Kigoma: Wanaume walia kunyanyaswa na wake zao, wataka Madawati ya Kuwatetea

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
DSC_0599.JPG

Viongozi na wananchi wa Kijiji cha Murufiti, Nyansha na Kigondo wakiwa kwenye makundi wakijadili mkakati wa kukabili ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwenye jamii za vijiji vyao katika kongamano lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).


Baadhi ya wanaume walioshiriki mjadala wa kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia wameomba kuanzishwa kwa dawati litakaloshughulikia utetezi kwa wanaume kutokana na manyanyaso na vipigo ambavyo kwa sasa wanaume wanavipata kutoka kwa wake zao.

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Murufiti, Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Chada Salum amesema hayo katika kongamano la wazi la wananchi kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia lililoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo alisema kuwa utetezi unaofanywa kwa wanawake umeleta shida kubwa kwa wanaume.

Salum Alisema kuwa historia na vitabu vya dini vinaeleza kuwa mwanaume ndiyo kichwa cha familia lakini kwa sasa wanawake hasa wanaopewa mitaji na serikali na mashirika mbalimbali wamekuwa hawaheshimu waume zao na kufanya mambo ambayo wanajisikia bila kushirikisha waume zao.

“Wanaume kwa sasa tunanyanyasika na wake zetu vya kutosha na ndiyo maana wanaume wanakufa mapema, tunaomba na sisi tupate dawati letu litakalokuwa linawatetea wanaume ili kuepuka vipigo na manyanyaso ambayo wanaume tunapata sasa kutoka kwa wake zetu,” alisema Chada Salum Mkazi wa Murufiti Kasulu.

Akizungumza katika kongamano hilo Mratibu wa vikundi vya taarifa na maarifa , Flora Ndabaniye kutoka TGNP alisema kuwa utetezi unaofanywa na taasisi mbalimbali kuwatetea wanawake haulengi kuwakandamiza wanaume badala yake unalenga kuweka uwiano sawa katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye maamuzi mbalimbali.

Flora alisema kuwa historia ilitawaliwa na mfumo dume ambao ulimnyima fursa na nafasi mwanamke katika kushiriki mambo mbalimbali ikiwemo kuibua na kupanga mipango ya familia na kukuta wanawake wakiathirika kwa kiasi kikubwa na maamuzi yaliyokuwa yakifanywa kwenye familia na sehemu za kazi.

“Naomba niwatoe wasiwasi wanaume kwamba mashirika ya utetezi wa mwanamke hayapo kwa ajili ya kuwafanya wanawake kuwa juu ya wanaume au wanawake kuwa na sauti na amri kwa familia zao bali kuweka uwiano wa kushirikiana kwenye kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali,” alisema Flora.

Naye Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya wilaya Kasulu, Zakharia Gabriel alisema kuwa kampeni na uhamasishaji unaofanywa na taasisi mbalimbali na serikali unalenga kuwaweka wanawake karibu katika kushiriki shughuli mbalimbali za kifamilia, shughuli za kiserikali na kuwezesha wanawake kupata elimu kuondoa mfumo dume.

Gabriel alisema kuwa vipo vituo na vikundi mbalimbali vimeundwa kwenye ngazi ya vijiji na kata kwa ajili ya kupinga ukatili wa kijinsia, malezi chanya kwenye jamii lakini ushiriki wa wanaume umekuwa mdogo na wengi wanaona kampeni hizo kama kuwapa kiburi wanawake bila kuwa na uelewa wa mambo hayo.


Chanzo: Malunde


Pia soma >>> Utafiti: Ukatili wa kiuchumi kwa Wanaume umeongezeka, kunyimwa haki ya kuwa na mtoto pia ni Ukatili
 
Ehh nlijuwa wanaume wa dar

Vp tena wanaume wa mkoani

Juzi juzi geita,leo kigoma tena

Ova
 
Nafikiri kuna haja ya wanaume kuanzisha na sisi aya madawati ya jinsia kwaupande wetu . Hawa wanawake wanapokwenda wanazidi kutupachangamoto
 
Nafikiri kuna haja ya wanaume kuanzisha na sisi aya madawati ya jinsia kwaupande wetu . Hawa wanawake wanapokwenda wanazidi kutupachangamoto
Mmmh! Sidhani kama Kuna haja hiyo, tatizo la Sasa ni kuoana badala ya kuoa wewe kama mwanaume oa Ili kuondoa hii migogoro, panga kabla ya kuoa unahitaji wake wangapi na watoto wangapi utakaoweza kuwaongoza kwenye serikali yako ya familia.
 
Flora amezungumza kinyume nia. Haya mashirika ya giza mbele ya mwanga yamefanikiwa sana ajenda zao kuvuruga mfumo wa ndoa
 
Ukosefu wa heshima na kutojua nini maana ya ndoa na familia ni janga kwa wanawake wengi sasa duniani kote.
Tamthilia zimefanikiwa Sana kumuangusha mwanamke.
Hakuna utii Hakuna ndoa.
Wababe wawili Katu hawakai pamoja ni nature lazima mmoja akatafute pa kupumulia.
 
Saikologia ya wanawake wengi awapendi demokrasia. Wanaume wengi wapole, wastaraabu na waungwana 90% wake zao pasua kichwa. Wanaume madikteta wale wanaoongea neno moja la pili ngumi ndoa zao zipo imara.
Hawa viumbe awapendi kabisa demokrasia. Wanaume wote wanaonyanyashwa ni democratic.
 
Saikologia ya wanawake wengi awapendi demokrasia. Wanaume wengi wapole, wastaraabu na waungwana 90% wake zao pasua kichwa. Wanaume madikteta wale wanaoongea neno moja la pili ngumi ndoa zao zipo imara.
Hawa viumbe awapendi kabisa demokrasia. Wanaume wote wanaonyanyashwa ni democratic.
Wengi wa wanawake huolewa wakiwa wamezidiwa umri na waume zao.Hivyo wanaume huwa wanabaki kupigwa na mshangao anapoona mdogo wake(mke)anamchachafya na kumuonea.
Pili,wanawake wanadekezwa mnoo na sheria.Zinawabeba sana na ndipo wanaume huogopa kutoa muitikio hasi/kupiga au kutoa adhabu Kali na hata nyepesi tu kwa kuogopa matokeo yake.
Jamii imeshamchukulia mwanaume kila muda ni mbabe na mwanamke hujiweka(hujifanya) mnyonge.Hivyo,mwanaume anaogopa hata kutoa onyo la mdomo au kipondo kwa kujua hawezi kutetewa na jamii inayomzunguka na hata jamii ya mbali itakavyopokea taarifa.Woga wa kutoonewa huruma na kupewa haki huzuka.
Kuna wanaume wengine wamezaliwa au kukuzwa katika mazingira ya kutopenda kuuishi ukorofi.Ni wapole tu.Sasa,upole wao huchukuliwa ni uzuzu,uoga,ujinga,ubushoke nk.Hivyo wanabaki kuonewa.Jamii ijikite kujitambua ukweli ili kuepusha upande fulani kupata madhila ya kimwili,kiakili,kiuchumi nk.
 
Wengi wa wanawake huolewa wakiwa wamezidiwa umri na waume zao.Hivyo wanaume huwa wanabaki kupigwa na mshangao anapoona mdogo wake(mke)anamchachafya na kumuonea.
Pili,wanawake wanadekezwa mnoo na sheria.Zinawabeba sana na ndipo wanaume huogopa kutoa muitikio hasi/kupiga au kutoa adhabu Kali na hata nyepesi tu kwa kuogopa matokeo yake.
Jamii imeshamchukulia mwanaume kila muda ni mbabe na mwanamke hujiweka(hujifanya) mnyonge.Hivyo,mwanaume anaogopa hata kutoa onyo la mdomo au kipondo kwa kujua hawezi kutetewa na jamii inayomzunguka na hata jamii ya mbali itakavyopokea taarifa.Woga wa kutoonewa huruma na kupewa haki huzuka.
Kuna wanaume wengine wamezaliwa au kukuzwa katika mazingira ya kutopenda kuuishi ukorofi.Ni wapole tu.Sasa,upole wao huchukuliwa ni uzuzu,uoga,ujinga,ubushoke nk.Hivyo wanabaki kuonewa.Jamii ijikite kujitambua ukweli ili kuepusha upande fulani kupata madhila ya kimwili,kiakili,kiuchumi nk.
Umesema kweli,Jamii tayari ishamuhukumu mwanaume,hata kama mke ndo chanzo cha ugomvi mme kaamua kujitetea katika kujitetea kule akamuumiza mwanamke.Still bado atahukumiwa na Jamii pia atahukumiwa na sheria pia.
 
Umesema kweli,Jamii tayari ishamuhukumu mwanaume,hata kama mke ndo chanzo cha ugomvi mme kaamua kujitetea katika kujitetea kule akamuumiza mwanamke.Still bado atahukumiwa na Jamii pia atahukumiwa na sheria pia.
Sasa,dawa ni kuiepuka jamii ilikwisha kukupa hukumu na kuiepuka serikali itakayokukomoa Kwa sheria kwa kuamua;
-kurara mbere (au)
-kuwa na mchepuko(mke muelewa), au,
-kuachana na hadithi ya kuishi na "mtu mwenye magego yaliyokomaa" na kuishi kiaina bila mke au
-kuishi kwa kununua ngono mitaani.
 
Wanaume wengi
= kuwa na michepuko.
=Kushinda bar zaidi kuliko nyumbani
=Kurudi usiku nyumbani na kuwahi kuondoka alfajiri
=Kuwa mbali mda mwingi nje ya familia kwa kisingizio cha ubize.
=Kuwa walevi mbwa
=Kufa mapema
=Mabosi kuwa wanoko ofisini
=Hasira maofisini
=Ukorofi na ugomvi
=Magonjwa ya moyo, pressure,kupooza,kisukari
=nk
Yoote haya chanzo kikuu huwa ni wanawake, chunguza mwanaume yeyeto mwenye hulka hizo ni lazima nyumbani hakupo sawa mwanaume anakimbia kelele.
"Aliyeimba " No woman no cry " aliona hayo.
Ipo haja somo la watu kufunzwa jinsi ya kuishi na watu lifundishwe shuleni, maana kuna watu wanatabia ngumu.
Mke mwema hawezi kuwa na kelele, maana kelele ukaa kwa mke mpumbavu.
 
MWANAMKE MPUMBAVU HUPIGA KELELE.

Kabla hatujatafuta mchawi wa mahusiano yetu, tunapaswa kujichunguza sisi wenyewe kwanza tupo sawa au tuna shida mahali ila hatujui kama hilo ndilo linatufanya tushindwe kuwa na amani kwenye mahusiano yetu.

Ukiwa kama binti, unaweza usiwe na tabia zingine mbovu unazojua wewe kama vile zinaa ila ukawa na kitu hichi, "kelele/makelele" unashangaa kila baada ya muda fulani mahusiano yako ya urafiki/uchumba yakikaa huwa yanavunjika.

Unaweza ukapata bahati ya kuambiwa shida yako na aliyekuacha, baada ya kukuonya mara nyingi huko nyuma, ama unaweza kuachwa kimya kimya bila kuambiwa shida yako ni nini.

Ukiwa kama mke, unaweza kuharibu ndoa yako kwa sababu hii, "kelele/makelele" kwa mume wako. Hasa ukiwa umeolewa na mwanaume ambaye hajasimama vizuri kwenye imani, na ambaye hajaokoka.

Ni rahisi sana mwanaume kuchoshwa na mke mwenye makelele/kelele, na kutoka nje ya ndoa yake. Sio njia ya kumaliza tatizo ila kwa mwanaume ambaye hajaokoka kwake haiwezi kuwa tabu kufanya hivyo.

Tunaweza kulalamika sana kuhusu waume zetu wanaochelewa sana kurudi nyumbani ila ukweli ni kwamba, kelele zetu ndio zinawafanya waume zetu waone ni heri kuchelewa nyumbani, kuliko kuwahi nyumbani ukakutana na kelele zisizo na mwisho.

Japo kuchelewa nyumbani hakuwezi kuondoa tatizo, wanaume wengi huona njia hiyo inawasaidia wao kuepuka kelele za wake zao. Sasa huko nje huwezi kujua huyu mwanaume anashindia wapi.

Ndio maana wanawake wengi huanza kuhisi vibaya waume zao, kwa kuwaambia wana wanawake wengine nje. Si unajua kusingiziwa kila siku kitu ambacho hukifanyagi huwa inauma na mtu mwingine inaweza kumwathiri. Na kuamua kufanya kweli, hasa kwa yule asiye na hofu ya Mungu ndani yake.

Kelele zisizoisha ndani ya ndoa zinaweza kuharibu kabisa ndoa ile, wawili hawa wanaweza kuonekana kwa nje wapo pamoja ila ukweli humo ndani hawapo pamoja.

Hebu tuangalie maandiko matakatifu yanasemaje kuhusu hili, huenda umepata ukakasi wa hili fundisho kutokana na kichwa cha somo hapo juu.

Rejea: Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.MIT. 9:13 SUV.

Mwanamke yeyote anayepiga sana kelele ni mpumbavu, na ni Mjinga, yaani ana sifa zote mbili, ya upumbavu na ya ujinga. Tena andiko likaongeza mkazo zaidi, HAJUI KITU.

Kwa lugha nyingine mwanamke wa namna hii, huwa mjuaji sana, kila kitu yeye anajua, yupo juu kwa kila kitu, kujishusha kwake ni hakuna. Mume wake hakuna anachoweza kuzungumza akaeleweka, yeye ni anachojua sana ni kelele.

Wanawake wa namna hii, huwa wanakimbilia wapewe haki SAWA, yaani 50 kwa 50, si unakumbuka ni kwa sababu HAWAJUI KITU! Ni andiko limesema hivyo, wanaojua kitu hawezi kupigizana hizo kelele.

Rejea: Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.1 KOR. 11:3 SUV.

Kichwa cha mwanamke ni mwanaume, na sio kichwa cha mwanaume ni mwanamke... huu sio ukabila. Maana kuna watu hawachelewi kusema huo ni ukabila/utamaduni wa watu fulani, hili ni andiko ndani ya Biblia.

Wanawake mtaponya ndoa zenu wenyewe, acheni kelele ndani ya nyumba zenu, ndoa inajengwa kwa hekima ya kiMungu iliyo ndani yako. Si kwa kelele zako ndani ya nyumba.

Rejea: Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. MIT.14:1 SUV.

Wasiosikia, endeleeni kuzibomoa ndoa zenu wenyewe huku mkilalamikia wanaume, utasema wewe hujui tu ninayoyapata, kwani wakati unaolewa naye hukujua hayo. Si hadi kuna watu walikuja kukunasua ukaona wanakufuatilia maisha yako! Basi tulia, acha kelele.

Tena tabia yake mbaya ulikuwa unaiona kwake ukasema Mungu atambadilisha akiwa ndani ya ndoa, kwa hiyo Mungu ameshindwa hiyo kazi? Jibu ni kwamba, ujuaji wako, upumbavu wako, Ujinga wako, na kutokujua kwako ndio kulikuingiza kwenye mahusiano yasiyo yako. Acha kelele.
 
Back
Top Bottom