KIGOMA: Wanawake walalamika kukimbiwa na waume zao na kwenda kuoa wakimbizi na kuishi nao huko

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
2576c4f9deb350c2f3419cb84f47e012.jpg
adbca4dbe61774f193afbb5853944b36.jpg
Wanawake wa Kijiji cha Kaziramihunda na Juhudi Kata ya Kasanda wilayani ya Kakonka mkoani Kigoma, wamelalamikia kutelekezwa na waume zao ambao wanatelekeza familia na kwenda kuoa wakimbizi kutoka nchi ya Burundi na kuishi nao katika kambi ya Mtendeli wilayani humo.

Akizungumza katika mkutano wa Kijiji uliofanyika katika kijiji cha Juhudi Kata ya Kasanda Mwenyekiti wa wanawake hao, Tatu Kiuliko alisema Wanaume wengi katika vijiji hivyo vilivyopo karibu na kambi ya wakimbizi wengi wao wamekuwa wakitelekeza familia zao na kwenda kambini kuoa wakimbizi jambo ambalo limekuwa Kero kwa Wamama hao na kumuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuwasaidia kuwarejesha.

Alisema baadhi ya wanawake wameachwa na watoto zaidi ya nane na nyumba zimeezuliwa na mvua ya upepo ilionyesha mwishoni mwa wiki hii, wanashindwa wafanye nini waweze kuwalea watoto wao, mpaka sasa ambapo ni msimu wa Kilimo wanaume hao wapo kambini wanaishi na wakimbizi wakikwepa majukumu yao.
 
2576c4f9deb350c2f3419cb84f47e012.jpg
adbca4dbe61774f193afbb5853944b36.jpg
Wanawake wa Kijiji cha Kaziramihunda na juhudi Kata ya Kasanda wilayani ya Kakonka mkoani Kigoma, wamelalamikia kutelekezwa na waume zao ambao wanatelekeza familia na kwenda kuoa wakimbizi kutoka nchi ya Burundi na kuishi nao katika kambi ya Mtendeli wilayani humo.

Akizungumza katika mkutano wa Kijiji uliofanyika katika kijiji cha Juhudi Kata ya Kasanda Mwenyekiti wa wanawake hao, Tatu Kiuliko alisema Wanaume wengi katika vijiji hivyo vilivyopo karibu na kambi ya wakimbizi wengi wao wamekuwa wakitelekeza familia zao na kwenda kambini kuoa wakimbizi jambo ambalo limekuwa Kero kwa Wamama hao na kumuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuwasaidia kuwarejesha.

Alisema baadhi ya wanawake wameachwa na watoto zaidi ya nane na nyumba zimeezuliwa na mvua ya upepo ilionyesha mwishoni mwa wiki hii, wanashindwa wafanye nini waweze kuwalea watoto wao, mpaka sasa ambapo ni msimu wa Kilimo wanaume hao wapo kambini wanaishi na wakimbizi wakikwepa majukumu yao.
Hii ni kweli kabisa niliwahi shuhudia mmoja kamtelekeza mke na mtoto mdogo kaenda kuoa mkimbizi wa kike huko kumbe dili linakua hivi..
Kule kuna wakati wakimbizi wanakuja chukuliwa wanapelekwa ulaya na america hasa canada huko wakienda huko wanaishi ndani ya uangalizi na kutumikishwa kwa miaka kadhaa alafu wanapewa uhuru kuishi wenyewe hapo ndipo anamchukua na mme wake wa huku anaenda ishi nae kule na hii njia wa kuchukuliwa wakimbizi vijana wengi wakitanzania hasa wa kule kigoma walikuaga wanaingia kinyemela kwenye makambi hayo wakijifanya wakimbizi na kuongea kikimbizi kimbizi wakinyemelea hizo fursa. Hii sijasimuliwa nilishuhudia mwenyewe
 
Umeongea sahihi. Mle makambini kuna wakimbizi wana 10+ years. Uraia wa Tanzania hawautaki, na kurudi kwao hawataki. Wanasubiria safari!
 
Back
Top Bottom