania wengi wameingia CHADEMA kwa ushawishi wa kambi ya zitto. Kwa sasa usalama na umoja wa chama ni muhimu sana kuliko kuoneshana umwamba. tuukubali udhaifu wa zitto ili chama kisimame na wakati huo tutafute njia mbadala ya kuufunika umaarufu wa zitto kanda ya ziwa na magharibi ili tutakapomtimua asiwe na athari kama zinazoweza kutokea sasa.

pia CHADEMA wawe makini na siasa za UKWELI ZA UKABILA na ukanda ndani ya chama. Inapotokea kila mchaga na anayetoka mikoa ya kaskazini mwa tanzania ni chadema na kila kiongozi ofisi kuu anatoka kaskazini inatukera sisi wagogo na wengineo. Na inapotokea kila mwenye nia ya kuwa mwenyekiti ikiwa hatoki kaskazini anashambuliwa kuna walakini! inapotokea manispaa kama Arusha madiwani wote kasoro mmoja ni wachaga, hapo kuna walakini. NI KAMA AMBAVYO WACHAGA na wameru WANAJIANDAA SASA KUANZA KUNISHAMBULIA!!!!!
 

DCONSCIOUS

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,269
1,500
Mta angaika sana mwakahuu, si kulikua na nafasi ya maswali kwann hawaku muuliza?
 

Roosevelt

Senior Member
Apr 1, 2012
100
0
Hahahaha kaazi kwelikweli kama ww unaepata hata nafasi ya kuoitia humu jf ukadoma na kupost pia umeshindwa kutambua kuwa zito amesimamishwa na hajafukuzwa je bibi yangu kule mwandiga atakuwa katika upande upi.....#teamacademia
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,447
2,000
Hao wote waliokuwa wakizungumza ni maccm hatutawashangaa
maccm ndo wamedandia hii issue ya zito hapa pana jambo
haiwezekani zito afanye kosa alafu maccm ndo wapambe wake wakuu
tena wanamshabikia kwa kufanya hivyo
Watz we have to question on this!
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Wanataka kuelezwa kwani hawajui kusoma wala hawasikii Kiswahili kwenye TV na Redio??? Kuelezwa kitu ambacho unakijua ni upuuzi ambao Slaa hawezi fanya, wakitaka mambo ya namna hiyo waende mikutano ya CCM. Umesikia Mandela alimuuliza JK mbona bado anakua?????
 
Dec 8, 2013
59
0
Huyu ni kipenzi cha wana kigoma(Zuberi Zitto Kabwe)ameleta maendeleo kwa kushirikiana na wabunge wote wa mkoa wa kigoma,watu wanajua juhudi zake na jinsi alivyo mzalendo.Slaa angemumunya tu asingesalimika aliona mbali
 

Victor wa happy

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
11,677
2,000
Eti wameingia chadema kwa ajili ya zzk

in myself huyu msalit hajawahi ni inspire hata cku moja

kna watu makn km mnyka,lema,lisu,mbowe,wenje na wengne wakzungumza unaona kbs anamaanisha

sio huyu msalit zzk
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Ukiona unataka ushauri kwa mambo ambayo unamajibu yake, kwa dhati kabisa hekima yako imeanza kulingana na upumbavuu wako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom