Kigoma: Wanafunzi 5,400 hawataweza kuanza Sekondari kwa uhaba wa madarasa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Shule za Sekondari zilizoko mkoani Kigoma zinakabiliwa na uhaba wa madarasa 109 hali ambayo inafanya watoto 5,400 waliomaliza sekondari mwaka 2020 kushindwa kuanza kidato cha kwanza.

Shule za msingi na sekondari zinatarajiwa kufunguliwa Jumatatu, Januari 11. Mkuu wa wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko amesema wanaendelea kushirikiana na wananchi katika kujenga vyumba vya madarasa.

Wanafunzi ambao walipaswa kuanza kidato cha kwanza wanalazimika kusubiri hadi vyumba vya madarasa vikamilike. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye ametaka mpango wa ujenzi wa madarasa kuwa endelevu.
 
Kila shule Tanzania ilazimishwe, ^ITAKE, ISITAKE^ imchukue mwanafunzi mmoja wa ziada, wagawane hao 5400 wanafunzi hawa wapate haki yao.

cc: Mh. Suleiman Jaffo (Mb)
Ndiyo maana wazungu wanatucheka sana,miaka 60 ya Uhuru bado mnawaza vyumba vya madarasa,
Hao wanafunzi wapo shuleni miaka 7 na elimu ya msingi ni kuanzia Darasa la kwanza mpaka kidato Cha nne.
Hivyo kwa watu wenye akili timamu lazima idadi ya wanafunzi wanaomaliza na kuingia kidato Cha kwanza wanajilikana,inakuwaje kuwe na upungufu wa madarasa ?
Au mpaka waje wawekezaji?
 
Attachments

  • 20201124_182411.jpg
    20201124_182411.jpg
    21.4 KB · Views: 2
Ndiyo maana wazungu wanatucheka sana,miaka 60 ya Uhuru bado mnawaza vyumba vya madarasa,
Hao wanafunzi wapo shuleni miaka 7 na elimu ya msingi ni kuanzia Darasa la kwanza mpaka kidato Cha nne.
Hivyo kwa watu wenye akili timamu lazima idadi ya wanafunzi wanaomaliza na kuingia kidato Cha kwanza wanajilikana,inakuwaje kuwe na upungufu wa madarasa ?
Au mpaka waje wawekezaji?
Wazungu wanatucheka kwamba kila kitu mpaka tuwapigie wao mfano wa kuwaaminisha watu mazungumzo yako as if wao ndio rubber stamp ya reliability & credibility
 
Shule za Sekondari zilizoko mkoani Kigoma zinakabiliwa na uhaba wa madarasa 109 hali ambayo inafanya watoto 5,400 waliomaliza sekondari mwaka 2020 kushindwa kuanza kidato cha kwanza.

Shule za msingi na sekondari zinatarajiwa kufunguliwa Jumatatu, Januari 11. Mkuu wa wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko amesema wanaendelea kushirikiana na wananchi katika kujenga vyumba vya madarasa.

Wanafunzi ambao walipaswa kuanza kidato cha kwanza wanalazimika kusubiri hadi vyumba vya madarasa vikamilike. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye ametaka mpango wa ujenzi wa madarasa kuwa endelevu.
UCHUMI WA KATI
 
Wapelekwe shule wasome kwa shift wengine waende saa 1 had 6.. wengine waingie 7 had 12. Huku madarasa mapya yakijengwa.
Kila mdau wa elimu ajitolee kujenga shule moja au madarasa kadhaa ili kuokoa kisomo nchini. Wakati wa JN nadhani wenye elimu walihimizwa kuwafundisha wale ambao hawakuwa wanajua kusoma wala kuandika.
 
Sio Kigoma peke yake, hata Dar es salaam bado Kuna wanafunzi wameachwa wengi. Mpwa wangu amepata wastani wa 'B' mpaka leo hajapata shule.
 
Back
Top Bottom